Ufunguzi wa Ubalozi mpya wa Vatican huko Abu Dhabi,Nchi za Falme za Kiarabu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Wito wa kuendelea katika njia iliyonzishwa kwa kutia sani katika Hati ya Udugu wa Kibinadamu iliyotiwa saini mnamo tarehe 4 Februari 2019 ili kuishi kidugu na watu wote bila ubaguzi wa rangi, dini, imani na utunzaji wa kazi ya uumbaji. Alikumbusha hayo Katibu Msaidizi wa Vatican akiwa huko Abu Dhabi katika sherehe za uzinduzi wa Nyumba mpya ya Papa, yaaani Ubalozi Mpya wa Kitume, kama ishara ya umakini wa Papa kwa nchi hiyo na hasa kwa Jumuiya ya Kikatoliki. Kwa hakika hilo sio jengo rahisi katika nchi kama hiyo ya uarabuni, lakini ni mahali pa ishara na umakini mkubwa wa Papa kwa Nchi ya Falme za Kiarabu hasa kwa kuzingatia jumuiya nzima ya kikatoliki inayoishi huko. Na zaidi ya yote, kutokana na kuongeza nguvu ya kile kwa kile ambacho kinadumisha na Azimio la Hati ya Udugu wa Kibinadamu, ambalo kwa hakika linazinduliwa kwa upya njia ya mazungumzo dhidi ya upotoshaji wowote au udanganyifu wa dini. Kwa maneno hayo muhimu, Askofu Mkuu Edgar Peña Parra, Katibu wa Sekretarieti ya Vatican, Ijumaa tarehe 4 Februari 2022, alizindua ofisi rasmi mpya ya kitume katika Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu, katika afla hiyo huko Abu Dhabi mbele ya mamlaka za kiraia na viongozi wa kidiplomasia.
Tukio hilo linaangukia katika kipindi kilichojaa kumbukumbu na sherehe ambayo ilikuwa ni Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu, iliyotangazwa kufanyika katika siku hiyo na Umoja wa Mataifa; maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa kwa nchi hiyo; maadhimisho ya miaka 15 ya uwepo wa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Falme za Kiarabu na Vatican; pamoja na mwaka wa Pili wa kutiwa saini kwa Hati na Papa na Imamu Mkuu wa Al-Azhar, Ahmad Al-Tayyeb. Na ni kutokana na kurasa hizo za kihistoria, ambazo zimekuwa msingi wa mahusiano kati ya Wakristo na waislamu, ambazo zilimpatia tafakari ya Askofu Mkuu Peña Parra. Askofu Mkuu Parra akifuatana na Monsinyo Yoannis Gaid, mjumbe wa Kamati Kuu ya Udugu wa Kibinadamu na katibu wa zamani wa kibinafsi wa Papa Francisko, alisema kwamba katika kutia saini hati hiyo, Imam mkuu na Papa walionesha nia yao kwamba inaweza kutumika kuwa kama mwongozo kwa vizazi vijavyo ili kuendeleza utamaduni wa kuheshimiana katika utambuzi wa neema kuu ya kimungu inayowafanya wanadamu wote kuwa ndugu na dada. Ni matumaini yake kwamba inaweza pia kutumika kama mfumo wa kuimarisha uhusiano wao wa kidiplomasia.
Wito kwa waumini, uliozaliwa kutokana na hati hiyo na kuzinduliwa kwa upya na askofu mkuu, ni kuishi katika udugu na watu wote bila ubaguzi wa rangi, dini au imani na kulinda kazi ya uumbaji, kwa ajili ya nyumba yetu ya pamoja. Kinyume na upotoshaji wowote au upotoshaji wa dini, jibu la wito huo linaweza kuchagua njia ya mazungumzo tu, ambayo uleta maelewano na ushirikiano bora. Na alihimiza kuzidisha juhudi za kuhamasisha yaliyomo kwenye Hati ili kusaidia kujenga ulimwengu wa haki na amani. Juhudi, hizi alisisitiza kwamba ni muhimu sana leo hii tunapoendelea kuona matokeo mabaya ya kuchukua nafasi ya ukweli upitao maumbile juu ya mwanadamu na juu ya uumbaji kwa maadili ya juu juu na utumiaji hovyo.
Kufunguliwa kwa Ubalozi wa kitume uarabuni utadumisha kukutana,mazungumzi na ushirikiano
Matumaini ya kiongozi wa Vatican ni kwamba uwakilishi huu mpya wa kidiplomasia wa Makao ya Kitume ya Kipapa na ambao unaweza kufafanuliwa kwa usahihi kama Nyumba ya Papa, unaweza kutumika kama mahali pa kukutana na mazungumzo kwa ushirikiano wao na nchi mbili kwa miaka mingi ijayo. Hasa kwa jumuiya ndogo ya Kikatoliki ya nchi,alisema Askofu Mkuu Peña Parra na pia kudhihirisha uchungaji wa Baba Mtakatifu kwao. Kwa kuhitimisha alisema mahali hapo panaweza kuwa chanzo cha faraja kwao wanapojitahidi kuishi imani yao na kuwa mifano ya udugu wa kibinadamu kama kaka na dada zao wote katika nchi hiyo.