Tafuta

Mheshimiwa sana Padre Gélase Armel Kema wa Jimbo Katoliki la Ouesso ameteuliwa na Papa Francisko kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Ouesso Jamhuri ya Congo Brazzaville. Mheshimiwa sana Padre Gélase Armel Kema wa Jimbo Katoliki la Ouesso ameteuliwa na Papa Francisko kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Ouesso Jamhuri ya Congo Brazzaville. 

Askofu Gélase Armel Kema Jimbo Katoliki la Ouesso, Congo Brazzaville

Askofu mteule Gélase Armel Kema alizaliwa tarehe 26 Oktoba 1972. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kipadre, tarehe 29 Agosti 1999 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu wakati huo amewahi kuwa Paroko, Gambera wa Seminari, Makamu wa Askofu na Paroko. Hadi kuteuliwa kwake alikua ni Mkurugenzi wa Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa Kitaifa, PMS. Ni jaalimu wa Sheria.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu Yves-Marie Monot, C.S.Sp. wa Jimbo Katoliki la Ouesso la kutaka kung’atuka kutoka madarakani. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteuwa Mheshimiwa sana Padre Gélase Armel Kema wa Jimbo Katoliki la Ouesso kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Ouesso Jamhuri ya Congo. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteule Gélase Armel Kema alikuwa ni Mkurugenzi wa Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa Kitaifa. Askofu mteule Gélase Armel Kema alizaliwa tarehe 26 Oktoba 1972. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kipadre, tarehe 29 Agosti 1999 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu wakati huo amewahi kuwa Paroko-usu, Gambera wa Seminari, Makamu wa Askofu na Paroko.

Tangu mwaka 2007 hadi mwaka 2010 alitumwa na Jimbo kujiendeleza zaidi kwa masomo ya juu na kufanikiwa kutunukiwa Shahada ya uzamivu katika Sheria za Kanisa kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana kilichoko mjini Roma. Kati ya Mwaka 2010 hadi mwaka 2013 alifanya utume kwenye Parokia ya Collesalvetti, Jimbo Katoliki la Livorno, Italia. Kati ya Mwaka 2014 alikuwa ni Jaalimu wa Sheria za Kanisa, Seminari kuu ya Kardinali Emile Biayenda. Na tangu mwaka 2018 hadi kuteuliwa kwake, Askofu mteule Gélase Armel Kema alikuwa ni Mkurugenzi wa Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa Kitaifa nchini Jamhuri ya Congo.

Uteuzi
08 December 2021, 16:21