Tafuta

2022.01.10 Matashi mema kwa wanadiplomasia 2022.01.10 Matashi mema kwa wanadiplomasia  

Decano wa Mabalozi amshukuru Papa kwa jitihada za maendeleo

Balozi Georgios F. Poulides kutoka Cyprus ni Dekano wa Mabalozi pamoja na wawakilishi wa Mashirika mbalimbali ya Kimataifa mjini Vatican,kwa niaba ya Mabalozi wenzake,amemshukuru Baba Mtakatifu kwa jitihada zake bila kuchoka katika maendeleo fungamani ya binadamu,kuhamasisha amani,kutia moyo,utambuzi wa wanawake,utetezi wa mazingira,wakimbizi na wahamiaji hasa katika kipindi cha dharura ya kiafya.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 10 Januari 2022 amekutana na kuzungumza na Mabalozi pamoja na wawakilishi wa Mashirika mbali mbali ya Kimataifa yenye uhusiano wa kidiplomasia na Vatican. Dekano wa Mabalozi Balozi Bwana  Georgios F. Poulides kutoka Cyprus,  kwa niaba ya Mabalozi wenzake pamoja na wawakilishi wa Mashirika mbalimbali ya Kimataifa mjini Vatican, amelezea alivyopata na heshima kubwa kwa mara nyingine tena kuwakilisha wao ili kumtakia heri na baraka na afya njema ya utume wake. Ametumia fursa kuelezea furaha ya kuweza kuishi pamoja naye katika mkutano huo ambao umewajaza mioyo yao matumaini na kuonekana ulimwenguni  ile alama, ya  wawakilishi wa Mataifa yaliyomzunguka Baba Mtakatifu. Mwaka ambao bado janga linaendelea umeona sura ya Papa  ikiendeleza jitihada bila kuchoka kwa ajili ya Amani, ya ujenzi wa mazungumzo, utetezi wa mazingira na ulinzi wa watu walio dhaifu zaidi na wasio na mlinzi. Kwa namna moja,  “opportune et inopportune”, amesema mwanadiplomasia huyo kuwa  Baba Mtakatifu alisisitiza bila kuchoka kwamba “hatuwezi kujiokoa sisi binafsi”. Na kama alivyoelekeza katika Waraka wa Fratelli Tutti kwamba “Janga ni jaribio la wakati wetu ambapo hakuna anayeweza kutoguswa,  awe binafsi au kwa pamoja”, kwa maana suala hili linagusa ubinadamu wote..

Kutokana na mgogoro wa kiafya uliotokana na UVIKO-19, haiwezekani kuondokana  nao na kurudi ukawaida na mateso lakini kwa kutafuta suluhishi mpya amabazo ziweze kubadilisha mitindo yetu ya maisha ya kuishi. Na kwa waraka wa Frattelli Tuuti, pia Baba Mtakatifu alipendelea kusisitizia mapinduzi ya kidugu ambamo wote wanaweza kuwa wadau kwa ajili ya wote.  Kuwa ndugu ina maana ya kuwa na nyumba ya pamoja. Dekano wa Mabalozi amesema huo ni ujumbe ambao unafanana n aule wa  Baba Mtakatifu alivyo ueleza hata katika Waraka wa Laudato si’ 2015. Kulikuwa na haja katika ujumbe wake kwenye miaka hii ambapo  umechangia pakubwa kuandaa ardhi yenye rutuba kwa ajili ya mabadiliko na mchakato wa sera za mazingira  mada ambayo inatawala sehemu kubwa ya Umoja wa Mataifa kama ile inayojulikana ya COP26 iliyofanyika huko Glasgow mwishoni mwa mwaka uliopita.

Kwa utambuzi ya kwamba matatizo yanaweza kutatuliwa kwa njia ya ushirikiano wa wote, Baba Mtakatifu alizindua na  kutia saini mjini Vatican, mnamo tarehe 4 Oktoba wito wa pamoja uliowaelekeza washiriki wa COP26, akiwa pamoja na makundi ya viongozi wakuu wa kidini na kisayansi ambao walikuwa wanaomba kuchukua hatua ya mafunzo ya ikolojia fungamani ambayo inasaidia mitindo ya utamaduni inayojikita juu ya udugu.  Waraka wa ‘Wote ni ndugu’ na ‘Nyumba yetu ya pamoja’ yaana Laudato si  ni ujumbe ambao kila mmoja anaweza kuulewa na ambao una thamani kubwa ya kimaadili na kisiasa, amesisistiza Dekano wa Mabalozi. Akiendelea amebainisha jinsi ambavyo Baba Mtakatifu anapenda uharaka wa kubadilisha dira ili kupita ule utamaduni wa kibaguzi  na kueleke utamaduni wa utunzaji wa nyumba ya pamoja, kwa sababu vijana hawatakuwa na sayari tofauti na ile ambayo tunawaachia(..). Huu ni wakati wa kufanya maamuzi ambayo yanawapatia wao sababu ya kuwa na imani ya wakat ujao (Ujumbe kwa  Bwana Alok Sharma, Rais wa COP26, mnamo 29 Oktoba 2021).

Dekano wa mabalozi amependa kukumbusha maneno ya Baba mtakatifu aliyotamka katika ujumbe wakati wa kuzindua Mkataba wa Elimu Kimataifa mnamo 2019:  “Kila mabadiliko yanahitaji mchakato wa elimu ili kufanya ukomae mshikamamo mpya wa ulimwengu na jamii moja yenye ukarimu zaidi”. Kwa maana hiyo nguvu ya ujumbe huo wa amani unakita ndani ya mwaka zaidi ambao umeanza. Mbele ya kuibuka kwa mateso mapya na kuongezeka katika majanga ya kizamani, Baba Mtakatifu anatoa suluhishi rahisi kuanzia na maono yenye vizingiti lakini kwa kuwaalika kujenga amani ya kudumu. Kila mmoja wao, amesema ni lazima ahisi kuwa mstari wa mbele katika kujenga dunia ya amani , kwa kujikita zaidi kwenye matendo yao katika miongozo mitatu ambayo Baba Mtakatifu aliibainisha vizuri ikiwa: “kujikia katika mazungumzo kati ya vizazi  kwa kuandaa mipango shirikishi; kuhamasisha elimu kama muktadha wa uhuru, uwajibikaji na maendeleo; kuhamasisha hali za kazi ambazo zinakamilisha hadhi ya binadamu (taz. Ujumbe wa siku ya amani Duniani Mosi Januari 2022)

Dekano amempongeza baba Mtakatifu juu ya kuwa na hisia maalum ya matatizo ya kibinadamu na ukosefu wa msimamo kijamii ambayo imeonesha kwa nguvu ya ziara yake katika moyo wa Ulaya, nchini Slovakia. Kwa hapo anasema aliweza kutetea hadhi na haki ya kazi kwa nmaneno ambayo amependekea kushirikisha”: Kama ilivyo bila mkate hakuna kumwilishwa, na bila kazi hakuna hadhi” (Mkutano na mamlaka ya rais na Wanadiplomasia Bratislava, 13 Septemba 2021).  Kwa maana hiyo amesema Papa anawaalika kujenga jamii ya haki na mshikamano ambayo inajikita juu ya Kazi ili pasiwepo na mtu anayehisi ametengwa na kulazimisha kuacha familia  na nchi yake asili kwa kutafuta mahali penye fursa zaidi. Katika sehemu ambazo bado zinakaa katika hali hiyo lazima kwamba dunia isigeuze kisogo upande mwingine.

10 January 2022, 18:22