Kard.Parolin:Kulipuliwa hospitali ya watoto,Ukraine ni jambo lisilokubalika
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kulipuliwa kwa hospitali ya watoto ni jambo lisilokubalika. Hakuna sababu. Hivi ndivyo Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican alisema kando ya mkutano wa Roma, huku akielezea wasiwasi wake wa vita vya kila upande. Kauli ya Katibu wa Vatican imekuja baada ya shambulio la anga la Urusi ambalo, kwa mujibu wa mkuu wa utawala wa kijeshi wa mkoa wa Donetsk, liliharibu hospitali ya Mariupol yenye wodi za uzazi na watoto: kuna mazungumzo ya mauaji kati ya watoto na wanawake wajawazito.
Kardinali Parolin alisema kuwa nafasi ya mazungumzo ni finyu, hata hivyo anatumaini kuwa nafasi ya mazungumzo inaweza kufikiwa. Akizungumzia kwa simu aliyompigia Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergej Lavrov, Kardinali Parolin alisema kuwa mahojiano hayo hayakutoa dhamana yoyote. Hakukuwa na, hasa, hakuna uhakikisho kwenye nia za huduma za kibinadamu.
Vatican iko tayari njia ya upatanisho
Kardinali Parolini alibainisha jisni ambavyo Vatican inayo nia yake ya kuchukua hatua katika nyanja ya kidiplomasia kutafuta suluhisho zinazoweza kukomesha vita. Kwa namna ya pekee, Vatican imeomba kusitisha mzozo huo na kuunganisha mazungumzo, kwa kuonesha uwezekano wa kuwa mpatanishi ikiwa inaaminika kuwa inaweza kusaidia, lakini lazima waitwe kufanya hivyo.
Kuwepo nchini Ukraine kwa makadinali wawili, Msimamizi wa Sadaka ya Kitume Kardinali Konrad Krajewski, na Mwenyekiti wa muda wa Baraza la Kipapa la Maedneleo Fungamani ya Binadamu, Kardinali Michael Czerny, alisema ni ishara kwamba Papa anataka kutoa mchango wake, na vile vile juu ya madhubuti zaidi ngazi ya kidiplomasia na kiroho, pia juu ya ile ya misaada ya kibinadamu. Hatimaye akizungumzia maneno ya Patriaki wa Kiorthodox wa Urusi Kirill, Kardinali alisema kwamba taarifa hizi hazipendekezi na haziendelezi maelewano, badala yake zina hatari ya kuchochea roho hata zaidi, na kusababisha kuongezeka ambayo haisuluhishi mgogoro huo kwa amani.