Mahmoud Ali Talaat Mahmoud, Balozi Mpya wa Misri Mjini Vatican
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 8 Januari 2022 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Bwana Mahmoud Ali Talaat Mahmoud, Balozi mpya wa Misri mjini Vatican ambaye ameoa na kubahatika kupata watoto wawili. Kunako mwaka 1986 alitunukiwa Shahada ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Marekani, nchini Misri. Tangu mwaka 1987 amewahi kufanya kazi katika Benki ya Biashara Kimataifa, MAE, Katibu wa Ubalozi wa Misri nchini Tanzania kati ya Mwaka 1991 hadi mwaka 1995, MAE huko Mto Nile kati ya Mwaka 1991 hadi mwaka 1996. Katibu wa Ubalozi wa Misri nchini Poland kati ya Mwaka 1996 hadi mwaka 2000 na Idara ya Ushirikiano wa Uchumi Kimataifa, MAE 2000 hadi 2002.
Aliwahi kuteuliwa kuwa ni Mshauri wa Ubalozi wa Misri nchini Ukraine kati ya mwaka 2002 hadi mwaka 2006. Mkurugenzi wa Ushirikiano kati ya Misri na Nchi za Ulaya ya Mashariki kati ya mwaka 2006 hadi 2007. Waziri na Balozi wa Misri nchini Ureno kati ya mwaka 2007 hadi mwaka 2011. Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Kiuchumi Kikanda kati ya Mwaka 2011 hadi mwaka 2014. Balozi wa Misri nchini Kenya na Mwakilishi wa Misri kwenye: Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP na Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani, UN-Habitat yenye makao yake makuu Jijini Nairobi, nchini Kenya kati ya mwaka 2014 hadi mwaka 2018. Aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Uhusiano wa Utamaduni Kimataifa kati ya mwaka 2018 hadi mwaka 2021. Alikuwa ni mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Misri na Japan kati ya mwaka 2020 hadi mwaka 2021.