Tafuta

2022.02.21 Kanisa Kuu la Maria Mpalizwa la Oria,Brindisi, Italia 2022.02.21 Kanisa Kuu la Maria Mpalizwa la Oria,Brindisi, Italia 

Kard.Parolin:leo hii kila kitu kinawekwa kitakatifu,kwa Wakristo altare ni kitovu cha imani

Katibu wa Vatican aliongoza Misa Takatifu Jumapili tarehe 20 Februari 2022 katika Kanisa Kuu la Oria,katika Wilaya ya Brindisi nchini Italia mara baada ya miaka mitatu kufungwa kwa sababu ya ukarabatiwa kwake.Katika mahubiri yake amesema kwamba leo hii kila kitu kinawekwa kitakatifu,lakini kwa waamini wakristo Altare inabaki daima kuwa kitovu cha imani.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Paa na mfano wa mtumbwi katika ndiyo maelezo ya mambo ya ndani. Kanisa Kuu la Oria, ni moja ya Kanisa lenye urembo mashuhuri wa usanifu wa Salento, ambalo limezaliwa kwa upya kutoka katika vumbi la kazi ya ujenzi, shughuli ambayo imedumu kwa miaka mitatu na katika uzuri huo uliopatikana unaweza kuona ishara ya uhusiano, wa ule wa Yesu ambaye anawezesha kuzaliwa kwa upya na kubaki na uhai. Ni katika tafakari ya Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican wakati wa ibada ya misa Takatifu aliyoongoza Dominika tarehe 20 Februari 2022 , lililojengwa katika mji wa Puglia katikati ya karne ya XVIII na kufungwa mnamo 2019 kwa ajili ya kulifanya kazi  za ukarabati ambazo zimelidumisha na kulirekebisha kwa upya.

Askofu anafundisha kwa ushuhuda wake

Katika mahubiri ya Ibada ya Misa Takatifu, Katibu wa Vatican  Kardinali Parolini amewapatia hata  salamu kutoka kwa  Baba Mtakatifu Francisko kwa waamini na kuwakumbusha Askofu Vincenzo Pisanello wa Oria, pamoja na waliokuwa wanashiriki misa pamoja (wakonselebranti) na waamini juu ya jukumu la Kanisa kuu.  Kwa mujibu wa Kardinali alisema, Kanisa ambalo ni  kiti cha askofu, ni mahali ambapo mafundisho ya mamlaka yanatolewa kwa jumuiya, lakini tutakuwa na makosa ikiwa tutafikiri kwamba mafundisho ya askofu ni orodha ya  kwanza  ya sheria. Kinyume chake Mafundisho yake, ni ushuhuda wa mkutano na uzoefu wa maisha, badala ya kuwa mfumo wa mafundisho. Na kuta za jengo ni ishara kwamba watu mbalimbali, wanaotoka sehemu mbalimbali na uzoefu wao mbali mbali, wanakuwa watu wamoja, ambao wameunganishwa na Neno la upendo na pamoja na askofu kitovu cha umoja wa imani, Kardinali Parolin alithibitisha.

Altareni ni mahali pa utakatifu wa kweli

Walakini, Kardinali ameonya kuwa ukweli huu hauangazi kila wakati katika tabia ya watu, kwa kiasi  kikubwa mara nyingi watu wengi huvutiwa na liturujia nyingine. Na kwa kutoa mfano amebainisha kuwa ni kwa muda sasa, jamii ya kisasa imekuwa ikisherehekea ibada nyingi katika maeneo mbalimbali kama vile katika vituo vya ununuzi ambavyo vinaonekana kuwa mali ya ukoloni wa wakati wetu. Siku za Jumapili, kabla ya janga kutokea, viwanja vya michezo vilikuwa vinatembelewa zaidi kuliko makanisa na vilikuwa mahali pa ibada takatifu, za kuzingatiwa kwa uangalifu. Lakini tukichunguza kwa makini, mahali pa kweli panapotengeneza muungano kwa ajili yetu sisi Wakristo ni na lazima daima kubaki kuwa altare ambayo furaha ya kukutana na Kristo inafanywa kwa upya ili kwamba hakuna uzee katika umri na ugonjwa wowote wa maisha, kadiri umri unavyosonga mbele , alihitimisha  Kardinali Parolin.

21 February 2022, 15:52