Tafuta

2019.01.22 Siku ya Kimataifa ya wagonjwa wa ukoma 2019.01.22 Siku ya Kimataifa ya wagonjwa wa ukoma 

Kard. Czerny:Bado kuna tatizo la kunyanyapaa wagonjwa wa ukoma!

Tangu tiba ya dawa nyingi kuanzishwa katika miaka ya 1980,dalili za kimwili za ugonjwa ukomazimeweza kudhibitiwa na zimetoa matumaini ya kutokomeza kabisa.Hata hivyo, matukio ya ulimwenguni yanaonesha bado kuwa ya juu na wagonjwa mara nyingi wana matatizo mengi na kunyanyapaliwa.Ndivyo unasema ujumbe wa Siku ya 69 ya Ukoma Duniani mwwaka 2022.Ni ujumbe Katikaulitolewa na Kardinali Czerny.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ukoma ni ugonjwa mbaya, ingawa unaweza kuponywa,na ambao umepungua kwa miongo kadhaa. Tangu tiba ya dawa nyingi kuanzishwa katika miaka ya 1980, dalili za kimwili za ugonjwa huu zimeweza kudhibitiwa na zimetoa matumaini ya kuweza kuutokomeza kabisa ukoma kwa pamoja. Hata hivyo, “matukio ya ulimwenguni kote yanaonesha kuwa bado ya juu na wagonjwa mara nyingi wana matatizo ya muda mrefu yanayohusiana na ugonjwa huo. Ndivyo unaanza ujumbe wa Siku ya 69 ya Ukoma Duniani kwa mwaka 2022, uliochapishwa tarehe 30 Januari 2022. Katika ujumbe ulitolewa na Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa mpito wa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Maendeleo Fungamani ya Binadamu, unaeleza kwamba katika miaka iliyopita, kesi mpya 127,000 ziliripotiwa kwa kuonesha idadi ndogo zaidi ya miaka iliyopita, ingawa imeshuka kwa kuoneshwa kidogo na ripoti kutokana na wakati wa janga. Mbali na changamoto hizo zinazohusiana na ukoma   inaongezwa hali halisi ya kukatisha tamaa ambayo ni kunyanyapaa jambo ambali ni kizingiti kwa ujumla cha afya na kuponesha.

Idadi ya watu kunyanyapaliwa inakuwa kubwa zaidi

Shirika la Afya ulimwenguni (WHO) linabainisha kuwa watu milioni 3 na 4 wanaishi au kuwa na dalili za ukoma. Kwa sababu ya kunyanyapaliwa, ukoma na ulemavu husababisha kutengwa kwa jamii katika jamii nyingi watu hawa na idadi ya watu wanaopata kunyanyapaliwa na ukoma huenda ikawa kubwa zaidi. Kauli mbiu ya siku ya ukoma duniani kwa mwaka huu ni:  “Umoja kwa Hadhi”, kwa kupendekeza kwa kila mtu ambaye anauzoefu wa ukoma kwamba anayo haki ya kuishi maisha ya uhuru dhidi ya ugonjwa wa kunyanyapaliwa na kubaguliwa. Sehemu nyingi za duniani mahali ambapo ukoma upo kwa wingi, walioambukizwa wanaendelea kuishi nje na kutengwa na kusababisha matatizo mengi ya afya ya akili na kuendeleza mzunguko wa afya mbaya. Watu hasa tu tu kuwa na ugonjwa wa kimwili, lakini pia wanafanya uzoefu wa shinikizo la kisaikolojia na kutengwa hadi kufikia wao kujinyonga.

Maono fungamani ya kiroho na kimwili

Maono fungamani ya afya yanagusa mwili ikiwa ni pamoja na kiroho kwa kuwa na huruma kwa afya ya kisaikolojia na salikolojia ya mwili. Kunyanyapaa na kubaguliwa kunamwathiri mtu kisaikolojia na inahitaji uwajibikaji kamili wa kibinafsi na ufungamanishwaji kwa jumuiya nzima yenye kuwa na huruma. Katika waraka wa Fratelli tutti, yaani wote ni Ndugu, Papa Francisko amegusia Msemo wa Yesu kuhusu Msamaria Mwema aliyemsaidia aliyemkuta kando ya barabara akiwa amejeruhiwa na majambazi na kumfunga majeraha. Walipita baadhi ya watu, bila kumpatia msaada. Papa Francisko aliandika kuwa: “Hatuwezi kuwa wasiojali mateso; hatuwezi kuruhusu mtu yeyote kupitia maisha kama mtu aliyetengwa. Badala yake, tunapaswa kuhisi hasira, na changamoto ya kuibua kutoka katika kutengwa kwetu na starehe zetu ili kubadilishwa na mawasiliano yetu na mateso ya wanadamu”.  Kwa maana hiyo hiyp Kardinali anasisitiza katika ujumbe huo kuwa hiyo ndiyo maana ya hadhi. "Kuunganishwa kwa heshima kunamaanisha kugeuzwa, kwa kuona mambo kwa njia tofauti na kutenda ipasavyo".

Yesu alikutana na watu wengi wagonjwa aliwapokea bila kubagua

Katika Ujumbe wa siku ya ukoma duniani, unabainisha kwamba utunzaji kwa wale wenye ukoma lazima na kamwe usinyanyapae na kuwabagu kati yao. "Ni hadhi yetu ya pamoja ambayo inapiga magoji kwa pamoja. Yesu Kristo alitufundisha hali halisi ya maana kubwa kwa maneno yake, na hata mifano yake ming"i. Papa Francisko alieleza kwamba: “kwa kupitia huduma yake alikutana na watu wengi wagonjwa wengi; aliwabeba katika mateso yake; alibomoa kuta za unyanyapaa na kutengwa ambazo zilizuia wengi wao kuhisi kuheshimiwa na kupendwa. Kwake Yesu, ugonjwa kamwe sio kizuizi cha kukutana na watu, badala yake ni kinyume chake. Alitufundisha kwamba mwanadamu sikuzote ni wa thamani, sikuzote amepewa hadhi ambayo hakuna chochote na hakuna mtu anayeweza kufuta, hata magonjwa.”

Ili kupunguza kunyanyapaa lazima kufanya vipimo mapema na tiba inayofaa

Wataalam wakubwa wanasema kwamba labda moja ya matokeo ya njia za kupunguza unyanyapaa ni kuanza vipimo mapema na matibabu yanayofaa. Janga la UVIKO-19 limefanya mahali pengi katika ulimwengu kuwa na matatizo hasa ya kutunza kwa ujumla. Lakini si changamoto ambayo inaweza kubadili hadhi ya mtu binadamu, awe wa kike au kiume kwa sababu hadhi yake haiwezi kukiukwa na ni yenye thamani katika jamii na wakati hadhi ya binadamu ikiheshimiwa na haki zake kutambuliwa na kuhakikishwa, ubunifu na kutegemeana husitawi kupitia matendo ambayo yanaendeleza wema wa wote.  Haya yatakuwa ni matokeo ya mwisho ya kuunganishwa kwa hadhi, matunda ya ubunifu unaowezesha jamii na watu binafsi kutambua thamani ya kila mtu, hasa wale wanaougua magonjwa na ulemavu, unasisitiza ujumbe huo. "Ili kujibu muafaka wa changamoto ya ukoma tunaweza kufahamu kwani dawa na teknolojia zimetoa usaidizi na tiba ambazo hazikuwahi kupatikana hapo awali. Ugunduzi wa mapema na matibabu ya dawa nyingi huendelea kuleta matumaini na uponyaji kwa maelfu. Kilichobaki kwetu sasa ni kusonga mbele tukiwa tumeungana kwa hadhi, tukitumaini kwamba tutaona pia unyanyapaa na ubaguzi ukididimia. Mama yetu, Msaada wa Wagonjwa, aendelee kutuombea, ili tuweze kutambua kuwa watu wote wanayo hadhi na thamani ya pekee ambayo Mungu ameikabidhi kwa familia ya kibinadamu".

30 January 2022, 14:19