Kard.Krajewski:Katika eneo la vita ninapeleka ujumbe wa Papa
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kardinali Konrad Krajewski, Msimamizi wa sadaka ya Kitume ya Papa, akiwa Ukraine, kabla ya kuingia ndani zaidi amethibitisha kwamba amekwenda katika maendeo ya matukio ya vita kupelekea msaada na matumaini hasa kwa kufuata Injili: “Nimekuja hapa na saiahala tatu nyeti sanda, ya Injili, Sala, kufuna na kutoa sadaka”. Amethibtisha hayo katika mahojiano yaliyotolewa huko Lviv katika TV mahalia ya Kiukreni iitwayo “Zhyve.tv”, akiwa katika utume ambao Papa Francisko amemkabidhi kufika Ukraine. Akiwa anajiandaa kuacha Leupoul ili kuweza kufikia eneo la ndani zaidi amethibitisha kwamba “Leo hii nchi ni mahali pa maumivu lakini ni lazima kuwepo hapa ili kulifanya Kanisa zima lijisikie karibu na watu walio katika matatizo makubwa”.
Je, kuwapo kwake kuna umuhimu gani?
Ni muhimu kuwepo katika taifa hilo la Ukraine la kuteswa, ambapo uwepo kwanza wa neno la upendo. Na baadaye kiukweli, pamoja na usaidizi wa kimaadili, pamoja na imani ambayo wanabeba wao wenyewe, pia amepeleka tumaini kutokana na hali hii mbaya waliyo nayo. Kuna misaada madhubuti kwa Ukraine ambayo inapelekwa kupitia njia za kidiplomasia lakini pia kutoka nchi hiyo.
Sala ya pamoja ya kidini katika Kanisa kuu la Lviv
Katika wakati huu wa kutisha wa vita na mateso ya wanadamu, wakati wa kukata tamaa kwa kupoteza wapendwa wetu au kwa kutelekezwa kwa nyumba zetu, tunataka kumwambia Baba yetu wa mbinguni sala ya dhati ya amani. Alisema hayo Askofu Mkuu wa Lviv, Mieczyslaw Mokrzycki wakati wa sala ya pamoja na madhehebu mbalimbali iliyofanyika tarehe 10 Machi 2022 katika Kanisa kuu la Kilatini la Bikira Maria kupalizwa mbinguni na kuongozwa na Kardinali Krajewski mwenyewe.
Katika hotuba yake ya kuwakaribisha wale waliohudhuria, akiwemo askofu mkuu Sviatoslav Shevchuk wa Kiev-Halyč wa Kanisa Katoliki la Kigiriki la Kiukreni na viongozi mbalimbali, kasisi huyo alimshukuru Msimamizi wa Sadaka ya kipapa kwa uwepo wake nchini Ukraine katika wakati huu mgumu sana. Baadaye wawakilishi mbalimbali wa Makanisa na jumuiya za kidini wakaelekeza maombi yao kwa ajili ya amani kwa Mungu. “Leo tunaweka mbele ya macho yako maumivu na mateso ya Ukraine, milima ya maiti, mito ya damu na bahari ya machozi alisema hayo Askofu Mkuu Shevchuk katika sala yake kwa kuinua kwa Baba wa Mbingu. “Tunawaombea wale wote waliotoa maisha yao kwa ajili ya nchi yao, aliongeza kwa ajili ya majeshi yetu, kwa wana na binti za Ukraine ambao kwa miili yao wenyewe wanalinda maisha yao kutoka kwa adui. Hatimaye, Askofu Mkuu huyo alisali kwa ajili ya raia wote wasio na hatia waliouawa na kwa ajili ya waathirika wa Mariupol waliozikwa katika makaburi makubwa ya halaiki bila kuzikwa ipasavyo.