Papa amekutana na Bw.Borut Pahor,rais wa Jamhuri ya Slovenia
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 7 Februari 2022 amekutana na kuzungumza na Rais Borut Pahor, wa Jumhuri ya Slovenia, na aliosindikizana nao. Baada ya Mkutano huo pia amekutana na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin akiambata na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa, Vatican.
Katika mazungumzo kati yao na mgeni huyo wameridhishwa na uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya nchi hizi mbili ndani ya mzunguko wa miakatherathini tangu kuufungua na kupongezana juu ya mazungumzo yaliyopo katika Kanisa na Mamlaka ya raia nchini Slovenia.
Wakiendelea na mchakato wa mazungumzo yao kati ya Rais Borut Pahor na viongozi wakuu wa Vatican, wametazama pia masuala ya kimataifa na kikanda, miongoni ni pamoja na ushirikiano wa kikanda, upanuaji wa uanachama wa Umoja wa Ulaya katika Nchi za Mashariki ya Ulaya na hali halisi inayoendelea nchini Ukraine.