Tafakari ya Kard.Czerny:'Niliona vita katika macho ya wakimbizi'
Na Angella Rwezaula – Vatican
Kuanzia trehe 8 hadi 11 Machi 2022, Kardinali Michael Czerny SJ, Mwenyekiti wa muda wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu alitembelea nchini Hungeria ili kuwapelekea wakimbizi wa Ukraine na wale wote ambao wanawapokea mkumbatio na baraka ya Papa. Alipofikia huko Budapest baadaye alikwenda huko Mashariki ya Barabás, sehemu muhimu ya mpaka wanapofikia wakimbizi wanaotoka Ukraine. Kuanzia hapo aliweza kwenda mbele kwa kilometa kadhaa katika eneo la Ukraine hadi kufika mji wa Berehove. Katika maoni yake kuhusiana na nafari hiyo ya mkumwakilisha Papa amesema aliona vita, sio moja kwa moja kwa sababu eneo alilofikia lilikuwa bado halijaanza mgogoro. Aliona katika macho ya wanawake na wanaume aliyokutana nao, watu ambao wametolewa katika mizizi yako, wanahangaika, ambao wambeba mikoba na mifuko waliyokimbia nayo. Kwa namna nyingine wamepoteza mengi na maisha na zaidi vita vimewaondolea na wakati huo huo bado hawajaanza kujenga lolote.
Maoni yake baada ya ziara hiyo Kardinali Czerny amebainisha kuwa “ Katika hilo, unaweza kwa hakika kuelewa vema wahamiaji wageni ambao idadi kubwa waliokuwa Ukraine walikuwa ni wanafunzi wapatao 75,000, kutoka bara la Afrika, Asia na Amerika Kusini. Hata wao walikimbia pamoja na watu wa Ukraine, hata wao waliokuwa na mfuko au saduku japokuwa hawakupoteza maisha, lakini waliweza kukumbana na matukio ya ubaguzi wakati wa safari yao. Sehemu kubwa ya wakimbizi ni wanawake na watoto, wakati huo kwa ajili yao, kuna hatari kubwa ya biashara ya wanadamu. Zimefika historia za ulimwengu wa kisovitiki aambazo walikuwa wamejifunza kukabidhi kila kitu katika mikono ya umma na serikali kwa namna ya kuandaa mabasi ya serikali, lakini kwa kufanya mchezo mbaya wa biashara mbaya na ambao wengine kwa magari binafsi walikuwa wakiwapa usafiri wa bure na kumbe ni watu wabaya”.
Kardinali Cerny akiendelea na mazungumoz hayo amebainisha jinsi ambavyo hakuona hilo tu, lakini zaidi aliona kitu kingine, yaani watu wengi ambao wanajikabidhi kufanya amani, wanawakaribia wakimbizi wakati maaskari wanafanya vita, mara kadhaa kwa mbali, wakitazama skrini za komputa, kwa sababu wanapinga vita vya kiteknolojia. “Ni jeshi la kweli la amani ambalo limejipanga kwa ajili ya mipango ya kukaribisha na mshikamano, katika ngazi mbalimbali. Kuna mshikamano wa Mataifa, ambayo kwa muda wa siku chache yameweka miundo msingi na kurekebisha taratibu zinazoruhusu kuingia kisheria kwa wakimbizi, ambayo hutoa mabasi au kuruhusu usafiri wa bure kwa treni; kuna ya viongozi wa umma wanaofanya shughuli hizo. Baadaye kuna mshikamano ulioandaliwa na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Makanisa na jumuiya za kitawa kwa wale wote waliokuwepo katika eneo nililotembelea”.
Kardinali Czerny aidha amebainisha kuwa hawa ni “Wakatoliki wa utamaduni wa Kilatini na Mashariki, Waorthodox, Waprotestanti na Wayahudi na wenye uwezo wa kushirikiana katika roho ya uekumene wa vitendo”. Kwa mujibu wa Kardinali amethibitisha kuwa “Kilichonivutia zaidi ni mshikamano wa moja kwa moja wa watu wa kawaida. Kwa watu wa Hungeria, kiukweli, lakini pia wa watu wengi niliokutana nao, ambao walikuja kutoka Italia, Ubelgiji, na Uhispania ...: hawa wote waliacha kile walichokuwa wakifanya na wakaweza kuendesha gari kwa maelfu ya kilomita, kwa gharama zao wenyewe, kufika huko. Walifika Mpakani mwa Ukraine kupakua misaada ambayo walileta na kupakia watu ambao wangewakaribisha nyumbani kwao. Nimeona Ulaya yenye uwezo wa kuweka kando vizingiti na hofu, yenye uwezo wa kufungua milango na mipaka, badala ya kujenga kuta na ua. Nimeona Watu wa Ulaya bado wana uwezo wa kuwa na tabia kama ya Msamaria Mwema, wakipakia kwenye magari na mabasi sio tena juu ya farasi au punda, wageni waliokutwa nusu maiti, kando ya barabara zinazoelekea mpakani. Ninaomba kwamba, mara tu mgogoro huu utakapomalizika, Ulaya na watu wake wa Ulaya wasitarudi nyuma, lakini wabaki wazi na wakaribishaji!”
Kardinali Czerny amesisitiza kwamba “Kwa ufupi, niliona Ndugu wote wakiwa katika matendo, katika mikono na nyuso za watu, katika matendo yao na kwa maneno yao. Nadhani kama Kanisa tunayo kazi kubwa ya kufanya hapa: wakati Vatican na diplomasia yake inaendelea kutafuta njia za kumaliza mzozo huo, na kujitolea wenyewe kama wasuluhishi, katika ngazi nyingine lazima tujitoe kuunga mkono na kuimarisha, juhudi hizi za mshikamano. Itahitajika kwa sababu mgogoro unaweza kurefushwa, lakini zaidi ya yote kwa sababu mara tu amani ikirejeshwa, mshikamano uleule, pengine hata mkubwa zaidi, utahitajika ili kusinikiza watu kurudi nyumbani, ili waweze kurudisha maisha ambayo wanayo sasa, inaonekana wamepoteza, kushinda huzuni, majeraha na mateso kwamba vita kuondoka katika eneo la Ukraine na kujenga mustakabali wa amani kwa nchi ya mtu”.
Kwa msisitizo huo amesema “Jitihada za wanaume na wanawake wa Ukraine tayari zimeanza. Niliporudi Roma, waliniambia kuhusu tukio lililotokea huko Medyka, mji wa mpaka wa Poland. Baadhi ya wafanyabiashara walijaribu kuwashawishi wanawake waliokimbia kupanda mabasi mawili ambayo yangewapeleka hadi Denmark, ili kuwaweka kwenye pete ya ukahaba. Wanawake wengine wa Kiukreni, ambao tayari wanaishi Poland, waliomba kutazama utambulisho wa wafanyabiashara hao haramu, ambao walitoweka kwa haraka. Kwa sasa Wanawake wa Kiukreni wanajipanga ili kuzuia matukio kama haya kutokea tena. Tunaweza kufikiria tu kile watakachosimamia mara tu watakapoweza kurudi nyumbani, wakiwa na roho ile ile na azimio saw”a. Amesema Kardinali.
Kwa kuongeza na kuhihitimisha Kardinali amesema: “Ili kuipa Ukraine mustakabali, ni muhimu kwamba silaha zao zinyamaze, lakini hiyo haitoshi: wakimbizi wanahitaji kurudi, na zaidi kurudi kazini, kurudi shuleni ... Nchi haiwezi kuishi bila wananchi wake! Wiki iliyopita niliondoka kenda kwenye mamombi, unabii na laana. Hivyo ndivyo ilivyokuwa. Lakini kwa kurudi ninaweza kusema pia ilikuwa safari ya ushuhuda, upendo na matumaini. Kwa roho hii, na sasa ninaondoka kuelekea Slovakia”. Amebainisha hayo Kardinali Czerny, Mwenyekiti wa Muda wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu mara baada ya kurudi kutoka Hungeria na kabla ya kuondoka tena kwenda Slovakia katika utume mwingine.