Tafuta

Msaada  unahitajika Msaada unahitajika 

Krajewski:Mwakilishi wa Papa kwenda ukraine kupeleka msaada na baraka!

Msimamizi wa sadaka ya Kitume amekwenda Poland katika muda wa saa chache zijazo ili baadaye kuhamia nchi iliyozingirwa na kutekeleza utume wa kuunga mkono idadi ya watu na wa kujitolea wanaosaidia wakimbizi:"Sijui ni wapi ninaweza kwenda,lakini nitajaribu.Kumwonesha mtu yeyote ninayekutana naye ukaribu na faraja ya Baba Mtakatifu.Siogopi,ninafikiria Injili."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ratiba ya safari haina uhakika, lakini lengo liko wazi kwa ajili ya kuwafikia watu wanaoteseka na kuwaonesha ukaribu wa Papa, kwa kuwaeleza kwamba anawapenda na kusali kwa sababu sala pia ina uwezo wa kusimamisha vita. Amesema hayo Kardinali Konrad Krajeswki, Msimamizi wa Sadaka ya Kitume Vatican ambaye tayari alikwenda katika Kanisa kuu la Roma la Mtakatifu Sofia mnamo tarehe 3 Machi 2022 kupeleka vifurushi vya misaada kwa ajili ya jumuiya ya Kiukraine. Hata hivyo ni mmoja wa  makadinali wawili ambao Papa Francisko anawatuma kwenda Ukraine kutoa msaada na msaada wa kiroho kwa idadi ya watu ambao wameishi chini ya mabomu na vitisho kwa siku kumi na moja sasa. Pamoja na Kadinali, huyo kuna hata Kadinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa Muda wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu.

Huu ni ujumbe wa kweli ambao, kama Papa alivyo sema kwenye sala ya Malaika wa Bwana, unataka kuonesha kwamba Vatican iko tayari kufanya kila kitu, kujiweka katika huduma ya amani hii.  Zaidi ya yote, uwepo wa makadinali wawili huko sio uwepo wa Papa tu, lakini kama wawakilishi wa Wakristo wote wanaotaka kukaribia na kusema: 'Vita ni wazimu! Acha, tafadhali! Tazama ukatili huu!”

Msimamizi wa kitume akieleza juu ya safari hiyo amesema: “Baba Mtakatifu anatumia mantiki ya Injili na kuwasogelea wagonjwa, wanaouawa, waliohamishwa kutoka katika nchi zao. Ninaondoka hivi karibuni na ninaenda Poland, kwa sababu kutoka Poland nina hakika nitaweza kuingia Ukraine. Kisha tutaona ni umbali gani tunaweza kuwafikia watu hawa na kuonesha ukaribu wa Papa, kusema kwamba anawapenda, kwamba anawaombea, kwamba anataka kuwatia moyo. Pia ninaondoka kuwasilisha Rozari za Baba Mtakatifu ili kwa maombi tuweze kuhamisha milima na hata kuacha vita.

06 March 2022, 15:00