Tafuta

Papa Francisko amemteua Askofu mkuu Charles Daniel Balvo kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Australia. 17 Januari 2022. Papa Francisko amemteua Askofu mkuu Charles Daniel Balvo kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Australia. 17 Januari 2022.  (Vatican Media)

Askofu mkuu Charles D. Balvo Balozi Mpya wa Vatican Nchini Australia

Askofu mkuu Charles D. Balvo alizaliwa tarehe 29 Juni 1951 huko New York nchini Marekani. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 6 Juni 1976 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo kuu la New York. Baada ya uzoefu na utume katika diplomasia ya Kanisa tarehe 1 Aprili 2005, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu mkuu na Balozi.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Charles Daniel Balvo kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Australia. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Charles Daniel Balvo alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Jamhuri ya Watu wa Czech. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Charles Daniel Balvo alizaliwa tarehe 29 Juni 1951 huko New York nchini Marekani. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 6 Juni 1976 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo kuu la New York.  Baada ya uzoefu na utume katika diplomasia ya Kanisa tarehe 1 Aprili 2005, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu mkuu na Balozi wa: New Zealand, Fiji, Visiwa vya Marshall, Micronesia, Shirikisho la Visiwa vya Pacific, Vanuatu, Tonga na Kiribata. Akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu tarehe 29 Juni 2005.

Tarehe 25 Machi 2006, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican kwenye Visiwa vya Cook na Samoa. Tarehe 30 Januari 2007 akamteuwa tena kuwa Balozi wa Vatican huko Nauru. Ilikuwa ni tarehe 17 Januari 2013 Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI alimpoteua kuwa Balozi wa Vatican nchini Kenya na Mwakilishi wa Vatican kwenye Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani UN-Habitat yenye Makao yake makuu Jijini Nairobi. Tarehe 21 Desemba 2013 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican Sudan ya Kusini na tarehe 21 Septemba 2018 akamwamisha na kumpeleka kuwa Balozi wa Vatican Jamhuri ya Watu wa Czech. Na hatimaye, tarehe 17 Januari 2022, Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu mkuu Charles Daniel Balvo kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Australia.

Uteuzi
17 January 2022, 15:33