Balozi wa Vatican huko Kiev:Vigumu kupata msaada,nikumtumaini Mungu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Jengo lililorushwa na kombora la Urusi, ambulensi iliyosimama kati ya mkanda wa gari la kivita na kizuizi cha farasi wa Friesian. Barabara kuu ambazo mizinga inapitia na kurushiana risasi. Wazimu wa Kiev, ambapo siku nne zilizopita msongamano wa magari haukuweza kuzuilika wa watu kwenda kula chakula cha jioni kwenye majengo, ambapo kwa sasa yote yamo katika picha za ukiwa ambazo wanafika mamia ya watu kutoka uwanja wa vita uliofunguliwa na Urusi huko Ukraine na kuashiria hali mbaya ambayo inapitia taifa zima tangu Alhamisi 24 Februari 2022. Katika mtego wa mapigano, raia hutafuta kimbilio chini katika misingi ya jiji au kwa miguu kuelekea mipakani, wakivuta toroli pamoja nao kama watalii kwenye likizo ya kipuuzi.
Shuhuda wa kile kinachotokea moja kwa moja huko Kiev ni Balozi wa Vatican, Askofu Mkuu Visvaldas Kulbokas, ambaye hatima yake, na ya wahudumu wake, haitofautiani na ile ambayo mamilioni ya wananchi wenzake wanapitia. Akihojiwa katika vyombo vya habari vya Vatican na Alessandro De Carolis amebainisha kinachoendelea kwamba: “Hili ndilo jambo langu kuu: jiji la Kiev, ambako niko na kujiruhusu kuzungumza, ni kubwa na watu chini ya milioni tatu tu, na sasa kwa siku hizi umegandishwa kabisa na hatua ya vita. Mbali na makombora ambayo yanapita na kwa hivyo watu kujificha wawezavyo, kwenye vyumba vya chini, kwenye vituo vya chini ya ardhi, swali linalonijia ni: wagonjwa wanafanya nini? Wagonjwa wenye aina yoyote ya ugonjwa, kwa sababu ni vigumu wagonjwa kutembe, ni vigumu kuzunguka, kutafuta msaada ... Je wanafanyaje?
Habari kutoka nchini humo zinarejesha taswira ya mji wa ajabu ambapo pamoja na huduma ya afya sasa ni vigumu pia kupata maji na chakula ...
“Ndiyo, kwa kujua kwamba siku ngumu zilikaribia, kila mtu alijaribu kukusanya baadhi ya vitu kwa ajili ya kuishi, lakini hizi zitaendelea kwa siku chache na kwa hiyo swali linakuja: nini kitatokea ikiwa hali hii itaendelea kwa siku kadhaa? Je, watabakia kula nini? Kwa sababu hakuna njia ya kuongeza mafuta sasa, na pia ni hatari kukaa katika vyumba, kwenye nyumba, ni vigumu kukaa katika maeneo ya kawaida ... Sisi pia, katika Ubalozi tunajaribu kukaa katika jengo la chini ambapo hatari ni ndogo ya kupigwa. Na kwa hiyo ni vigumu zaidi kwenda nje na kukuta baadhi ya maduka yako wazi, na sidhani kama yapo maduka yaliyo wazi au yana uwezo wa kuwa ma bidhaa, kwa sababu hata barabara zimekatika ... Nini kitatokea katika siku chache, ni swali kubwa”.
Tunaona picha na video za watu ambao wamekimbilia kwenye mapango kwenye andaki za chini ya ardhi, hasa wanawake na watoto wengi, ambao kwa hakika hawaelewi ni nini kimebadilisha maisha yao ghafla ...
“Hili ni swali jingine kubwa. Sisi watu wazima tunawapa watoto maandalizi gani? Kwa sababu labda mtu mzima anapitia mateso, lakini mtoto ... nilikuwa tayari nimekutana nchini Italia na katika nchi nyingine za Ulaya watu ambao walikulia wakati wa Vita vya Pili vya Dunia: ni mateso gani wanaendelea kuteseka hata leo hii ... kufikiri asubuhi ya leo kuhusu watoto wa Kiev: watakapokua, watakuwa na mtazamo wa aina gani kwa wengine walioishi siku za kwanza, miezi ya kwanza, miaka ya kwanza ya maisha chini ya risasi, chini ya makombora? Hili ni swali lingine kubwa ...
Je mko hali gani hapo ubalozini?
Katika ubalozi tunajua kwamba sisi tupo katika eneo la makazi ya kirais na kwa hiyo si mara moja kuwa uwazi wa wa jiji. Hata hivyo, unaweza kusikia makombora yakipita, unaweza kusikia milipuko na hata usiku wa jana , vita katika maeneo ya jirani ... Sisi pia, wafanyakazi wa Ubalozini tuko kwenye eneo cha chini ya Jengo tayari kukimbilia kwenye msingi huo, ikiwa tutaona hitaji la haraka. Lakini tuombe: tujiombee wenyewe, kwa ajili ya wengine, tuombe amani, tuombe kwa ajili ya uongofu wa kila mtu.
Je, ungependa kutoa wito gani?
Zaidi ya ombi, ninajiuliza swali mbele ya Mungu: Mungu wa milele ananiambia nini kuhusu hali hii? Nifanye nini na mimi? Na mimi, kama Mkristo, ninaelewa kwamba hakuna kinachotokea ambacho kimefichwa kwa Bwana Yesu na kwamba hata katika hali ngumu kama hiyo wito wangu ni kutafuta uongofu wangu lakini pia kujaribu kusaidia wengine. “Wengine” inamaanisha “wote”: kuongoka na kuhakikisha kwamba sio tu kupata amani, lakini pia udugu, na heshima kwa kila mmoja.
Kanisa linasali kwa ajili ya amani nchini Ukraine na litafanya hivyo kwa namna ya pekee tarehe 2 Machi kama alivyoomba Papa Francisko.Ni wakati ambao tunafikiria mtaunganishwa na nguvu ...
“Kwetu sisi, mnamo Machi 2 bado ni mbali, tunahitaji kufika huko. Tunaomba kwa ajili ya amani kila wakati, kwa sababu pia ni wakati unaotutia moyo, kwa sababu unachochea sala hii ya nguvu, ya amana kwa Bwana, ya dhamana kwa Bikira Maria, Mama wa wote na sio wa Kanisa la Wakristo tu. Sisi Wakristo tunajua kwamba Waislamu wanamheshimu sana Bikira Maria, hivyo tuunganishe maombi yetu na ya kwao pia, ili Bikira Maria atuombee sote”.