Tafuta

Askofu Mkuu  Jan Graubner, Rais wa Baraza la Maaskofu wa Jamhuri ya Ucheki. Askofu Mkuu Jan Graubner, Rais wa Baraza la Maaskofu wa Jamhuri ya Ucheki. 

Kanisa la Ucheki watapokea wakimbizi kwenye parokia na Monasteri

Wimbi la mshikamano wa Jumhuri ya Czech.Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Slovakia ameandika barua kwa wawakilishi wa Makanisa ya Ukraine kuhusu nia ya kukaribisha wakimbizi hata katika parokia na monasteri.Katika nchi nzima wanakusanya vifaa ili kusaidia wakimbizi na watu wanaobaki Ukraine.

Vatican News

Askofu Mkuu wa Olomouc na rais wa Baraza la Maaskofu wa Jamhuri ya Czech (CEC), Askofu  Jan Graubner ametuma barua yake  kwa viongozi wa Makanisa Katoliki nchini Ukraine: Askoufu Mkuu M. Mokrzycki, Rais wa Baraza la Maaskofu katoliki nchini Romania; Askofu Mkuu S. Shevchuk, wa  Kyiv-Halych; na msimamizi wa Kitume cha Upatriaki wa Mukachevo N. Lushchak. Katika barua yake kwa viongozi wa Kanisa la Ukraine, Rais huyo anaelezea ukaribu wake na msaada wake katika kipindi hiki kigumu ambacho wanapitia wao kwa ajili ya taifa lao na watu wao.

Kituo cha makaribisho kwa wakimbizi kutoka Ukraine
Kituo cha makaribisho kwa wakimbizi kutoka Ukraine

Askofu Mkuu analaani kwa dhati uvamizi wa kirusi katika nchi hiyo. Askofu Mkuu Graubner, ameandika kwamba kwa niaba ya Baraza la Maaskofu wa Czech, wa maaskofu, mapadre wote na waamini wa Jamhuri ya Czech wanataka kuwahakikisha sala zao. Kwa njia ya upendo wa Jamhuri hiyo walikuwa tayari wametangaza makusanyo ya kitaifa katika makanisa yote, ambapo kile kitakacho kusanywa kitapelekwa kwa watu wao kupitia Caritas ya Jamhuri ya Czech.

Kituo cha makaribisho kwa wakimbizi kutoka Ukraine
Kituo cha makaribisho kwa wakimbizi kutoka Ukraine

Askofu Mkuu aidha amebainisha jinsi ambavyo wako tayari kusaidia wale ambao wanatafuta kimbia kutoka katika balaa la vita na kuwapa mahali pa kufikia na rasilimali msingi katika  parokia zao  au monastery za watawa. Vile vile amealika waamini washiriki kukaribisha wazalendo wote wa Ukraine katika nyumba zao. Na ikiwa lazima, watatoa hata nguvu zao za upendo na watu wa kujitolea moja kwa moja nchini Ukraine. Siku za mwisho wa ameona wimbi la mshikamano kutoka kwa majimbo jumuiya za kidini na parokia katika nchi zao. Wanaomba wao na wanataka kuwasaidia na wao hawako peke yao.

07 March 2022, 17:12