Ile'mito ya damu'huko Ukraine:Ni'vita',si'operesheni ya kijeshi!
ANDREA TORNIELLI
Kinachotekea Ukraine ni “vita” sio “operesheni ya kijeshi”. Mwanzoni mwa wito wake kwa upya kwa ajili ya amani Papa Francisko alikanusha habari za uwongo ambazo zingependelea kuwasilisha kile kinachotokea kwa hila za maneno ili kuficha ukweli wa ukatili unaotendeka. Papa Francisko alielezea kile kilichopo machoni pa wote, nyumba za raia zilizoharibiwa, wazee, wanawake, watoto waliouawa kwa kuthibitisha kwamba nchini Ukraine“mito ya damu na machozi inatiririka”. Haya si maneno nasibu, lakini yanarudia kwa kiasi kikubwa yale yaliyosemwa siku mbili zilizopita na askofu mkuu wa Kiev, Sviatoslav Shevchuk, ambaye anaishi chini ya kuzingirwa katikati ya watu wake katika mji mkuu wa Ukraine.
Msisitizo wa tatu unahusu uharaka wa hatua za kibinadamu. Papa ameomba kwamba mikondo ya huduma za kibinadamu zihakikishwe na msisitizo lazima uwekwe kwenye ukweli, ambao unaonesha jinsi jana, ya kwamba licha ya matamko ya nia ya jeshi la Kirusi ambalo linavamia Ukraine, lakini hiyo haiendani na ukweli. Askofu wa Roma pia ameomba kuheshimiwa sheria za kimataifa pia ambazo ni dhahiri zilikiukwa na wale waliotaka kuanzisha vita hivi vya uchokozi.
Tena, Papa Francisko ameomba kwamba “mashambulizi ya silaha yakome, kwa sababu ni wazi kwamba tunazungumzia vita vya uchokozi, ambapo kuna wale wanaoshambulia na wale wanaojilinda. Na ambapo kuna watu wanaolipa matokeo mabaya kama vile kifo, mateso, familia zilizovunjika na mamilioni ya wakimbizi.
Hatimaye, baada ya shukrani kwa wale wanaowakaribisha wanaokimbia, shukrani za Papa pia zimewandea waandishi wa habari wanaohatarisha maisha yao ili kuhakikisha hupatikanaji wa habari, hivyo kuruhusu kila mtu kuwa karibu na janga la wa watu wa Ukraine na “kutathmini ukatili wa vita”. Shukrani ambayo inakuja siku tatu tu baada ya kuidhinishwa kwa sheria mpya inayoruhusu raia wa Urusi na wa kigeni kuhukumiwa kifungo hadi kufikia miaka kumi na tano kwa kueneza “habari za uwongo kuhusu vikosi vya jeshi”. Kwa sababu kuna wanaodai kufafanua vita hii chafu kuwa ni “operesheni ya kijeshi”.