Barua ya Papa kwa wenzi wa ndoa:Gambino anasema ni mafundisho ya Baba mwema
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Papa Francisko Dominika tarehe 26 Desemba 2021 katika sherehe ya Familia Takatifu ya Nazareti ya Yesu, Maria na Yosefu akiwakilisha barua yake kwa wenzi wa Ndoa alisema: "Ni zawadi moja ya Noeli kwa ajili yenu wenzi wa ndoa, kwa kuwatia moyo, kuwa ishara ya ukaribu na fursa ya kutafakari”. Ni mandishi ambayo yanafika baada ya mwaka mmoja tangu mnamo tarehe 27 Desemba 2021, wakati mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana alitangaza mwaka wa “Famiglia Amoris laetitia”. Ni mchakato wa njia iliyojaa matunda na yenye alama ya huruma ya Baba ambayo inafanywa kwa upya katika "maandishi ya 'Magisterium', au mafundisho. Amesema hayo Bi Gabriella Gambino katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, katika mahojiano na Vatican News kufuatia wa uchapishwaji wa Barua ya Papa Fracisko. Bi Gambini amefafanua jinsi alivyo shangazwa na huruma iliyosikia ya sauti ya upendo ambao Baba Mtakatifu amependa kuelezea kwa familia katika wakati huu mgumu ambao bado unatawaliwa na janga la kiafya. Leo hii kuna familia nyingi ambazo zinaishi kwenye mgogoro na matatizo ya kila aina ambayo Papa Francisko anayatooa umakini wake kama baba. Bi Gambini aidha ameshangazwa kwa namna ya pekee ya umakini alio nao Papa kuhusu sakramenti ya ndoa. Uzofu wa zawadi hiyo ambayo leo hii amesisitiza ni mgumu sana kufanya ueleweke kwa vijana na ambao kuna uwepo wa Kristo ambaye anaishi katika familia, katikati ya maisha yao ya kila siku.
Bi Gambino akiendelea na ufananusi wa kujibu maswali hayo amesisitiza kuwa “Ni umakini wa hali ya juu na ajabu, ambapo Papa anaingia katika maisha yetu ya kila siku, katika mienendo ya familia, karibu kutushika mkono ili kututia moyo na sio tu lakini ni kutufanya tusijisikie peke yetu katika safari hii. Na anawasihi vijana waweze kuoa, watumainie katika neema inayowawekeza wanandoa, ambayo huwadumisha katika maisha yao yote katika dhamana ya ndoa, hata katikati ya dhoruba”. Kimsingi, Papa anawakumbusha wenzi wa ndoa kwamba: “Kama Wakristo hatuwezi kukataa kupendekeza kwa vijana wazo bora la ndoa, yaani ule mpango wa Mungu katika ukuu wake wote. Kutofanya hivyo kutakuwa ni ukosefu wa upendo wa Kanisa kwa vijana. Kuelewa hali za kipekee kamwe haimaanishi kuficha nuru ya ubora kamili, au kupendekeza chini ya kile ambacho Yesu anatoa kwa mwanadamu. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anatukumbusha hili katika waraka wa Amoris laetitia yaani furaha ya upendo ndani ya familia".
Barua hiyo imefika baada ya mwaka mmoja kamili tangu wakati huo mnamo tarehe 27 Desemba 2020, ambapo Papa alipotangaza mwaka wa Familia, ikiwa ni kuenzi miaka mitano baada ya kuchapishwa kwa Wosia wa Kitume wa Amoris laetitia. Bi Gambino amesisitiza kuwa mara baada ya kuchapishwa huko walianza haraka shughuli za familia kichungaji katika ulimwengu mzima”. Baada ya miaka 5 ya tafakari na makabiliano ya mafundisho ya Kanisa, hatua imefanyika na Baraza lao likihimizwa na Baba Mtakatifu limeweza kufafanua nyenzo nyingi za kichungaji ili kusaidia majimbo na mabaraza ya Maaskofu katika kutafsiri Waraka wenyewe kwa njia ya matendo na ubunifu wa kichungaji. Pia kwa kuzingatia matazamio ya Mkutano wa ulimwengu ambao utafanyika baada ya miezi 6, tangu sasa, Barua kutoka kwa Papa kwa wenzi wa ndoa ni andiko muhimu sana la mafundisho juu ya familia, ambalo parokia na majimbo wataweza kutumia ili kuandaa familia kwa ajili ya Mkutano huo, kwa kutafakari pamoja na familia: jinsi familia ilivyo na jinsi leo hii, katikati ya matatizo mengi, kama Mtakatifu Yohane Paulo II alivyosema, inaweza kuwa yenyewe! Kwa maana hiyo, kiukweli Bi Gambino ameawaalika jumuiya nzima na parokia zote kusoma barua hiyo na kuitafakari majumbani mwao, huku wakipendekeza na kuisambaza kwa wanandoa wengine wa pande zote za dunia.
Bi Gambino akiendelea na ufafanuzi wake juu ya matunda ambayo yamekuwa mazuri kwa mwaka huu amesema, bila shaka na kwa ujumla, kumekuwapo na mipango mingi ambayo ulimwengu unajulisha Baraza lao la kipapa la Walei , Familia na Maisha, na yote ambayo hayajawafikia tangu Papa alipowapatia huo msukumo. Parokia nyingi, majimbo, mabaraza ya maaskofu, hata shule na vyuo vikuu vinawaandikia kuwalezea kile ambacho wanafanya ili kuitikia wito wa Baba Mtakatifu, kwa kusindikiza familia, wanandoa, katika hali tete zaidi, kwa miunganiko mipya, ambayo Bwana anazidi kutafutwa. Mchakato wa ubunifu wa kichungaji umeanzishwa ambao unapelekea pia ushirikiano mkubwa zaidi, katika mazingira mengi, kati ya wachungaji na familia, ili kujifunza kusikilizana wao kwa wao, pia kuimarisha nafasi za familia na wanandoa katika Kanisa. kwa mujibu wa Bi Gambino hatahivyo hafikchi kusema kwamba mchakato huo sio rahisi, lakini kila mahali wanahisi shauku ya kufanikiwa, kujaribu kuelewa jinsi ya kutembea pamoja na pia kusindikiza na hali ngumu zaidi, ambazo hapo awali ziliachwa kando kidogo. Familia ni wema kwa ajili ya Kanisa, lakini uthibitisho huo katika miktadha mingi bado haijaelewa jinsi ya kuitafsiri katika vitendo, amesisitiza.
Akijibu swali jinsi ya kuandaa tukio la mkutano wa familia ulimwenguni 2022 katika kuhitimisha mwaka wa Familia, Bi Gambino amesema kuwa Wosia wa Amoris laetitia, ndio kiongozi ambao unawaongoza kuelekea katika Mkutano wa Ulimwengu na ambao unawaomba wafanye mang’amuzi juu ya mtindo na jinsi ya kutoa huduma zao za kichungaji inavyotakiwa na ambavyo Baba Mtakatifu anawaalika sasa kujikita katika safari hii ya sinodi ya Kanisa kwa njia ya muungano, ushiriki na utume wa kila mjumbe wa Watu wa Mungu, na hii ikiwa ni pamoja na familia zote. Wachungaji na familia pamoja, chini ya uongozi wa Roho mtakatifu. Na jinsi gani ya kufanya lakini? amesema ingependeza, kwa mfano, katika wakati huu wa safari ya sinodi na wakati ule ule wa matayarisho ya Mkutano wa Ulimwengu, kujaribu kuchanganya mchakato wa mang’amuzi ya kikanisa pia kuanzia na uhusiano wa Kanisa na familia, kwa kujiuliza baadhi ya maswali tofauti kidogo na yale ambayo yamezoeleka. Kwa mfano: ni jinsi gani familia inaweza kusaidia Kanisa kuwa la sinodi zaidi?
Je, Kanisa linaweza kujifunza nini kutokana na njia ya kifamilia ambayo imajulikana ya kupambanua, kusikiliza na kukaribisha? Kanisa linaweza kujifunza nini kutokana na jinsi wazazi, watoto, ndugu hujaribu kupendana kwa udhaifu wao, na mazingira magumu yao, migogoro na mitazamo tofauti? Maswali haya na mengine yanaweza kufungua njia mpya ya kufikiri juu ya uchungaji, kwa njia ya mtindo tofauti, kwa ushirika thabiti zaidi kati ya familia na Kanisa. Si hivyo tu, bali wangeanzisha hata mchakato mpya wa kufanya mang’amuzi ambayo, baada ya kuhitimishwa kwa Mkutano wa Familia ulimwenguni na Mwaka wa Familia wangeweza kuendeleza angalau hadi kufikia Sinodi, ikawa ndiyo kuendeleza chachu ya huduma ya kichungaji ya familia duniani kote.