Leo tunaweza kuchagua maisha au kifo cha ubinadamu
Sergio Centofanti
Leo kuliko wakati mwingine wowote ule wa ubinadamu una hatima yake mikononi mwake: unaweza kuchagua maisha au kifo. Hali halisi ndiyo: tunakabiliwa na mzozo ambao unaweza kuwa na matokeo mabaya kwa ulimwengu. Matarajio yetu ni kuona kwamba wale walioufungua wanajikuta zaidi na zaidi peke yao. Ubinadamu unataka kuishi.
Huko New York, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lililaani vikali uvamizi wa Urusi. Huko Geneva, karibu wawakilishi wote wa mataifa mbalimbali katika kikao cha Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa walitoka nje ya chumba wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi ulipoanza hotuba yake: picha yenye muktadha mkubwa ambayo inalaani kama ilivyo nje ya historia dhidi ya nchi huru. Urusi imefukuzwa kutoka katika matukio makuu ya michezo na kisanii, imetengwa na mfumo wa kifedha wa kimataifa na usafirishaji wa kimataifa. Kwa bahati mbaya, vurugu za shambulio hilo zinakuwa mbaya zaidi na za kutisha zaidi.
Hofu na maumivu vinaongezeka kati ya Waukraine kwa mauaji ya wasio na hatia yaliyosababishwa na mchokozi, lakini pia ujasiri, upinzani, uimara, umoja wa watu na mshikamano wa ubinadamu unazidi kuongezeka. Tumaini ni kuona kwamba mshikamano wa mbele wa Urusi unazidi kuvunjika: makuhani wengi wa Kiorthodox wa Urusi wameshutumu waziwazi vita, kama vile wanasayansi, wasomi, wasanii na wanamichezo. Na wapo nchini ambao wanaoendelea kuingia mitaani kuandamana dhidi ya mzozo huo, hata kwa kuhatarisha maisha yao binafasi. Matumaini ni kwamba sauti hizi za amani ziweze kukua zaidi na zaidi.
Utawala unazidi kutengwa. Kwa bahati mbaya, vurugu za mashambulizi zinaongezeka. Raia wanapigwa mabomu, majengo ya makazi, shule, hospitali, makanisa yanapigwa mabomu. Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu imefungua uchunguzi wa uhalifu wa kivita. Katika kutengwa huko, vitisho vinakuwa hatari zaidi. Maonyo hayo yanaangazia, karibu usaliti: hatari ya vita vya nyuklia ambavyo havitaacha ulimwengu wala washindi au walioshindwa. Kiukweli wazimu wa vita ni wa kishetani: inataka uharibifu tu.
Somo la kwanza la siku ya Alhamisi baada ya Jumatano ya majivu, kulingana na ibada ya Kirumi, limetukumbusha kwamba mwanadamu ana uhuru wa kuchagua kati ya maisha na kifo (Kum 30: 15-20). Tunaweza kumtii Mungu wa wema na huruma au sanamu za ubinafsi, kiburi na jeuri. Tutakuwa na tunachofuata. “Kumbuka mwisho wako na uache kuchukia” kifungu kutoka kitabu cha (Sir 28,6) kinasema. Mwisho ni furaha ya milele ambayo Mungu anataka kwa viumbe wake. Lakini tunahitaji kuongokea upendo na haki. Tuko huru. Tuna uzima na kifo mbele yetu. Je, tutakuwa wazimu kiasi cha kuchagua kifo?
Kwaresima ni wakati mzuri wa uongofu. Wakati wa maombi ya kina zaidi. Raia wa Ninawi ilionekana kuwa haiwezekani walipokabiliwa na mahubiri ya Yona, waliondoa kazi za uovu na hawakupata uharibifu bali amani. Tumaini ni kwamba hata leo wale wanaopanda uharibifu hatimaye watakataa uovu na kuchagua uzima. Tumaini ni kwamba sote tunaweza kupinga chuki. Leo hatima ya wanadamu wote iko hatarini.