Askofu Mkuu Peña Parra:onyo la kutokuhukumu bila upendo
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Katika kurasa za Gazeti la Osservatore Romano limeweka mahubiri ya Askofu Mkuu Edgar Peña Parra, Katibu Msaidizi wa Mambo ya Sekretarieti ya Vatican, wakati wa Ibada ya misa katika Kikanisa cha Paulina, mjini Vatican katika fursa ya uzinduzi wa Mwaka wa Mahakama ya Kitume, tarehe 27 Januari 2022, taasisi inayojikita kwa lengo la kichungaji ambalo hasa ni usimamizi wa haki katika Kanisa, kwa niaba ya Papa.
Kipimo mnacho pima ndicho mtapimiwa
Akirejea kifungu cha Injili kilicho kuwa kimependekezwa na liturujia ambayo inahusu hukumu fupi za Bwana Yesu, Askofu mkuu Parra alirudia kusema kwamba hakuna jambo la siri ambalo halipaswi kufichwa na hakuna lililofichwa ambalo halipaswi kufichuliwa. Kana kusema kwamba, ukweli hatimaye utadhihirika kwa sababu unatokana na Nuru ambayo ni Yeye Bwana, kwa hiyo ni mwanga kwa asili na huepuka giz na kujifanya na ili kuwa na uwazi. Na pia hukumu ya pili iliyo kuwa inapendekezwa na liturujia ni fasaha kwamba: “Zingatieni kile mnachosikia. Kwa kipimo kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa”. Huo ni mwaliko wa nguvu, alisema askofu mkuu, kujihadhari na hukumu za kijuujuu tu na bila upendo. Yesu anatuomba tuhukumu jinsi tunavyotaka kuhukumiwa sisi wenyewe kwa ukaribu huo ambao nidhamu mpya juu ya sababu za ndoa zinapendekeza,na ambayo ni kitu kingine kabisa ikilinganishwa na kukubali hatia au kutoeleweka kufanya wema; ni, kwa neno moja, upendo. Ambalo ni sawa na kuwekwa chini ya macho ya Mungu yenye huruma na haki”, alisisitiza Askofu Mkuu.
Hakimu ajitoe kwa upendo
Lakini Je, kiukweli, mchakato huo ni nini kama si utafutaji makini, wa dhati na kamwe usio rasmi wa kutafuta ukweli? aliuliza Askofu Mkuu. Kwa kuongezea alisema, Mtakatifu Yohane XXIII, alifafanua mchakato huo kuwa huduma ambayo lazima itekelezwe kwa ukweli na kwa kupendeleza ukweli. Ni kweli kwamba kazi bado ni suala la ukweli wa kiutaratibu, ambao humpeleka mwamuzi mwaminifu kwa unyenyekevu, wenye afya na wajibu. Na bado juhudi lazima zilenge kuhakikisha kwamba ukweli wa kiutaratibu, hata ikiwa ni mdogo na sio mkamilifu kama ulivyo wa kibinadamu, unalingana, kwa kadiri iwezekanavyo na ukweli halisi, hasa msingi wa takwimu. “Hakimu hawezi na hapaswi kuridhika na ulinganifu wa baridi na usio na maana na sheria za nje lakini kwa kujitolea kwa uaminifu na halisi kwa kujitoa na upendo kwa kadi alizonazo mbele na nyuma ambazo daima kuna watu waliojeruhiwa, ni wajibu wa kuingia kwa uangalifu katika kesi inayohusika na kuhukumu wakati huo huo kwa haki na huruma. Mchanganyiko wa fadhila hizi mbili una jina la juu sana liitwalo aequitas, yaani ule wa haki iliyotiwa moyo na utamu wa huruma.
Upendo unaogeuka kuwa ukaribu na ukaribu kuwa huruma
Uhusiano wa hakimu na sheria, kwa hivyo hauwezi kuacha katika uasilia au wema wa juu juu ambao unaweza kushawishi kuupuuza kwa urahisi, au kwa utaratibu ulio kavu na baridi. Kawaida lazima itumike kwa kuzingatia mwisho, uwiano wa kawaida wenyewe, ambao mara nyingi huithibitisha na hata kuvuka:"Hapa basi ni thamani ya equitas kwa heshima na strictum jus, ambayo ni halali kwa kila aina ya hatua, lakini hasa kwa wale wahalifu. Kimsingi, ni swali, kwa maana ya kweli ya Kikristo, ya upendo unaogeuka kuwa ukaribu na ukaribu unaogeuka kuwa huruma alihitimisha, akikumbuka maneno ya Papa kuhusu Mtakatifu Joseph kuwa "Upole ni njia isiyotarajiwa ya kutenda haki".