Dubai:Expo,vijana wa imani tofauti kuishi udugu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kuanzia tarehe 2 hadi 5 Februari 2022, katika wiki ambayo inaadhimishwa mwaka wa Pili wa Kimataifa wa Udugu wa Kibinadamu inayoadhimishwa kila tarehe 4 Februari, siku ambayo imetiwa saini kwa Azimio la vijana wapatao arobaini kutoka mabara yote na imani tofauti na wawakilishi wa dini kuu za ulimwengu pamoja na waamuzi wa kisiasa ni pendelezo la waandaaji, wanajadili jinsi ya kutekeleza kanuni za kuishi pamoja kwa amani na udugu kati ya watu wa tamaduni na mataifa tofauti, kufanya kazi pamoja katika mipango inayohudumia jamii na ulimwengu, kuhakikisha maisha bora ya baadaye kwa wote. Tarehe 2 Februari asubuhi, katika Banda la Vijana la Maonesho ya Ulimwenguni, juu ya mada: “Kukuza Udugu wa Kibinadamu, Waziri wa Masuala ya Vijana katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Shamma Al Mazrui, Jaji Abdulsalam, katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Umoja wa Mataifa na Andrea Fontana, balozi wa Umoja wa Ulaya katika Umoja wa Falme za Kiarabu, walizungumza na vijana wapatao arobaini kutoka duniani kote, waliokaribisha shukrani kwa mpango uitwao “Youth Majlis”, katika chumba cha mapumziko kwa vijana.
Huu ni mpango wa ushirikiano kati ya Kamati Kuu ya Udugu wa Kibinadamu, Umoja wa Ulaya na Mamlaka ya Vijana ya Umoja wa Falme za Kiarabu, uliotokana na lengo kuu la kuwapa vijana fursa ya kujenga uhusiano imara nchini kote ulimwenguni na unaohusishwa na ahadi ya Umoja wa Ulaya ili kusherehekea 2022 kama Mwaka wa Vijana. Kwa mujibu wa waandaani wamebainisha kuwa ‘Majlis ya vijana’, inalenga kuwaleta pamoja vijana na watoa maamuzi katika mazungumzo ya kushirikisha juu ya kile kinachohitajika ili kukuza udugu wa kibinadamu katika sekta mbalimbali. Kila mzungumzaji alielezea jinsi alivyojaribu kukuza nguzo tofauti za udugu wa kibinadamu katika uwanja wake kwa vitendo, na washiriki vijana baadaye waliuliza maswali katika mazungumzo ya wazi, ambayo yaliruhusu kubadilishana ukweli wa mawazo.
Yote hayo ndani ya mpango wa Tamasha la pili la Udugu wa Kibinadamu, ambalo linalenga kuhamasisha kanuni za Hati ya Udugu wa Kibinadamu kwa amani ya ulimwengu na kuishi kwa pamoja, iliyotiwa saini mnamo Februari 4, 2019 huko Abu Dhabi, kama vile amani, imani ya uhuru, uvumilivu, maadili, ulinzi wa maeneo ya ibada, mapambano dhidi ya ugaidi, uraia hai, mahusiano ya Mashariki-Magharibi, haki za wanawake, haki za watoto, ulinzi wa watu walio katika mazingira magumu.
Alasiri, takriban wanafunzi ishirini wa Vyuo Vikuu kutoka Falme za Kiarabu na nchi nyingine za ulimwengu, Waislamu, Wahindu, Wakristo na Wayahudi, walikuwa wahusika wakuu wa kikao cha uchoraji kwa masaa manne, kilichoongozwa na kikundi cha wasanii wa kimataifa kiitwacho: “We love art”, yaani “Tunapenda sanaa”. Katika chumba ndani ya Banda la Umoja wa Falme za Kiarabu, kinachoangalia paa kubwa lililo wazi la Al Wasl, kitovu cha Maonesho hayo, walichora pamoja katika roho ya udugu wa kibinadamu. Kufuatia na maelekezo ya awali ya Denise Schmitz, msanii mwanzilishi wa “Tunapenda sanaa”, na washiriki wake, lakini kulingana na unyeti wao wa kibinafsi, walichora tena kwenye turubai ya Picha ya “Gioconda di Leonardo” yaani ya “Mona Lisa ya Leonardo”, na kuendelea kwa kumbukumbu msanii Dali na uso wa ngamia na msanii wa Morocco.
Maria Yandulova, mbunifu kutoka Urusi na msanii wa “Tunapenda sanaa”, ambaye alisoma nchini Italia na kuolewa na mwanafunzi mwenzake wa Italia na baadaye kuhamia Dubai, anaamini kuwa ni vyema kwamba wasanii kutoka nchi mbalimbali wanaweza kuwafundishe vijana hao mbinu zilizosafishwa katika nchi zao. Hapo Falme za Kiarabu hakuna shule nyingine za sanaa, ni jambo jipya kwao pia. Na ana shauku juu ya mpango huo, kwa sababu sanaa ni lugha inayounganisha mataifa, haina vikwazo vya kidini, umri au jinsia. “Sisi sote ni sawa, tuna brashi sawa, rangi sawa tunayotumia kupitia macho yetu, kuleta hisia zetu kwenye turubai. Na hii ni nzuri. Kupitia sanaa tunaelewana, tunazungumza lugha moja”, alisema Bi Yandulova.
Karibu naye, alikuwa ni Zahra Khalifa, kutoka Wizara ya Uvumilivu na Ushirikiano wa Falme ya Nchi za Kiarabu, inayojishughulisha na vikundi vya uvumilivu katika vyuo vikuu, ambaye alisema kwamba wanachofanya ni kuwaleta wanafunzi na vyuo vikuu pamoja, kuwafanya wajulikane na kujenga uvumilivu katika mazoezi ya kila siku. Katika muktadha wa Umoja wa Falme za Kiarabu, alieleza, kwamba “uvumilivu ni sawa na udugu, na hiyo ndiyo maana ya kikao hicho cha uchoraji. “Kwetu sisi kuvumiliana sio tu kuvumiliana na mtu usiyemjua au kumpenda bali ni kutaka kujua, kujifunza kumpenda mtu wa tofauti na wewe na kuwa na akili timamu, kuelewa na kujifunza kutoka kwa tamaduni na watu mbalimbali, hata kama hukubaliani nao. Kwa hivyo haufungi tu na wale kama wewe na kutoka kwa tamaduni yako mwenyewe. Ni kuishi kwa maelewano na kujifunza kutoka kwa kila mmoja, kwa sababu ulimwengu unakuwa bora tu, ikiwa tutaunganisha nguvu”.
Jina lililochaguliwa kuongoza kikao cha uchoraji ni “Lamasat”, ambalo kwa Kiarabu linamaanisha “kuwasiliana”, na hapa wanafanya kupitisha sanaa ambayo ni lugha ya ulimwengu wote, na ni rahisi sana kuunganisha watu katika njia hii. Wasanii pia ni watu wanaounganisha tamaduni tofauti, kwa sababu ni maarufu. Chaguo la kupakwa rangi ya Mona Lisa ya Leonardo ni kwa sababu ni mojawapo ya michoro inayojulikana na inayopendwa sana katika historia. Na Salvador Dalì, ambaye ameelezea kwamba wakati ni kama udanganyifu, na kwamba: “tunaishi katika hali halisi ambayo inasonga haraka sana, na inatufanya tuelewe kwamba sio wakati wa kupoteza uhusiano kati yetu. Ngamia pia ni ishara ya jangwa, ambayo ni sehemu ya mazingira yetu, kulindwa kutokana na mabadiliko ya tabianchi.