Tafuta

Papa Francisko amemteua Monsinyo Arnaldo Sanchez Catalan kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Rwanda. Papa Francisko amemteua Monsinyo Arnaldo Sanchez Catalan kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Rwanda. 

Askofu Mkuu Arnaldo S. Catalan Balozi wa Vatican Nchini Rwanda

Askofu mkuu mteule Arnaldo Sanchez Catalan alizaliwa Jimbo kuu la Manila nchini Ufilippin kunako tarehe 18 Septemba 1966 na historia inaonesha kwamba, anakuwa ni Balozi wa kwanza kutoka Jimbo kuu la Manila. Tarehe 25 Machi 1994 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre na kupokelewa kwenye Jimbo kuu la Manila. Tarehe 1 Julai 20021 akaanza diplomasia ya Kanisa sehemu mbalimbali.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Arnaldo Sanchez Catalan kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Rwanda na kumpandisha hadhi ya kuwa Askofu mkuu. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu mteule Arnaldo Sanchez Catalan alikuwa ni mshauri wa ubalozi wa Vatican. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule Arnaldo Sanchez Catalan alizaliwa Jimbo kuu la Manila nchini Ufilippin kunako tarehe 18 Septemba 1966 na historia inaonesha kwamba, anakuwa ni Balozi wa kwanza kutoka Jimbo kuu la Manila. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 25 Machi 1994 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre na kupokelewa kwenye Jimbo kuu la Manila.

Jimbo kuu la Manila linampongeza kwa kuteuliwa kuwa Balozi nchini Rwanda.
Jimbo kuu la Manila linampongeza kwa kuteuliwa kuwa Balozi nchini Rwanda.

Kitaaluma, Askofu mkuu mteule Arnaldo Sanchez Catalan ana shahada ya uzamivu katika taalimungu na sheria za Kanisa. Tangu tarehe 1 Julai 2001 alianza kutoa huduma yake kwenye diplomasia ya Kanisa na kubahatika kupelekwa kwenye Balozi za Vatican nchini Zambia, Kuwait, Mexico, Honduras, Uturuki, India, Argentina, Canada, Ufilippin na China, huko Taiwan. Kardinali Jose Advincula wa Jimbo kuu la Manila, amemshukuru Baba Mtakatifu Francisko kwa kumteuwa Askofu mkuu mteule Arnaldo Sanchez Catalan kuwa Balozi wa Vatican nchini Rwanda na hivyo kuandika historia ya Jimbo kuu la Manila kama Balozi wa kwanza kutoka Jimboni humo. Kwa niaba ya watu wa Mungu Jimbo kuu la Manila, Kardinali Advincula amempongeza Askofu mkuu mteule Arnaldo Sanchez Catalan kwa kukubali uteuzi wa Baba Mtakatifu Francisko. Watu wa Mungu Jimbo kuu la Manila wataendelea kumtegemeza kwa hali na mali katika maisha na utume wake wa kidiplomasia ndani ya Kanisa.

Balozi Rwanda

 

01 February 2022, 15:33