Inatishia kusikia tu wanasema Vita Kuu ya Dunia
Na Angela Rwezaula - Vatican.
Kiongozi fulani mkubwa alianza kuzungumza. Inatia wasiwasi kusikia tu neno la kutamka: “Vita vya dunia”. Rais wa Marekani Joe Biden alishauri hivi karibuni wazalendo wa Marekani kuacha haraka nchi ya Ukraine kwa sababu mambo yanaweza kuwa ya wazimu kwa haraka. Ni vita vya dunia ikiwa wamarekani na Warusi wanaanza kupigana”. Inatia hofu kusikia kuzungumza juu ya vita vya dunia. Inashangaza neno pia lililitomuka la uwenda wazimu. Papa Francisko katika katekesi ya Jumatano iliyopita akiwaalika kwa nguvu ya kuendelea kusali kwa ajili ya amani mbele ya mivutano inayokuwa ya mgogoro wa Ukraine alisema: “Msisahau: vita ni wenda wazimu”. Alikuwa alikwisha sema mara nyingi kama vile kwenye Mkutano kuhusu “Mediteranea, mpaka wa Amani, uliofanyika mnamo tarehe 23 Februari 2020, ambao uliandaliwa na Baraza la Maaskofu Italia kwamba: “Vita (...) ni kinyume na akili (...) ni wazimu, kwa sababu ni wazimu kuharibu nyumba, madaraja, viwanda, hospitali, kuua watu na kuangamiza rasilimali badala ya kujenga mahusiano ya kibinadamu na kiuchumi. Ni uwazimu ambao hatuwezi kujikabidhi”. Ndivyo anatoa maoni yake Dk. Sergio Centofanti Makamu Mhariri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano kuhusiana na suala upepo unaovuma wa kivita kati ya Urusi na Ukraine.
Katika maoni yake Dk. Centofanti anaandika kuwa mnamo tarehe 13 Septemba 2014, katika Misa aliyoongozwa katika Kanisa la Kijeshi ya Redipuglia katika kumbukumbu ya miaka mia moja tangu ilipoanza Vita vya Kwanza vya Kidunia, Papa Francisko alisema kwa nguvu: “Vita ni wazimu. Wakati Mungu anatekeleza na kundeleza kazi yake ya uumbaji na sisi wanadamu tumeitwa kushirikiana katika kazi yake, lakini vita huharibu. Pia huharibu kile ambacho Mungu ameumba kizuri zaidi yaani mwanadamu. Vita huvuruga kila kitu, hata uhusiano kati ya akina ndugu. Vita ni wazimu, mpango wake wa maendeleo ni uharibifu wa kutaka kuendeleza kupitia uharibifu! Uchoyo, kutovumilia, tamaa ya madaraka ... ni sababu zinazosukuma uamuzi wa kuweka vita mbele, na sababu hizi mara nyingi huhesabiwa haki na itikadi; lakini kwanza kuna shauku, kuna msukumo potofu. Itikadi ni uhalalishaji, na wakati hakuna itikadi, kuna jibu la Kaini: “Ina umuhimu gani kwangu?”.
Katika muktadha huo Dk Centofanti anakumbusha juu ya maandikoa matakatifu kwa mujibu wa Papa alivykumbusha. "Mimi ni mlinzi wa kaka yangu? (Mwanzo 4:9). Vita haiangalii mtu yeyote: wazee, watoto, mama, baba ... “Ina nihusu nini kwangu?”. Juu ya mlango wa kaburi hili, kaulimbiu ya dhihaka ya vita inazunguka: “Inanihusu nini mimi? Watu hawa wote, wamelala hapa, walikuwa na mipango yao, walikuwa na ndoto zao…, lakini maisha yao yalivunjika. Kwa sababu gani? Kwa sababu ubinadamu umesema: “Ina umuhimu gani kwangu?” Hata leo hii, baada ya kushindwa kwa mara ya pili kwa vita vingine vya dunia, labda tunaweza kuzungumza juu ya vita vya tatu vilivyogawanyika vipande, na uhalifu, mauaji, uharibifu (...) Je! Inawezekana kwa sababu hata leo nyuma ya pazia kuna maslahi, mipango ya kijiografia, tamaa ya fedha na madaraka, kuna sekta ya silaha, ambayo inaonekana kuwa muhimu sana! Na wapangaji hawa wa ugaidi, waandaaji hawa wa mgongano, pamoja na wajasiriamali wa silaha, waliandika mioyoni mwao: “Inanihusu nini kwangu?”. Inafaa kwa wenye busara kutambua makosa, kuhisi maumivu, kutubu, kuomba msamaha na kulia.
Kwa kuhitimisha Dk. Sergio Centofanti anaandika kwamba katika karne iliyopita, baada ya maneno ya Papa Benedikto XV juu ya mauaji ya Vita vya Kwanza vya Dunia na yale maneno ya Papa Pio XII, juu ya vita ya Pili ambapo alisema: “Hakuna kinachopotea kwa amani. Kila kitu kinaweza kupotea na vita”. Mnamo mwaka wa 1963, Papa Yohane XXIII, mbele ya kukabiliwa na vitisho vya mzozo wa kinyuklia, kwa waraka wake wa “Pacem in terris” aliandika kuwa: “Wanadamu wanaishi chini ya jinamizi la kimbunga ambacho kinaweza kutokea wakati wowote kwa nguvu isiyoweza kuwaziwa. Kwa vile silaha zipo; na ikiwa ni vigumu kushawishi kwamba kuna watu wenye uwezo wa kuchukua jukumu la uharibifu na maumivu ambayo vita ingesababisha, haijatengwa kwamba tukio lisilotabirika na lisiloweza kudhibitiwa linaweza kuanzisha cheche inayoanzisha vyombo vya vita”. Katika historia tumeona cheche nyingi sana zikigeuka kuwa mioto mikali. Leo kitu pekee ambacho kinatutia hofu ni ukweli kwamba tunazungumza juu ya “vita vya dunia”. Katika vita vya Bosnia na Herzegovina vya miaka ya 90 ya karne iliyopita, watu wengi walionusurika wamerudia maneno ambayo yalisikika sawa, licha ya kuwa katika pande zinazopingana kwamba: “Sikuwahi kufikiria kwamba inaweza kutokea hapa tena”.