Kard:O’Malley:'Praedicate evangelium'inaongeza nguvu ya ulinzi wa watoto
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kwa mara ya kwanza, Papa Francisko ametengeneza njia ya usalama na ulinzi wa watoto kuwa sehemu msingi ya muundo wa serikali kuu ya Kanisa yaani ‘Curia Romana’. Amesema hayo Kadinali Seán Patrick O’Malley alikaribisha Katiba mpya ya Kitume huko akitoa maoni yake kuhusu kutangazwa kwa Katiba mpya inayoongozwa na kauli mbiu: “Praedicate Evangelium” yaani “Hubirini Injili” ambapo inahusu Kanisa Kuu la Roma na huduma yake yote ya Kanisa na Ulimwengu. Kardinali O’Malley alisema Katiba hiyo inathibitisha jukumu la Tume “katika kuhakikisha Kanisa linakuwa mahali salama kwa watoto na watu walio katika mazingira magumu. Kuunganisha Tume kwa ukaribu zaidi na kazi ya Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa inawakilisha hatua kubwa ya kusonga mbele katika kuboresha Kanisa, mahali na mamlaka ya Tume, ambayo inaweza tu kusababisha utamaduni wenye nguvu zaidi wa kulinda katika Curia Romana na Kanisa zima la Ulimwengu.
Kardinali alipongeza uamuzi wa kudumisha Tume kama chombo tofauti ndani ya Baraza ambacho kinafurahia kupata moja kwa moja kutoka kwa Baba Mtakatifu na kwa uongozi wake na wafanyakazi. Kardinali O'Malley aliongeza kuwa kusema kuwa tume ya Kipapa iliyopyaishwa na iliyoidhinishwa upya itatekeleza jukumu kubwa zaidi katika kuhakikisha Kanisa linakuwa mahali salama kwa watoto na watu walio katika mazingira magumu.” Iliyotangazwa na Papa, maandishi hayo yana na kuweka utaratibu wa marekebisho mengi ambayo tayari yametekelezwa katika miaka ya hivi karibuni. Katiba Mpya itaanza kutumika tangu tarehe 5 Juni, katika Sherehe ya Pentekoste. Katiba mpya inatoa muundo wa kimisionari zaidi juu ya Curia ili izidi kuhudumia Makanisa mahalia na uinjilishaji.
Ikumbukwe Katiba mpya ya Kitume “Praedicate Evangelium” kuhusu Curia ya Kirumi na huduma yake kwa Kanisa na kwa ulimwengu ilichapishwa siku ya Maadhimisho ya Mtakatifu Yosefu, msimamizi wa Kanisa, tarehe 19 Machi 2022 na itaanza kutumika tarehe 5 Juni, katika Sherehe ya Pentekoste. Matokeo ya mchakato wa kusikiliza kwa muda mrefu ulioanza kwa Mikutano Mikuu iliyotangulia Mkutano Mkuu wa 2013, Katiba mpya, ambayo inachukua nafasi ya ‘Pastor bonus’ ya Yohane Paulo II iliyotangazwa tarehe 28 Juni 1988 na kuanza kutumika tangu tarehe Mosi Machi 1989 imejikita katika ibara 250. Kuna mabadiliko ya kuunganisha mabaraza ya kipapa kama vile Baraza la Kiapapa la Ujinjilishaji wa Watu na Baraza la Kipapa la Unjilishaji mpya litakuwa chini ya Uongozi mkuu wa Papa. Wakati Tume ya Ulinzi wa Watoto inakuwa ndani ya Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. Na ndiyo maana Kardinali amethibitisha hayo kutokana na Tume ambayo sana inaingia kuswa sehemu hiyo ya Baraza.