Tafuta

Kard.Parolin kuhusu “kufuta”:sio namna ya kupambana na ubaguzi

Katika mahojiano na Vyombo vya habari Vatican News,Katibu wa Serikali ya mji wa Vatican,Kardinali Parolin akichambua hati ya Kamati ya Ulaya ambayo ililikuwa inaalika kutotumia neno au maneno ya Kuzaliwa kwa Bwana,Maria au Yohane,alisema:“Anayekwenda dhidi ya ukweli anajiweka katika hatarini”.Hata hivyo baadaye Kamati hiyo imeondoa suala hilo ambalo limeleta mjadala mkubwa sana.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Katika maoni ya Kardinali Piero Parolin Katibu wa Vatican, mara baada ya kuchapishwa katika Hati moja ya ndani ya Tume ya Ulaya ambayo ilikuwa na madhumuni ya kuzuia ubaguzi na kukaribisha kujumuishwa amesema: “Kwa bahati mbaya, tabia ni kusawazisha kila kitu, bila kujua jinsi ya kuheshimu tofauti sahihi, mwishowe kuna hatari ya kumwangamiza mtu”. Katika mwongozo wa mawasiliano, wanaaalika wapendekee zaidi usemi: “kipindi cha siku kuu”,  badala ya kusema “kipindi cha kuzaliwa kwa Bwana”. Kiukweli, ili kuhakikisha haki ya kila mtu kutendewa kwa usawa maneno kama vile “Bi” “Bibi” yanafutwa, lakini pia Kuzaliwa kwa Bwana na majina kama vile “Maria” au “Yohane”. “Hatupigi marufuku matumizi ya neno Kuzaliwa kwa Bwana,” alisema msemaji wa Tume ya Ulaya.

Kwa maana hiyo katika maoni ya Kardinali Parolin kuhusu tukio hili , Yeye anaamini kuwa wasiwasi wa kufuta ubaguzi wote ni sawa. Ni njia ambayo imepatikana ufahamu zaidi na zaidi na ambayo bila shaka lazima pia kutafsiriwa katika uwanja wa vitendo. Walakini, kwa maoni yake, hii sio njia ya kufikia lengo hili. Kwa sababu katika mwisho kuna hatari ya kuharibu, kuangamiza mtu, katika njia kuu mbili. Ya kwanza ni ile ya upambanuzi ambao ni sifa ya ulimwengu wetu, tabia kwa bahati mbaya ni kubishana kila kitu, bila kujua jinsi ya kuheshimu hata tofauti zinazofaa, ambazo bila shaka hazipaswi kuwa upinzani au chanzo cha ubaguzi, lakini lazima ziunganishwe kwa usahihi ili kujenga ubinadamu kamili na fungamani.

Ya pili Kardinali amebainisha kuwa ni kusahau kile ambacho ni ukweli. Na yeyote anayekwenda kinyume na ukweli anajiweka katika hatari kubwa. Na baadaye kuna kufutwa kile amcha ni mizizi, hasa kuhusu sikukuu za Kikristo, mwelekeo wa Kikristo pia wa Ulaya nzima. Bila shaka, Kardinali amsema kuwa tunajua kwamba Ulaya inadaiwa kuwepo kwake na utambulisho kwa michango mingi, lakini kwa hakika haiwezi kusahau kwamba moja ya mchango mkuu, ikiwa sio moja mkuu tu, ilikuwa yaUkristo wenyewe. Kwa maana hiyo, kuharibu tofauti na kuharibu mizizi inamaanisha kuharibu mtu.

Kardinali akifafanua kuhusu ziara ya Papa ambaye kwa hakika anakwenda kukutana na tamaduni na thamani ambazo zinahusu makaribisho ambayo yanajumuisha ujenizi wa Ulaya ambayo inataka kufuta mizizi yake kwa maoni yake amesisitiza kuwa ni kweli kwamba Papa, hata katika ujumbe kwa  njia ya video aliohutubia Ugiriki na Cyprus kabla ya kuondoka kwake, siku chache zilizopita, amesisitiza hasa mwelekeo huu wa Ulaya: ambayo ni, kwenda kwenye vyanzo vya Ulaya, na baadaye  kugundua tena ni vipengele gani vya msingi. Hakika, utamaduni wa Kigiriki ni mojawapo ya vipengele hivi. Baadaye  Papa pia anaitaja Cyprus kama mojawapo ya chipukizi cha  Ulaya cha  Ardhi Takatifu. Kwa maana hiyo inaonekana kwake kuwa safari hii imefika kwa wakati ufaao, ni safari ambayo inawaalika  wote kurudi kwenye vipimo hivi msingi ambavyo haviwezi kufutwa. “Ni lazima tugundue upya uwezo wa kuunganisha ukweli huu wote bila kuupuuza, bila kupigana nao, bila kuuondoa na kuuweka pembeni”,alisistiza Kardinali Parolin Katibu wa Vatican.

01 December 2021, 09:11