Kanisa la uvumilivu ndilo linaombwa huko Cyprus katika nuru ya safari ya Sinodi
ANDREA TORNIELLI
Kutoka Cyprus, Papa Francisko, akizungumza na jumuiya ndogo ya Wakatoliki lakini iliyochangamka na hai, ametoa maelekezo yenye thamani kwa ajili ya mchakato wa safari ya sinodi ambayo Kanisa la ulimwengu ndio kwanza imeanza. Akikumbuka mtazamo wa Mtakatifu Barnaba, mtakatifu mlinzi na msimamiz wa kisiwa hicho, Papa ameeleza imani yake, usawa na zaidi ya yote uvumilivu. Alipochaguliwa kutembelea jumuiya mpya ya Kikristo ya Antiokia, inayoundwa na waongofu wapya kutoka upagani, mtume Barnaba alikutana na watu waliotoka katika ulimwengu mwingine, utamaduni mwingine, unyeti mwingine wa kidini. Watu ambao walikuwa na imani iliyojaa shauku, lakini ambayo bado ni dhaifu. Naye Barnaba akakaribisha, akasikiliza, akasubiri. Alijua jinsi ya kungoja mti ukue, kwa ilikuwa inahitajika uvumilivu wakati wa kuingia katika maisha ya watu wasiojulikana hadi wakati ule; kukaribisha mambo mapya bila kuhukumu kwa haraka; hekima ya utambuzi, ambayo inajua kuzishika ishara za kazi ya Mungu kila mahali". Zaidi ya yote, ni uvumilivu wa kuwasindikiza, tabia ambayo inamgusa sana Papa kwamba ni subira ambayo inatuwezesha kukua, kwa kusindikiza. Hi haikandamizi imani dhaifu ya wageni kwa misimamo mikali, isiyobadilika, au kwa maombi ya kulazimisha sana juu ya utii wa kanuni.
Akiendelea Papa anauliza "Je mabadiliko ya enzi tunayopitia sasa si mfanano huo? Je, hatupiti wakati ambapo utangazaji wa Injili unapata tatizo la kuangazia ulimwengu mwingine na tamaduni nyingine ambamo tumezama? Mbele ya bara la kizamani kukabliwa na maporomoko kuna kishawishi cha kujifungia katika mitazamo ya kusikitisha na ya kuomboleza, au kuota kwamba Kanisa linarudi kuwa pale lilipokuwa, linalofaa kwenye jukwaa la ulimwengu". Badala yake, Papa Francisko anaeleza, Kanisa lililogubikwa na mtikisiko wa imani, jinsi lilivyo sasa Ulaya ni vyema likapata msukumo kutoka katika mtazamo wa Barnaba na kuanza tena kutangaza Injili kwa subira, hasa kwa vizazi vipya kwa njia ya ushuhuda wa huruma. Kanisa la subira halitulii, bali liko wazi kwa matendo, lisilotabirika la Roho Mtakatifu. Halifanani kwa sababu linajua kwamba msingi wa mazungumzo yoyote ni mtazamo wa kiroho wa kusikiliza, yaani, kukaribisha na kutoa nafasi kwa wale walio na hisia au maono tofauti, kuthamini utajiri unaowakilishwa na tofauti ambazo Roho huleta pamoja umoja. Kumkaribisha mwingine ili kutoa nafasi kwa Mwingine. Ni Kanisa ambalo pia linajadili kwa uhuishaji lakini haligawanyi.
Papa Francisko akizungumza huko Cyprus na jumuiya mbalimbali katoliki za kisiwa hicho, amesema sio kufanya vita, si kwa kujilazimisha, bali kueleza na kuishi uhai wa Roho, ambao ni upendo na umoja. Kunakuwapo na mabishano lakini tunabaki kuwa ndugu. Kama vile inavyotokea katika familia. Hii ndiyo njia ya kwenda ili Sinodi isipunguzwe na kuwa jukumu lingine la ukiritimba wa kujumuishwa katika mipango ya kichungaji iliyosomwa mezani au katika mikakati ya masoko ya kidini, ambayo ni upropaganda wa kisasa,badala yake iwe kama fursa ya kupata uzoefu wa kuishi udugu. Papa amesema kwamba “Tunahitaji, Kanisa la kidugu ambalo ni chombo cha udugu kwa ajili ya ulimwengu”.