Tafuta

2022.02.11 Katika Siku ya Wagonjwa duniani, Kardinali Turkson ameaonoza misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na kuwapaka mafuta ya mpako wagonjwa na wazee 2022.02.11 Katika Siku ya Wagonjwa duniani, Kardinali Turkson ameaonoza misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na kuwapaka mafuta ya mpako wagonjwa na wazee  

Kard.Turkson:Katika uponyaji kimwili,mwanadamu anaonja wokovu wa Yesu

Kardinali Turkson ameadhimisha Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro Vatican kwa ajili ya kuadhimisha Siku ya XXX ya Wagonjwa Duniani.Katika mahubiri ametafakari thamani ya faraja ambayo Mkristo anaitwa kutoa katika mateso:kuwa na huruma inaleta maana fulani kwa wataalam wote wa afya.Kwa kutazama Lourdes ambapo unatokea uponyaji wa udhaifu na maradhi ya mwili,Bikira Maria anawafanya wanadamu kuonja wokovu ambao Mwana wake anatoa.

Na Angella Rwezaula - Vatican

Kardinali Peter K. A. Turkson anaongoza mwaka huu katika adhimisho la Misa Takatifu katika Siku ya XXX ya Wagonjwa Duniani inayoongozwa na kauli mbiu "Kuweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Ijumaa tarehe 11 Februari 2022. Siku hii inaadhimishwa kwa kumbukumbu ya kutokea kwa Bikira Maria huko Lourdes ambaye, Kardinali amethibitisha katika mahubiri yake kwamba amewapa watu wengi ulimwenguni ishara ya huruma ya Mungu inayowasindikiza wanadamu wanaoteseka katika safari yao ya maisha. Kujiruhusu kuvutiwa na kuongozwa na mantiki ya huruma ya Mungu maana yake ni kurudi kwenye moyo wa chaguo la Kikristo. Kwa kupata huruma za Bwana, mtu hujifunza kuwa na huruma. Kardinali anarejea somo la kwanza lililosomwa kutoka katika Kitabu cha Nabii Isaya ambapo faraja ya Mungu inafanana na ya mama: “Kama mama amfarijivyo mtoto ndivyo nitakavyokufariji wewe”.

Kardinali Turkson akiongoza Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro katika Siku ya Wagonjwa Duniani
Kardinali Turkson akiongoza Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro katika Siku ya Wagonjwa Duniani

Kufariji kuna maana ya kutia moyo

Kardinali Turkson ameeleza kuwa faraja na kufariji kunamaanisha kutia moyo, kuhimiza, kupata furaha. Faraja ni huduma inayotolewa kwa watu, ambayo mfariji hutoa zawadi ya uwepo wake kwa wale ambao wakati huo wanaishi katika hali ya udhaifu, kwa kukaribisha hisia zake ndani yake mwenyewe. Na inafanya hivyo kwa kupata msukumo na nguvu kutoka kwa Mungu huyo ambaye daima katika historia amejifanya kuwa karibu na wanadamu, hivyo pia kuwa shuhuda wa kazi za Mungu zilizokamilishwa katika maisha yake mwenyewe.

Kardinali Turkson akiongoza Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro katika Siku ya Wagonjwa Duniani
Kardinali Turkson akiongoza Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro katika Siku ya Wagonjwa Duniani

Mungu ni muweza wa yote

Mada ya ushuhuda wa upendo wa Mungu uliopokelewa, ambayo inawafanya wengine wawe na matumaini ya kupokea huo huo, inaturudisha nyuma kwenye sehemu ya Injili ya leo ambapo tendo la Maria anakutana na binamu yake Elizabeth inasimuliwa baada ya malaika Gabrieli kumtangazi Maria na wakati huo huo Malaika pia alikuwa amemtangazia Bikira juu ya mimba ya Elizabeth kama uthibitisho na ushuhuda wa uwezo wa Mungu ambao, tayari unafanya kazi ndani ya Maria mwenyewe. Ziara kwenda kwa Elizabeti inazungumza juu ya upendo wa Maria kwa jamaa yake mzee, lakini pia ni uthibitisho kwa Maria wa maneno ya malaika. Elizabeth kwa hiyo alikuwa shuhuda wa Maria, kwa kile Mungu alichofanya kwa Elizabeth, na sasa anakifanya kwa Maria na kwa maana hiyo ndiup Maria anamtukuza Bwana katika wimbo wake wa sifa, amethibitisha Kardinali Turkson.

Kardinali Turkson akiongoza Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro katika Siku ya Wagonjwa Duniani
Kardinali Turkson akiongoza Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro katika Siku ya Wagonjwa Duniani

Haruma ya Mungu imeenea kizazi hadi kizazi

Huruma ya Mungu inaenea kutoka kizazi hadi kizazi, Kardinali Turksono amekumbuka, na kwamba “tunaadhimisha kama kila mahali wachungaji na waamini wanapokusanyika kwa jina la Bwana kuwapaka mafuta ya mpako wagonjwa. Hivi ndivyo hali ilivyo katika hospitali, nyumba za wazee, hospitali za wagonjwa na katika maeneo yote ambayo watu dhaifu zaidi hutibiwa. Katika maeneo haya, kuwa na huruma inapata maana maalum kwa wahudumu wote wa afya, ambayo Papa Francisko anazingatia sana na ambaye kila mana anakumbusha: “Mikono yako inayogusa mwili wa Kristo unaoteseka inaweza kuwa ishara ya mikono ya huruma ya Kristo katika Baba”.  Ka maana hiyo kuwa na huruma ni mafuta mazuri ya maisha, amesema Kardinali, na shukrani kwa Roho Mtakatifukwamba wote tunaweza kuwa “mafuta ya maisha kwa wengine”. Na amehitimisha kwa kuwaalika waamini watazame tena huko Lourdes ambapo katika uponyaji wa udhaifu na maradhi ya mwili Bikira Maria anawafanya wanadamu kuonja ule wokovu ambao Mwana wake anautoa.

Kardinali Turkson akiongoza Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro katika Siku ya Wagonjwa Duniani
Kardinali Turkson akiongoza Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro katika Siku ya Wagonjwa Duniani
11 Februari 2022, 16:14