Tafuta

Sala kwa ajili ya Ukraine iliyoongozwa na Askofu Mkuu Gallagher, Katibu wa Vatican wa mahusiano na ushirikiano na nchi. Sala kwa ajili ya Ukraine iliyoongozwa na Askofu Mkuu Gallagher, Katibu wa Vatican wa mahusiano na ushirikiano na nchi.  (ANSA)

Askofu Mkuu Gallagher:wahusika wakuu wajihusishe na amani kwa ajili ya Ukraine

Katika kujibu mwaliko wa Papa,Jumatano tarehe 26 Junuari usiku katika Kanisa la Mtakatifu Maria Trastevere,Katibu wa Vatican kwa ajili ya Mahusiano na Ushirikiano na Mataifa ameongoza sala Maalum kwa ajili amani katika taifa la Ulaya Mashariki,kwa kutoa wito wa nguvu kwa wahusika wa mataifa wasisubiri kufikia mikataba bali kufanya jitihada wote za kupyaisha mioyo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kwa kuunganika pamoja kusali kwa ajili ya amani kwa ajili ya nchi ya Ukraine, waamini katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria, huko Trastevere Roma waliweza kujibu wito wa Papa Francisko ambaye Jumatano asubuhi tarehe 26 Januari wakati wa Katekesi yake kwa  mara nyingine tena aliweza kusali na kuomba wakristo wote kufanya hivyo, ili katika moyo wa Ulaya ujazwe na udugu badala ya chuki na tishio. “Tunyamazishe upepo wa vita, wanaume, wanawake na watoto walindwe majeraha na balaa la migogoro”.

Kuna wanaoanzishwa na waoteseka na migogoro

Aliyeongoza tafakari ya sala hiyo alikuwa ni Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Ushirikiano na Nchi ambaye alisema kuunga mkono wito wa  Papa Francisko na  kila anzisho liwe kwa ajili ya huduma ya udugu wa kibinadamu. Katika maneno yake, awali ya yote yalimulika hali ya kushangaza ya migogoro na tofauti iliyopo kati ya wale wanaoiamua na wale wanaoteseka, kati ya wale wanaoitekeleza kwa utaratibu na wale wanaosumbuliwa na maumivu yao.

Vita ilivyo kali na matokeo yake mabaya

Askofu Mkuu alisema hizi ni hali chungu zinazowanyima wanaume na wanawake wengi hata haki za kimsingi. Lakini cha kusikitisha zaidi ni kuona kwamba wanaoteseka zaidi na migogoro sio wale wanaoamua kuianzisha au kutoianzisha, bali zaidi ya wote ni wahanga walio wanyonge zaidi tu. “Ni huzuni kiasi gani katika mgawanyiko wa watu wote unaosababishwa na mkono wa mwanadamu, kwa vitendo vilivyohesabiwa kwa uangalifu na kufanywa kwa utaratibu, na sio kwa hasira, au kwa majanga ya asili au kufanywa kwa nguvu za kibinadamu”.

Tujitambue sisi ni ndugu

Matukio haya yameenea sana leo hii, amebainisha Katibu wa Mahusiano na Mataifa, kwamba hayawezi kushindwa kutufanya tutambue sisi sote kama walioshindwa katika ubinadamu wetu na wakati huo huo wajibu wa pamoja wa kukuza amani. Lakini Mungu alituumba sisi kuwa ndugu na kwa hiyo, tukifahamu hali hii na kubeba mioyoni mwetu janga la migogoro inayosambaratika ulimwenguni, tunajitambua kuwa ni ndugu wa wale wanaowasababisha na wale wanaopatwa na matokeo, na katika Yesu Kristo tunawasilisha kwa Baba jukumu kubwa la wa kwanza na maumivu ya mwisho. Kwa wote tunaomba zawadi ya amani kutoka kwa Bwana”.

Tuombe amani na maridhiano yafikiwe

Askofu Mkuu Gallagher alisema: “Tunaomba amani, lakini bila kujiwekea kikomo katika kungoja mapatano na maridhiano yafikiwe na kuheshimiwa, lakini tukisihi na kujitolea ili hadhi mpya uzaliwe upya ndani yetu na katika mioyo yote”, tukiwa tumeunganishwa katika Kristo anayeishi kwa amani na kuamini, kwa nguvu ya amani”. Amani ni inaambukiza alirudia kusema Askofu Mkuu Gallagher, huku akinukuu maneno ya Papa aliyosema wakati wa kukutana na kikundi cha Wanadiplomasia na kwamba alionesha hii aahdi ya kutaka ulimwengu uwe na amani. Kwa hiyo wito wa mwisho amesema “Roho Mtakatifu awafanye watu wote, hasa viongozi wa mataifa, watenda kazi kwa ajili ya amani”.

27 January 2022, 16:12