Padre Guerrero Alves SJ .Mwenyekiti wa Uchumi Vatican, Padre Guerrero Alves SJ .Mwenyekiti wa Uchumi Vatican, 

Guerrero:tumepunguza gharama&tutaonesha hesabu zetu kwa mabaraza ya maaskofu

Katika mahojiano na Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Uchumi Vatican,amebainisha kuwa wigo la bajeti la Vatican linaongezeka kwa kujumuisha vyombo vipya.Makisio ya jumla yaliyotarajiwa kwa mwaka wa 2022 ni milioni 33 ikilinganishwa na 42 iliyokuwa inatarajiwa 2021:Kutozwa kwa gharama,bila kupunguza upendo wa Papa,badala yake kuongezaka.Hivi karibuni ripoti kuhusu fedha, itaoneshwa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kusaidia uchumi wa Vatican ili kukidhi mahitaji yake, kuhakikisha kwamba shughuli za kiuchumi hazisumbui au kuondoa uaminifu kutoka katika utume wa kusaidia umoja katika mapendo na utume wa uinjilishaji wa Kanisa, ndivyo Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Uchumi, Padre Juan Antonio Guerrero Alves,SJ anavyoelezea kazi ya idara yake ambayo ameiongoza kwa miaka miwili sasa. Katika mahojiano na vyombo vya habari Vatican kuhusu bajeti ya 2022, iliyofanywa na Dk. Andrea Tornielli, Mhariri Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, Padre Guerrero ametoa takwimu za bajeti mpya ya Vatican, ambayo mwaka huu imeongezeka kwa kiasi kikubwa kutokana na kuingizwa kwa vyombo vipya.

Katika mahojiano hayo  Mjesuti Padre Guerrero Alves amefupisha matokeo muhimu zaidi yaliyopatikana katika miezi ya hivi karibuni kama vule "Kuzuiliwa kwa gharama, bila kupunguza upendo wa Papa, bali kuuongezeka,  kutoa chanjo kwa wasio na makazi; ongezeko la misaada kwa makanisa yenye uhitaji, na wakati huo huo kupungua zaidi kwa mapato. Kuongezeka kwa mapato ya mali isiyohamishika na uwekezaji wa kifedha pamoja na miongozo ya siku zijazo. Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Uchumi, pia amezungumza juu ya mtindo wa uuzaji wa jengo la Sloane Avenue, huko London, kwamba ni operesheni iliyofanywa kwa uwazi na kwa mujibu wa sheria mpya za mikataba ya Vatican: Ofa kumi na sita zilipokelewa, na nne, zilichaguliwa, maa baada ya kufanya duru ya pili ya matoleo, na bora zaidi ilichaguliwa. "Mkataba wa mauzo umesainiwa na tumepokea asilimia 10% ya amana na kila kitu kitahitimishwa mnamo Juni 2022”, alibanisha Padre Guerrero.

Akiendelea na ufafanuzi wake katika maswali na majibu alisema:“Hasara ya kashfa inayodaiwa, ambayo imezungumzwa sana na ambayo sasa iko chini ya hukumu ya mahakama ya Vatican, ilikuwa tayari imezingatiwa katika bajeti”, na kwamba “Jengo hilo liliuzwa juu ya uthamini. tuliyokuwa nayo kwenye mizania na tathmini iliyofanywa na taasisi maalumu” alibainisha Padre Guerrero Vatican inaunganisha ahadi yake ya uwazi zaidi na udhibiti mkali wa rasilimali zake za kiuchumi. Mzunguko wa taasisi zilizojumuishwa umeongezeka kwa vitengo 30, na kufanya idadi ya taasisi zilizopo kwenye Bajeti kufikia 90”. Kwa maneno hayo, Padre Juan Antonio Guerrero Alves, Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Uchumi, alifafanua habari mpya za bajeti ya utume kwa mwaka 2022.

Pamoja na mipaka mipya, taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa Sekretarieti ya Uchumi iliyochapishwa kuna mapato ya euro milioni 769.6 na matumizi ya euro milioni 803, na upungufu wa jumla wa euro milioni 33.4, ikilinganishwa na milioni 42. ya euro iliyotarajiriwa mwaka jana.  “Bajeti, iliyoidhinishwa mwezi Desemba iliyopita, miezi mitatu mapema kuliko mwaka uliotangulia, pia ilipanua mtazamo wake kwa vyombo ambavyo, ingawa havihusiki kabisa na Curia ya Roma, inayonamilikiwa na Vatican au viko chini ya jukumu la Vatican, na  imeainishwa katika maelezo, ambamo inakumbusha kwamba vifungu vipya vya Baraza la Uchumi, vilivyoidhinishwa mwezi Julai iliopita, vimewezesha kuingiza hali halisi kama vile Hospitali ya Watoto ya Bambino Gesù, Makanisa yote  Makuu manne ya Kipapa jijini Roma na mahali patakatifu pa madhabahu ya Loreto, Pompei na Padova.

Padre Guerrero amesema kuwa: “na tayari tunatazamia mwaka ujao, pamoja na majumuisho zaidi, ili kuzuia zaidi vizingiti vya hatari”. Wakati huo huo, kwa Salio la Mwisho la 2021, ambalo linapaswa kuwasilishwa katika miezi michache, kufungwa kwa kila robo ya hebabu pia kumeanzishwa. Na kwa kueleweka, madhara ya janga la UVIKO-19, bado yana uzito wa vitu kwenye Bajeti, ingawa urejeshaji wa shughuli za kiuchumi unatarajiwa kwa mwaka 2022, kutokana na maendeleo ya michango kuwa midogo, ya mfuko wa Mtakatifu Petro, pamoja na fedha nyingine zinazostahiki, zinatarajiwa kubaki katika euro milioni 47.3, kama ilivyokuwa kwa 2021. Ikilinganishwa na utabiri wa mwaka jana, ukirejela hali halisi 60 iliyozingatiwa, matumizi yanafikia upungufu zaidi, kuanguka kwa 4 na hadi euro milioni 289.

Kwa mzunguko mpya, inaongezeka kwa euro milioni 10. Rasilimali nyingi zinazotolewa kwa ajili ya utume wa kiutume zimekusudiwa kusaidia makanisa mahalia katika shida na na muktadha maalum ya uinjilishaji (21%); kuwasilisha ujumbe wa Vatican (16%); kuhifadhi uwepo wake duniani (16%); kusaidia inada y ana Uinjilishaji Vatican (16%); kujhamasisha hisani na upendo (9%). Zaidi ya hayo, Sekretarieti ya Uchumi “inaendelea na dhamira yake ya kuboresha uwazi, ufanisi na uzuiaji wa gharama, hivyo kuhakikisha uendelevu wa Kiti Kitakatifu na kuhamasishaa utume wa Baba Mtakatifu. Ni safari ya subira na yenye uchungu, ambayo hupitia taratibu mpya na njia za uendeshaji”, kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Uchumi, Vatican.

29 January 2022, 15:35