Tafuta

Majonzi yalitowala baada ya kuvumbuliwa kaburi la alaiki ya watoto Asilia huko Canada. Majonzi yalitowala baada ya kuvumbuliwa kaburi la alaiki ya watoto Asilia huko Canada. 

Papa atakutana na watu wa asilia kutoka Canada

Kwa mujibu wa Msemaji wa vyombo vya habari Vatican Dk. Bruni, Papa Francisko atakutana na wawakilishi wa Watu wa Asilia wa Canada,wakisindikizwa na Maaskofu wao mnamo tarehe 28 na 31 Machi 2022.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Vyombo vya habari Vatican, Dk, Matteo Bruni, amebainisha kuwa k tarehe ya 28 na 31 Machi 2022, Papa Francisko atakutana binafsi na kuzungumza na wawakilishi wa watu asilia wa Canada, wakisindikizwa na maaskofu wao, ili kusikiliza mmoja mmoja ushuhuda wao. Mnamo tarehe Mosi Aprili katika Ukumbi wa Clementina kwenye Jumba la Kitume, watakuwa na mkutano, kwa wote washiriki na wawakilishi tofauti na Baraza la Maaskofu wa Canada ambao wakati wa mkutano huo ambapo Papa atakuwa na la kuzungumza nao. Mkutano wao unajikita katika mchakato wa safari ya uponyaji na maridhiano ulioanzishwa huko Canada ili kutoa utambuzi wa haki kwa waathirika wa kile kilichoitwa shule za bweni. Kwa maana hiyo zitakuwa siku tatu ambazo zitakuwa za mkutano na kusikiliza sura ya uchungu wa wakati uliopita ili kuweza kutembea kwa pamoja katika kuelekea uponywaji.

Kumbu Kukumbu ya Watu asilia huko Kamloops nchini Canada
Kumbu Kukumbu ya Watu asilia huko Kamloops nchini Canada

Tarehe Mosi Aprili 2022, mkutano huo utafanyika katika Ukumbi wa Clemetina katika Jumba la Kitume Vatican, kwa washiriki wote pamoja wa wawakilishi tofauti, na Baraza la Maaskofu wa Kanisa, wakati ambapo Papa ataweza kuzungumza nao kwa pamoja. Tarehe 29 Machi 2022 ni siku ambayo imetolewa kwa ajili yao kutembelea Makumbusho ya Vatican. Mkutano huo ulikuwa ufanyike mnamo Desemba iliyopita, lakini uliahirishwa kutokana na janga la Uviko. Ziara ya Wawakilishi wa watu Asilia inaingia katika mchakato ulioanzishwa na Baraza la Maaskofu Canada na Baraza Katoliki la Kanada la Asilia (Ccic), katika muktadha huo wa uchungu, taasisi za shule za serikali wa Kanisa kati ya mwisho wa mwaka 1800 na miaka ya mwisho 1900 wakitaka watoto wa asilia weweze kufanana kiutamaduni. Shule za Bweni zilikuwa zimekabidhiwa kwa makanisa ya Kristo mahalia miongoni yakiwa ni Katoliki. Katika Katika shule hizi zilizokuwa zinafadhiliwa watoto mara nyingi walipata mateso na nyanyaso.

Kumbu kumbu ya Shule ya Bweni kwa watoto Asilia huko Kamloops nchini Canada
Kumbu kumbu ya Shule ya Bweni kwa watoto Asilia huko Kamloops nchini Canada

Itakumbukwa kwamba Papa Francisko alishtuka sana na kuwa na uchungu wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana mnamo tarehe 6 Juni 2021 mara baada ya kujua taarifa hiyo kwa namna ya pekee ya taarifa ya kukuvumbuliwa kwa kaburi la alaiki la watoto 215 wa Shule ya Bweni ya Wahidi ya Kamloops.

24 March 2022, 17:41