Tafuta

Tafakari fupi kwa njia ya video ya Majilio:Safari kuelekea kuzaliwa kwa Yesu

Injili ya Dominika ya III ya Majilio na tafakari fupi ya Padre Luigi Maria Epicoco,msimamizi wa Kikanisa cha Baraza la Kipapa la Mawasilainao inatusindikiza kuelekea kuzaliwa kwa Mtoto.Adventus” yanaongozwa na neno msingi ambalo ni moto.Yesu anakuja kuleta ubatizo wa moto kwa sababu imani katika Kristo haitoki katika hisia bali katika ukweli unaotia alama.

Padre Epicoco anasema kwa maana hiyo, Siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana inabadilisha historia kwa sababu inaashiria kuwa moto, kwani mbele ya moto kile kisichohitajika kinaisha na kile kinachostahili kinang'aa.

Adeventus, Safari kuelekea Kuzaliwa kwa Yesu

Katika Dominika ya II ya Kipindi cha Majilio, Padre Epicoco anabainisha juu ya "sauti". "Sauti inaweza kutuadaa au kuchanganya au kuongoza na kutupeleka  kunyoosha njia. Sauti pia zisizostarehesha lakini pia zilizojaa ukweli ambazo zinazotusaidia kukipatia kivuli jina ili kuweza kukaribisha nuru".

Adeventus, Safari kuelekea Kuzaliwa kwa Yesu

Na katika Injili ya Dominika ya I ya kipindi cha Majilio, Padre Luigi Maria Epicoco alisema:“Katika sehemu ya kwanza neno ni “janga". Kila wakati kila jipya hutokea kiwewe cha mgogoro. Hii ndiyo sababu hatuwezi kujiandaa kwa hali mpya ya Kuzaliwa kwa Bwana ikiwa sio kuanzia tena na mtazamo tofauti juu ya wa migogoro yetu wenyewe

14 December 2021, 16:27