Kard.Krajewski huko Lviv:Amekutana na mkuu Shevchuk na Mokrz
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Kanisa Katoliki la Kigiriki la Ukraine, limebainisha kuwa Kardinali Krajewski yuko tayari Lvic nchini Ukraine ambapo amekutana na tarehe 8 Machi 2022 na Sviatoslav Shevchuk Mkuu wa Kanisa, katoliki la kilatini, Padre wa Kanisa Katoliki la Kigiriki na Mieczyslaw Mokszycki, Mkuu wa Kanisa la Lviv. Kwa maana hiyo Kardinali amethibitishwa haja ya kutembelea vituo vya kutunzia vya kijamii huku Ukraine ili kukuana na wakimbizi na wale wote ambao ni waathirika wa vita kati ya Urusi na Ukraine. Kiongozi mkuu wa kanisa la Kigiriki Katoliki na Mkuu Kanisa la Kilatini Mokszycki nchini Ukraine waliweza kuzungumza moja kwa moja na Papa Francisko. Wakati wa mazungumzo yao kwa simu, Kardinali Krajewski amemsimulia Papa hisia za kwanza za ziara hiyo, hasa kile alichokiona kwenye eneo la Kipolishi, ambako aliweza kuingia Ukraine.
Papa pia alisasishwa kuhusu mpango wa ziara ya mjumbe wake nchini Ukraine, iliyojadiliwa hapo awali na washiriki katika mkutano huo. Kardinali Krajewski hana tarehe ya mwisho ya utume wake kwani Baba Mtakatifu amemwagiza kukaa Ukraine kadiri inavyohitajika ili kutoa msaada kwa watu wa Ukraine kwa niaba ya makao makuu ya kitume katika nyakati hizi za kushangaza za historia. Na mkuu wa kanisa la Ukraine Shevchuk ametoa maoni yake kuwa Papa Francisko anataka kuwapo yeye binafasi kwa njia ya wawakilisho wake. Ndilo lengo la ziara safari hiyo.
Pamoja na kutojua ratiba yake Kardinali Krajewski nchini Ulaya. Alhamisi 20 Machi ametembelea vituo vya kijamii vya Kanisa katoliki la Kigiriki nchini Ukraine mahali ambapo ameshiriki sala ya pamoja na wawakilishi Baraza la Makanisa Ukraine pamoja na mashirika ya kitawa. Utume wa Kardinali Krajewski, ulitangazw ana Baba Mtakatifu wakati wa hitimisho la Sla ya Malaika wa Bwana mnamo tarehe 6 Machi. Papa alikuwa amebaisnisha juu ya kutumea Kardinali Krajewski na Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa Muda wa baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu.
Kwa maana hiyo Kardinali Krajewski aliingia Ukraine kupitia mpaka wa Paland wakati Kardinali Czerny ambaye kwa sasa yuko Hungeria mahali ambapo anaendelea kufanya mikutano na taasisi mbali mbali za mapokezi ya wakimbizi wa vita kutoka Ukraine na kutembelea miundo hiyo ya makaribisho. Tukumbuke Papa alikuwa amesisitiza kwamba uwepo wao makardinali wawili kwa niaba yake, hawawakilisho uwepo wa Papa laikini ni ishara ya uwepo wa watu wote wakristo wanaotaka kukaa karibu na kusema “vita ni wazimu, simamisheni vita tafahdali,Tazameni ni ukatili wa aina gani.