Jubilei ya 2025 ni fursa ya kuamka tena ulimwengu wote kwa upya!
Na Angella Rwezaula, – Vatican.
Katika Barua ya Papa Francisko iliyochapishwa mnamo tarehe 11 Februari 2022 kwa kuelekezwa kwa Askofu Mkuu Rino Fisichella, anaandika kwamba: “Jubilei ya 2025 inaweza kusaidia kurudisha hali ya matumaini na imani, kama ishara ya kupyaisha kuzaliwa kwa upya ambapo wote tunahisi udharura huo”. Baba Mtakatifu Francisko aidha amefafanua juu ya kauli mbiu ya “ Hija ya Matumaini” iliyochaguliwa kwa ajili ya Mwaka Mtakatifu wa kawaida unaokaribia na ambayo ilitangazwa wakati Ulimwengu mzima ukiwa bado umo ndani ya wimbi la nne la Janga la uviko. Katika barua Baba Mtakatifu anamweleleza kwa uhakika Rais wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji Mpya, Baraza ambalo limepewa jukumu la kuandaa vema Jibilei na kumkabidhi uwajibikaji wa kutafuta mitindo inayofaa ili Mwaka Mtakatifu uweze kuwaandaliwa vema na kusheherekewa kwa imani ya kina, matumaini hai na upendo hai. Katika barua hiyo Papa anasisitiza jinsi ambavyo inatokea kwa kawaida Barua ya mwongozo, ambayo itatangazwa muda mwafaka na ambayo itatoa maelekezo kamili kwa ajili ya kujiandalia na Jubilei ya 2025, lakini ambapo anaelekeza tayari baadhi ya mambo muhimu ya Mwaka Mtakatifu ujao na anakumbusha kuwa, kwa upande wa watu wa Mungu ni zawadi maalum ya Neema.
Askofu Mkuu Rino Fisichella ametoa maoni yake kuhusu Barua ya Kipapa iliyoelekezwa kwake akizungumza kwenye vipaza sauti vya Radio Vatican. Akizungumzia juu ya kuzaliwa kwa upya kama alivyoandika Papa, amesema haiwezekani kusahau kwamba tofauti ya Jubilei ya 2016 ni Jubileio ya kwaida na katika Historia ya Kanisa, Miaka Mitakatifu ya kawaida mara nyingi imejikita katika matukio ya kihistoria ya kisasa. Inatosha kufikiria mwaka ule wa 50, wakati Papa Pio XII alivyotaka kujenga kwa upya hali halisi ya imani mara baada ya vita ya II ya dunia au ile ya 1975, ambapo Papa Paulo VI aliifikiria kama kipindi muafaka cha kina cha umoja ndani ya Kanisa, mara baada ya mivutano iliyojitokeza baada ya mitaguso. Baadaye kufikiria mwaka wa 2000 ambao uliwakilisha kuingia kwa Kanisa katika Milenia ya Tatu ya Historia yake. Leo hii, katika Barua yake Papa Francisko, Askofu Mkuu Fisichella amebainisha kuwa anatuambia bayana kwamba tumeishi na tupo tunaendelea kuishi bado katika miezi ya udhaifu na hofu, mambo ambayo tumegusa kwa mkono hasa kwa ukosefu wa usalama na kwa bahati mbaya hata vifo, na kwa namna ambayo sasa tunapaswa kutazama wakati ujao na jinsi gani ya kuweza kujenga kwa upya miaka ijayo.
Askofu Mkuu Fisichella akijibu juu ya ufafanuzi wa Papa kuhusu kipengele cha “Jubilei ni zawadi ya neema” na nini maana ya Jubilei kwa Watu wa Mungu, amethibitisha jinsi yeye anavyoamini kwamba lazima kuweka moto kwa upya ule ambao ni asili yenyewe ya Jubilei. Tukio hili ambalo linatokea kila baada ya miaka 25 ni mwito hata kwa ajili ya kudumisha Maandiko Matakatifu yaliyomo katika Kitabu cha Walawi. Ni kipindi cha uongofu, cha kutoa jibu, na kipindi ambacho kinaingia katika uhusiano wa kina na Mungu, mtu binafsi na kazi ya uumbaji. Jambo hilo daima limeongoza kila Mwaka Mtakatifu. Ikiwa unafikiria kuwa katika maelekezo yanayotolewa katika kitabu cha Walawi, moja ya vitabu vitano vya Agano la Kale, Askofu Mkuu Fisichella amesisitiza kuwa tunapata maandiko yanayoelezea wazo kuwa watu, dunia wanyama wanapaswa kupumzika na kwamba mali zinarudi kuwa kwa watawala wake asili. Jubileio ni tendo la haki na kidogo kama vile kwa mfano ukutanavyo na mkulima anayegeukia ardhi ili kupanda mbegu kwa upya. Na ndiyo tazama maana yake ya Jubilei, ya kupyaisha maisha yetu ili kuweza kupanda chochote ambacho kinatuwezesha kuwa na imani na kuturuhusu kujenga kwa upya yale mahusiano kibinafsi.
Na matashi yake Baba Mtakatifu Francisko ni kuwa Mwaka wa Jubilei ujao uweze kusheherekewa hata kama fursa kwa ajili ya kutafakari uzuri wa kazi ya uumbaji na kusaidiana katika kutunza nyumba yetu ya pamoja. Hiyo ni kwa sababu ndiyo muktadha wa utunzaji kwa upande wa Papa Francisko na kama ulivyooneshwa katika Nyaraka zake mbili za ‘Laudato si’’ na baadaye ‘Fratelli tutti’. Kwa maana hiyo ukuu wa hija ni ule ambao unaonekana. Jubilei kiukweli lazima inandaliwa na kuishi katika nuru ya hija, maana ya kutembea kwa miguu. Hiyo kwa mara nyingine tena ni kuthibitisha kuwasiliana kwa mtu na asili na kila kitu kinachomzunguka. Historia ya hija inatufundisha kwamba daima vimekuwapo vipindi vyenye nguvu ya kiroho, kwa sababu mhujaji ni mtu anayeingia ndani kwa kina mwenyewe. Ni kipindi cha ukimya wa kina, sala, hasa cha ugumu mahali ambapo ni kutafuta msaada wa mahujaji wengine, lakini pia mahali pa kutafakari uzuri wa asili. Kwa maana hiyo umuhimu wa hija kwa namna nyingine unasaidia kutafakari kwa dhati. Kwa njia ya mchakato wa safari, unafika hatimaye katika Mlango Mtakatifu kuupitia na kwa hiyo kuingia kwa ishara hiyo ambayo ni ya kina na ndiyo Jubilei inawakilisha.
Jubilei 2025 itakuwa ni fursa ya kukaribisha mahujaji wengi kutoka ulimwengu mzima kuja Roma mara baada ya janga la UVIKO -19. Katika muktadha huo ni fursa ya kuzindua kwa upya baraka ya Ulimwengu. Lakini si tu kwa mji Mkuu. Mahujaji watakuja Roma, pia wengine kutoka Roma yenyewe na ambao wataelekea hata katika miji mingine mikuu ya Italia ambayo imejaa masuala ya kiutamaduni na kisanaa na zaidi katika uzoefu wa kidini. Askofu Mkuu Fisichela amesema ikiwa Roma ndiyo sehemu ya kwanza ya kuandaa makaribisho, kwa wakati wa Jubilei kwa namna nyingine inaweka harakati za kuzungukia ulimwengu mzima. Hatupaswi kusahau kuwa miaka hii ya janga imeangukia sana na kugusa katika muktadha wa safari, vizingiti vya kuzunguka kutoka sehemu moja na nyingine kwa njia Treni, Ndege na Meli. Kwa maana hiyo si katika mantiki ya kitalii lakini pia hata ile safari ya tafiti,mafunzo na kazi, vyote hayo yalifungwa. Kwa maana hiyo Jubilei kwa ajili ya Roma, Italia na kwa ulimwengu inajumuisha uhamsho wa dhati kwa wote. Fursa kwa ajili ya kuanza maisha tena ya daima na yake ya kila siku, lakini zaidi kwa ajili ya kupata ahadi tena ya kukutana kati ya watu. Kwa hakika ni kwamba Roma ndiyo kweli unapaswa uwe mji wa kwanza kukutwa uko tayari, umejiandaa kikamilifu!