Mabomu nchini Ukraine. Mabomu nchini Ukraine.  Tahariri

Vita baada ya janga:hatari kwa ubinadamu

Utafikiri ni suala lisilowezekana kuwa na vita barani Ulaya katika Karne XXI.Hatari kwa kizazi ni kubwa.Papa anaomba kusali kwa sala dhaifu lakini yenye nguvu dhidi ya nguvu za silaha.

Sergio Centofanti

Yupo ambaye halikuwa anaamini. Vita barani Ulaya katika Milenia ya tatu. Kisichowezekana lakini karibu kinawezekana. Kwa sasa tayari kuna vifo vingi. Kuna hofu ya umwagaji wa damu. Kwa kawaida wanaoathirika ni wale wasio na hatia, wasio na ulinzi, ambao wangependelea kuishi kwa amani na wengine, kwa wote, hata ikiwa wana bendera tofauti na nyingine. Kwa wenye nguvu hawa hawatazamwi ni wadhaifu wanayokumbana nayo.  Kuna mchezo mbaya kama ule wa Herode.  Hawasitishi mauaji kwa wasio na hatia. Baada ya mateso yaliyosababishwa na janga, inafikia maombolezo ya vita ambavyo hatujuhi kile kitakachotokea.

Kuna aliyekuwa amesema juu ya hatari ya vita vya tatu vya dunia. Tunaendelea kuamini kuwa haiwezekani. Tunaendelea kufikiria kuwa ubinadamu hauwezi kuwa kichaa hivyo kiasi cha kuangukia kwa mara nyingine tena.  Kwa sababu vita ni wenda uzima, haina maana. Ni mapepo. Na shetani anataka kuharibu maisha, anataka kuharibu ulimwengu. Leo ana silaha za kutosha kwa ajili ya kufikia malengo yake. Hatupaswi kudharau hivi hivi amani ya ulimwengu.

Papa Francisko akiwa amejaa uchungu na wasiwasi, ameomba sala na kufunga kwa ajili ya amani. Kuungana kwa sala dhidi ya nguvu za silaha.  Ni nani ataweza kutuamini? Ni nani atakataa jambo hili la kinyenyekevu la kufunga dhidi ya nguvu za  mizinga? Sala inaunganisha na Baba na kutufanya kuwa ndugu, kufunga kunatuondolea kitu cha kushirikishana na wengine hata kama mwingine ni adui. Sala ni mapinduzi ya kweli inayobadili ulimwengu kwa sababu inabadili mioyo. Tuna rasilimali ndogo dhidi ya vita kwa sababu, bila kutuondolea uwajibikaji wowote, shetani anatuongoza katika chuki, hila, na ukatili. Yesu alisema kuwa “aina hii ya pepo siyo rahisi kuondolewa kwa namna yoyote isipokuwa kwa njia ya maombi”.

VITA NYINGINE ULAYA NI MAPEPO
24 February 2022, 16:14