Kard.Sandri:Siku ya wagonjwa Duniani na fundisho la Mtakatifu Yohane Paulo II

Katika kesha la Siku ya Wagonjwa duniani, 11 Febaruari,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki,amemkumbuka Mtakatifu yohane Paulo II,ambaye amesema ni mwanzilishi wa Siku hiyo mnamo 1992 na alitoa wakati wake mgumu zaidi wa maisha kutangaza Injili.Na Dk.Andrea Tornielli,amesema kuwa hakujificha kwa vyombo vya habari na picha na ndiyo ilikuwa njia yake kuishi Injili.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki, Kardinali Leonardo Sandri, amesema kuwa  Mtakatifu Yohane Paulo II alitufundisha sisi sote jinsi ya kuishi nyakati hizi ngumu za uwepo wa mwanadamu  na kukumbuka mateso yaliyoashiria vipindi vya mwisho vya Upapa wa Mtakatifu Yohane Paulo II  wakati Kardinali huyo  aliposhika nafasi ya Katibu wa Vatican.

Na kwa mujibu wa mkurugenzi Mkuu wa uhariri wa Baraza la Kipapa la  Mawasiliano Vatican, Dk Andrea Tornielli, ambaye wakati huo yeye alikuwa mhariri wa Vatican wa gazeti liitwalo “ Kila siku” aliongeza kusema kuwa “Hakujificha kwa vyombo vya picha na ndiyo ilikuwa njia yake ya kuishi Injili hadi mwisho”, ka maana hiyo wote wawili wanakumbuka tukio hilo katika mkesha wa Siku ya Wagonjwa Ulimwenguni kama sehemu ya ripoti iliyotolewa na Televisheni ya Telepace kwa msingi wa nyenzo za kumbukumbu za Vyombo vya Habari vya Vatican. Picha hizo zinaanzia na kumbukumbu ya mwaka wa kwanza iliyoanzishwa mwaka wa 1992 na kuadhimishwa tarehe 11 Februari 1993 siku ya kumbukumbu ya Mama Yetu wa Lourdes.

“Daraja bora linatuunganisha, tuliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro, moyo wa Ukristo, na wale waliokusanyika kwenye uwanja wa Lourdes”, alisema Papa wa Kipoland, mwishoni mwa Ibada iliyoadhimishwa na Kardinali Camillo Ruini ambaye wakati huo alikuwa Makamu wa Papa wa jimbo la Roma. Ni kifungo cha kiroho, kilichojengwa juu ya imani ambayo inaungwa mkono na maombezi ya Bikira Msafi wa Moyo,

Kardinali Sandri anasema: “Ni Dhahiri kuona utofauti kutoka katika ubora wa juu wa kiufundi wa picha za leo. Lakini moyo umejaa hisia vile vile kumuona Papa mpendwa ambaye wakati huo tayari alikuwa amegundua kuwa alikuwa ameshikwa na ugonjwa wa Parkinson. Picha ya mateso yake hakika ni picha ya Njia ya Msalaba ya  mwisho kabla ya kifo chake”.  Kwa kuongezea amesema: “Alikuwa sahihi na mgongo wake kwa aliyekuwa anachukua picha ya video kwenye kamera ili asioneshe dalili za tracheotomy na alifuata maandamano ya Njia ya Msalaba siku ya  Ijumaa Kuu akiwa Vatican huku akiwa na msalaba mikononi mwake”. Na "Katika tukio hilo Yesu alijitoa kwa Baba kwa ajili ya wokovu wa ulimwengu, kama sisi sote tunavyopaswa kufanya na maisha yetu ya Kikristo”.

10 February 2022, 17:13