Tafuta

Radio Vatican kutimiza miaka 91. Alikuwa ni Papa Pio XI aliyeizundua mnamo 1931. Radio Vatican kutimiza miaka 91. Alikuwa ni Papa Pio XI aliyeizundua mnamo 1931. 

Miaka 91 ya Radio Vatican,chombo kinachoaminika

Ilikuwa ni tarehe 12 Februari 1931,Papa Pio XI alizindua Masafa ya Radio ya Kipapa yaliyoanzishwa na Guglielmo Marconi.Maadhimisho yanasukana na Siku ya Kimataifa ya Radio iliyanzishwa na Umoja wa Mataifa,13 Februari 1946.Msomi Enrico Menduni amesema ni daraja la kizamani ambalo linajitunza vizuri kwa umri,katika wakati huu wa janga kwani ni msindikizaji katika upweke na usumbufu kwa wengi.

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Radio na uaminifu ndiyo mambo mawili ambayo yanaongoza kauli mbiu ya mwaka 2022 katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Radio, ambayo ni zana chombo chenye nguvu sana kwa ajili ya kuadhimisha ubinadamu wote na utofauti wake.  Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa liridhia azimio la shirika   la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Teknolojia, UNESCO ambapo mnamo 1946 la kutaka tarehe 13 Februari ya kila mwaka kuwa siku ya kimataifa ya Radio duniani. Ni siku ambayo hata Radio ya Umoja wa Mataifa ilianza kufanya kazi ambapo Baraza Kuu lilitambua pia nafasi ya Radio katika kuwa na uwezo mkubwa wa kupasha habari idadi kubwa ya watu licha ya maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano. Halikadhalika Baraza Kuu lilipongeza jitihada za Radio ya Umoja wa Mataifa ya kuendelea kueneza vipindi vyake kwa lugha mbali mbali na kwamba ijitahidi kusambaza zaidi vipindi vyake maeneo mengi zaidi kwa kadri inavyowezekana. Siku ya Kimataifa ya Radio inalenga kuimarisha ushirikiano wa kimataifa baina ya watangazaji, na kuhamasisha vituo vikubwa vya radio na vile vya kijamii viendeleze haki ya msingi ya wananchi kupata taarifa na uhuru wa kujieleza kupitia radio.

Kabla ya hapo kwa miaka karibu 15, shukrani kwa maono ya mbali ya Papa Pio XI na Gwiji wa ufumbuzi Guglielmo Marconi, mnamo tarehe 12 Februari 1931 walizindua Radio hii ambayo hadi leo hii masafa yanaendelea ya kipapa katika kueneza kwa njia ya vyombo vilivyosasishwa na vyenye uwezo wa kutangaza ujumbe wote wa Kipapa ulimwenguni. Msemaji wa kwanza wa Radio ijayo ya Vatican alikuwa ni mwenyewe akiyeivumbua kwa njia ya Radio. Kama Padre Guglielmo Marconi aliyekuwa aliyekuwa mhusika wa kwanza wa Radio Vatican.  Alitangaza kuwa Papa altaweza kuzungumza na watu wote. “Ninayo heshima kwawatangazia kuwa kwa muda kitambo Baba Mtakatifu Pio XI atazindua Kituo cha Radio cha Mji wa Vatican. Masafa ya umeme yatabeba neno lake kupitia nafasi, la amani na baraka ulimwenguni kote. Kwa takriban karne ishirini Papa wa Roma alilifanya Neno la Mafundisho yake ya Kimungu yasikike ulimwenguni; lakini hii ni mara ya kwanza kwa sauti Yake kusikika kwa wakati mmoja juu ya uso mzima wa dunia”. Baada ya Guglielmo Marconi, Papa Pius XI alikaribia kipaza sauti.

Kwa ujumbe wake kwa njia ya Radio uliowalekeza watu wote, alitumia lugha ya kilatino  ambayo Baba Mtakatifu alizingatia kama lugha ya ulimwengu wa Kanisa na kusema kuwa: “ Kwa kuwa, na mpango mkuu wa Mungu, wafuasi wa Mkuu wa Mitume, yaani, wale ambao mafundisho yao na mahubiri yao kwa amri ya kimungu yamekusudiwa kwa watu wote na kwa kila kiumbe, na kuweza kwanza kufaidika na hili, mahali pa uvumbuzi wa kupendeza wa Marconi, na tuzungumze kwanza kabisa kwa vitu vyote na kwa watu wote, tukisema, hapa na baadaye, kwa maneno yenyewe ya Maandiko Matakatifu: “Sikilizeni, enyi mbingu, yale ninayokaribia kusema, sikilizeni nchi maneno ya kinywa changu. Sikilizeni, enyi watu wote, sikilizeni, ninyi nyote mkaao duniani, mlioungana katika nia moja, matajiri na maskini, Sikilizeni, enyi visiwa, sikilizeni, enyi watu wa mbali”.

Sauti ya Papa Pio XI wakati wa kuzindua Radio ya Kipapa 1931

Ulimwengu wa Radio utafikiri haujui wakati wa mgogoro. Shirika la Umoja wa Mataifa,  Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) linabainisha  kuwa katika kipindi hiki cha janga, kwa sababu ya kuendelea kwa habari za kughushi, Imani kwa vyombo vya habari imepungua kwa ujumla.  Lakini Radio, inaendelea kutumia zana zake za  kiajabu na kuelekeza katika habari za kuthibitisha na kutegemewa. Wazalendo wengi wana imani kubwa kwa Radio ambayo ni zaidi ya chombo kingine cha mawasiliano. Kuna mambo mengi na manufaa ambayo hufanya redio, hata leo hii kuwa katikati katika afya bora. Hivi ndivyo Profesa Enrico Menduni, mwandishi wa insha na msomi wa radio amesisitiza. Na kwamba hali halisi ya afya  duniani inabeba umri wake vizuri: maendeleo yake yanalindwa na unyenyekevu wake wa ajabu. Katika ulimwengu wa urekebishaji wa kiteknolojia unaoendelea, radio hudumisha kuegemea mara kwa mara. Ni ya bei nafuu, nafuu kwa mpokeaji na inahitaji vifaa vya gharama vya kawaida. Inaenea kupitia mtandao, masafa ya sumakuumeme na kebo na inaweza kutumika sana. Licha ya ushindani kutoka katika televisheni, radio iko katika hali nzuri kiafya.

Na akijibu ni kwa nini radio inaaminika na kusadikika amesema Radio ina kasoro kubwa na faida zake kubwa, awali ina hisia moja tu ya kusikia. Televisheni au sinema, kwa mfano, badala yake inatumia lugha ya sauti na taswira. Hii inaonekana kama hasara lakini, kiukweli, ni kipengele kinachofanya hadhira ya radio kuwa hai zaidi kuliko ile ya vyombo vingine vya habari. Ikiwa radio, kwa mfano, inazungumza juu ya farasi, ni msikilizaji ambaye lazima aunganishe: ikiwa farasi ni nyeupe, nyeusi, inaruka au imesimama, pia ni matokeo ya tafsiri ya kujitegemea na msikilizaji. Kwa hivyo radio ni chombo kinachokufanya ufikiri.

Msikilizaji lazima ajenge kwa upya, kuanzia na kusikia, yote ambayo yanakosekana. Jambo zuri ni kwamba, wakati farasi tunayemwona kwenye televisheni ni sawa kwa kila mtu, wakati mtangazaji wa radio ana pendekeza farasi wengi tofauti na wasikilizaji. Kuna aina fulani ya heshima kwa bioanuwai ya mawazo ya kila msikilizaji. Kwa upande wa Radio Vatican, ambalo linatimiza miaka 91 tarehe 12 Februari na ikiwa katika huduma y ana kuelekea katika wakati ujao ni kwamba Radio inatoa uwezekano wa kufikia wakati mmoja watu wote wa ulimwengu, matajiri na maskini na wale ambao wanazungumza lugha moja na wale ambao wanazungumza nyingine. Inauu wa nguvu wa ulimwengu. Radio ni chombo maalumu za ajabu cha kutuma ujumbe wa amani ulimwengu.

12 February 2022, 16:16