Tafuta

Mji wa Vatican na Kanisa la Mtakatifu Petro Mji wa Vatican na Kanisa la Mtakatifu Petro 

Mkutano wa tathimini za bajeti ya 2022 na uwekezaji

Mkutano wa Baraza la Uchumi uliofanyika Jumatano 14 Desemba kwa uwepo wa wajumbe na wengine kwa njia ya mtandao ambao wameweza kujadili hata mpango wa shughuli za mwaka kesho.Mkutano ujao umepangwa kufanyika mwezi Februari 2022.

VATICAN NEWS

Tarehe 14 Desemba asubuhi na mchana ulifanyika mkutano ili kutathimini bajeti za mwaka na kupanga  mipiango ya miezi ijayo.  Ndiyo kilicho fanyika katika mkutano wa Baraza la Uchumi ambao umejikita kujadili juu ya Bajeti ya 2022 ya Vatican na muda mwingi wamejikita kujadili juu ya uwekezaji na mipango ya shughuli kwa ajili ya mwaka 2022 iliyowakilishwa na Mkaguzi mkuu. Haya yamesema na msemaji wa vyombo vya habari Vatican.

Mkutano huo ulimeudhuriwa kwa uwepo wa sehemu kubwa ya wajumbe wa Baraza, na wakati sehemu ndogo ilishiriki kwa njia ya mtandao , ambao umewaona sehemu hizo zikiongonzwa na Makamu mratibu mpya, Profesa Charlotte Kreuter-Kirchhof, na  rais wake Kardinali  Reinhard Marx, na kuwahusisha itihada nyingine za kitaasisi. Katika hitimisho la Mkuntano huo Kardinali aliandhimisha misa tarehe 14 Desemba 2021, saa saba mchana na wakati huo huo mkutano ujao unatarajiwa kufanyika mnamo mwezi Februari 2022.

16 December 2021, 16:32