Tangu mwezi machi masaa mapya yanaanza kutumika katika Ofisi ya sadaka ya Kitume
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kwa kutoa uwezekano mkubwa wa kuongeza muda, kuna uwezekano sasa zaidi ka yule anapenda kwenda kuomba baraka ya kitume na kwa namna hiyo kutoa mchango wake wa upendo kwa Papa Francisko, sadaka hiyo ambayo inatumika kusaidia watu wengi wasio jiweza. Kwa maana hiyo kuanzia Jumanne tarehe Mosi Machi 2022, Ofisi ya Sadaka ya Kitume itafuata masaa mapya katika shughuli yake ya kila sikun kama ifuatavyo: Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumamosi, inawezekana kwenda kwenye ofisi iliyo njia ya Pellegrino kuanzia asubuhi saa 2.30 hadi saa 8.00 mchana, wakati masaa mapya yaliyoongzwa ni katika siku ya Jumanne na Alhamisi, ambapo inawezekana kwenda asubuhi kuanzia saa 2.30 hadi saa 12.00 jioni.
Shughuli za ofisi ya kitume ya Papa kwa ajili ya maskini na wahitaji
Mfuko wa kitume, una jukumu muhimu sana ambao umekabidhiwa kwa Papa ili kutoa chochote kwa ajili ya maskini na yule mwenye kuhitaji katika jamii nzima ya Kanisa na kijamii. Katika miaka hii, kiukweli haikukosekana kuona mipango mingi iliyo fanyika ya ubunifu wa upendo kama vile bahati nasibu ya ufadhili, iliyoanzishwa tangu 2014, lakini hata zawadi nyingine nyingi kama msaada kidogo wa fedha kwa ajili ya kulipa mahitaji na malipo ya umeme wa nyumba. Mto wa mshikamno ambao haukukatika kamwe kwa ajili ya kuwakimbilia watu na ambai unaweza kweli kuuongezeka, shukrani hata kwa njia ya baraka za kipapa. Ni mchango ambao unasaidia kuleta faraja katika mahangaiko na kuwafanya wahisi ule muungano katika kumtunza mmoja na mwingine na wote, kwa sababu sisi sote tumo katika mtumbwi mmoja, anathibtisha Papa Francisko katika kumjali ndugu mwenye kuhitaji.