Tafuta

Mahakama ya Kitume Vatican Mahakama ya Kitume Vatican  Tahariri

Kesi ya Jumba la London ni jaribio ambalo halijawahi kutokea!

Katika miongo ya hivi karibuni Vatican haijawahi kukabiliwa na uchunguzi na mchakato tata kama huu na kuwa na idadi kubwa ya washtakiwa.

ANDREA TORNIELLI

Mchakato ulioanza na kesi ya uuzaji wa mali ya London, na ambapo mchakato bado  upo katika hatua zake za awali zilizofuata na haulinganishwi kwa njia yoyote na uchunguzi na michakato ambayo Vatican imewahi kufanyika zaidi ya miongo ya hivi karibuni. Hili linadhihirika kwa idadi ya watu waliofanyiwa uchunguzi na baadaye kushtakiwa, kwa ushuhuda mwingi uliokusanywa na nyenzo za kompyuta zilizotumika, na kwa idadi na uzito wa uhalifu ulioshtakiwa, na hatimaye kwa utata wa matukio mbalimbali yaliyounganishwa. Yote  hayo yalianza na uchunguzi wa ndani ulioidhinishwa karibu miaka mitatu iliyopita na Papa Francisko, ambaye alisisitiza mara kwa mara umuhimu wa ukweli kwamba ripoti juu ya madai ya ukiukwaji, na malalamiko yaliyofuata, ambayo yametokana na mfumo wa udhibiti wa Vatican. Kwa maana hiyo inawezekana kusema kwamba kuanzishwa kwa kesi kuliwakilisha uthibitisho jaribio la mkazo halisi kwa mfumo wa mahakama ya mji wa Vatican.

Miongoni mwa mambo ya kipekee, hakika kulikuwa na ile ya kurejea kanuni ya utaratibu tofauti na ile iliyotumika nchini Italia, Finocchiaro Aprili ya 1913, ambayo baadhi ya sheria muhimu sana zimeongezwa katika nyakati za karibuni, lakini kwa hali yoyote ilikuwa kabla ya uchunguzi na kuzingatia yote ya sasa. Hili limezua matatizo ya kimalengo kwa sehemu zote za mchakato, ambazo zinaombwa kutumia kanuni hiyo kwa hali halisi ambazo mwanasheri wa karne iliyopita kwa hakika hangeweza kutabiri. Inatosha kutaja, kwa mfano, kushika au kukamata na matumizi ya nyenzo za mawasiliano (IT). Kwa upande mwingine, Ofisi ya Mhamasishaji wa Haki, Mwendesha Mashtaka wa Vatican, ambaye aliendesha uchunguzi kwa ushirikiano wa Kikosi cha Jeshi la ulinzi kama polisi wa mahakama, mara nyingi alilazimika kushughulikia masuala ya utata mkubwa na bila mfano: fikiria juu ya kiasi kikubwa cha nyaraka na barua nyingi muhimu za kujenga upya ule mtiririko wa fedha za  nje ya nchi ambazo zinaunda mfumo wa mashtaka.

Kama ilivyo kawaida mwanzoni mwa kesi yoyote, pingamizi za awali za washtakiwa zilikuwa na lengo lao fulani, maamuzi na baadhi ya tabia zilizopitishwa na Ofisi ya Mhamasishaji, kwa kuzingatia tafsiri tofauti za sheria inayotumika katika kesi maalumu. Hii ni awamu ambayo inaweza kufafanuliwa kama "physiological" wakati shughuli inayofanywa na mwendesha mashtaka wa umma inaletwa mbele ya hakimu na watetezi wanaitwa kutekeleza kazi yao muhimu. Ofisi hiyo hiyo ya Mhamasishaji , kando ya kesi hiyo, ilionesha “kushukuru kwa mazungumzo ya kawaida kati ya pande zote, shutuma na utetezi”, wakati huo huo ikisema kuwa ina uhakika wa ukweli wa uchunguzi uliofanywa na nyaraka zilizopatikana.

Katika mikutano ya kesi zilizofanyika hadi sasa, Mahakama ya mji wa Vatican imeonesha na hata kuipigia mstari  mweusi na mweupe katika mojawapo ya sheria zake, nia ya kuhakikisha heshima ya haki ya utetezi na kwa ujumla zaidi, mchakato unaotarajiwa.  Kanuni moja ya  mwisho kutekelezwa na Vatican na sheria ya tarehe 11 Julai  2013, iliyowekwa rasmi miezi michache baada ya kuanza kwa Papa wa sasa, ambayo ni sehemu ya sheria ya sasa(Oltretevere). Ni katika mantiki hasa ya kudhamini kesi ya haki, na ndani yake haki ya utetezi, kwamba Mahakama , kufuatia pingamizi la ubatili lililoombwa na watetezi, juu ya shaka ya tafsiri ya sheria, na maombi katika hatua hii pia iliyopokelewa na mashtaka yaleyale ya umma , alirudisha hati kwa Msimamizi wa Haki ili aweze kutoa maswali ya kukosekana kwa mshtakiwa. Kama inavyojulikana, Mahakama pia iliamuru Nhamasishaji  aweke hati zote alizo nazo; kama vile rekodi za sauti na video za mahojiano ya watuhumiwa na mashahidi, yaliyofanywa na vyombo ambavyo kwa hakika sheria ya 1913 haikuweza kutafakari.

Ofisi ya Mhamasishaji ilisema kwamba, kwa kuzingatia masharti ya Mahakama ya tarehe 6 Oktoba, Ofisi yake ilitoa utaratibu wa uwasilishaji kamili wa rekodi zote za sauti na video za mahojiano hayo na kwa hiyo “nyaraka zote ambazo ni chanzo cha ushahidi zinaweza kupatikana katika hukumu.” Mhamasishaji huyo (Promota) pia alieleza, kuhusiana na mapungufu yaliyopo katika baadhi ya sehemu za ripoti za mahojiano, kwamba “zinahusu taarifa zisizohusika” na mchakato huu na kwamba wamewekewa “mahitaji ya usiri kwa sababu ni mada ya uchunguzi huru wa  shughuli katika mashauri mengine.”

Kwa sasa Mahakama, kama alivyotamka Rais wakati wa kikao kimoja, inasubiri upande wa mashtaka uelezee misimamo ya baadhi ya washtakiwa kwa kufutwa kazi au kwa ombi jipya la wito. Na mhamasishaji wa Haki ametangaza kuwa shughuli hii itaisha katikati ya mwezi  Januari 2022, na maamuzi ya matokeo yatachukuliwa. Katika hatua hiyo na baada ya maamuzi yote juu ya tofauti nyingine zilizoundwa na watetezi, yale ambayo Mahakama bado haijatoa uamuzi, yamechukuliwa kwa maana moja au nyingine itawezekana kuanza mjadala wenye sifa za kesi zote na hivyo kuingia katikati ya awamu ya kesi ili kuweza kuchuja kupitia wingi wa hati na hati zinazounda mfumo wa mashtaka.

23 December 2021, 15:14