Tafuta

Papa Francisko tarehe 17 Januari 2022 amekutana na Rais wa Bosnia na Herzegovina. Papa Francisko tarehe 17 Januari 2022 amekutana na Rais wa Bosnia na Herzegovina.  (ANSA)

Rais Željko Komšić wa Bosnia na Herzegovina Akutana na Papa Francisko

Katika mazungumzo kati ya Baba Mtakatifu na mgeni wake, wameridhishwa na uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya nchi hizi mbili sanjari na dhamana na wajibu wa Mwenyekiti wa zamu ya Urais huko Bosnia Herzegovina uliopembuliwa kwa kina na mapana. Wamejielekeza zaidi katika masuala ya Kikanda na Kimataifa sanjari na upanuzi wa wigo wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, EU.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 17 Januari 2022 amekutana na kuzungumza na Rais Željko Komšić, Mwenyekiti wa zamu ya Urais wa Bosnia Herzegovina na baadaye, Rais amebahatika kukutana pia na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa mjini Vatican. Katika mazungumzo kati ya Baba Mtakatifu na mgeni wake, wameridhishwa na uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya nchi hizi mbili sanjari na dhamana na wajibu wa Mwenyekiti wa zamu ya Urais huko Bosnia Herzegovina uliopembuliwa kwa kina na mapana.

Baadaye walijikita katika hali ya mambo ya ndani ya nchi, kwa kukazia umuhimu wa utawala unaozingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi. Viongozi hawa wawili, walijielekeza kwenye masuala ya Kikanda na Kimataifa kwa kuangalia zaidi hali ya Nchi za Ulaya ya Mashariki sanjari na mchakato wa kupanua wigo wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, EU.

Bosnia
18 January 2022, 14:55