Kard.Czerny huko Ukraine:Sisi sote ni maskini katika uso wa vita,acha kushambulia raia
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Ujumbe wa mwakilishi Papa nchini Hungaria unaendelea. Awali ya yote kukutana na Naibu Waziri Mkuu na kutembelea mpaka wa Barabás, ambapo mamia ya watu wamekusanyika katika sehemu tano za mapokezi. Baadaye kupitia kivuko cha mpaka na kituo katika kijiji cha Ukraine cha Beregove, huko Transcarpathia, eneo ambalo halikushambuliwa kwa mabomu lakini lilikuwa mahali pa kukutania maelfu ya wakimbizi. Kardinali anashutumu shambulio la bomu katika hospitali ya Mariupol kwani hali hii inakufanya utetemeke. Huyu ni Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa muda wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya binadamu aliyetumwa na Papa kwenda Hungaria.
“Karibu Ukraine” ndivyo ilikuwa linasomeka bango liliofunikwa na matawi makavu, kwenye mpaka wa Baraba, kati ya Ukraine na Hungaria. Karibu kwa kufanya utani wa uchungu ukiangalia shimo ambalo nchi ya Ulaya Mashariki imekuwamo tangu tarehe 24 Februari, wakati wa kuzuka kwa vita hivi vya kikatili. Katika mpaka kulikuwa angalau magari hamsini yaliyokuwa yanasubiri kupita udhibiti mkali wa forodha na wa polepole sana. Saa 5.20 usiku gari nyeupe iliyobeba watu watano ilikuwa katikati ya mstari; muda mfupi kabla ya saa 2 usiku ilikuwa imesonga mbele kwa nafasi sita pekee.
Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa muda wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya binadamu aliyetumwa na Papa kwenda Hungari kuwafariji wakimbizi wa Ukraine, alivuka mpaka majira ya alasiri. Alisindikizwa na mapadre wawili waliojitolea kwa uchungaji wa wahamiaji na Askofu Mkatoliki wa Ugiriki wa Nyíregyháza, Ábel Szocksa, ambaye alitoa gari lake kwenda upande wa pili, hadi Beregove, kijiji cha Transcarpathian kilichoepushwa na mabomu lakini imekuwa moja ya sehemu kuu za umati wa wakimbizi.
Kardinali Czerny amekutana na wakimbizi wa Kiukreni huko Budapest na kuwaleza kuwa Papa yuko karibu nao. Mita chache kutoka katikati, ambapo maisha yanaonekana kutiririka kawaida, gari lililo na Kardinali linasimama mbele ya shule nyeupe ya bweni ambayo bado inajengwa. Ilitakiwa kuwa bweni la wanafunzi, sasa imekuwa kimbilio. Jina hili ni refu na tata lakini lingeweza kuitwa “Ndugu wote”, kwa vile linakusanya juhudi za Wakatoliki, Wagiriki-Wakatoliki, Wakatoliki wa Roma, Waprotestanti, Waijili. “Hakuna tofauti, sisi sote ni wasamaria wema walioitwa kusaidia wengine. Tumeelewa kuwa ikiwa hatutashirikiana, hatuwezi kutoa msaada wa kweli kwa wale wanaoteseka”, ahayo Nil Luschschak, akiwafanya wawakilishi wa dini mbalimbali kuketi mezani pamoja.
Kila mmoja alimwambia mjumbe wa Papa uzoefu wa kukaribisha watu wanaokimbia, baadaye kukutana na mgongano na janga la familia zilizonusurika kwa kifo au kutengana kwa mtu wa familia yake au majuto ya baadhi ya askari wa Kirusi ambao walidhani wanashiriki katika haraka za operesheni ya kijeshi na wakajikuta katikati ya vita. “Ni mauaji ya halaiki,” alisema askofu Péter Miklós Lucsok akiwa anamaaninisha waathirika. Kwa watu wetu ni Njia ya Msalaba na wengi wako tayari kwenda Golgotha. Wa Ukraine hawakimbii, hawakati tamaa, kwana tunataka kutetea maadili ya uhuru, ukweli, utu wa mwanadamu”.