Papa:Mazungumzo kati ya watu wa dini tofauti ni kudumisha urafiki amani na maelewano
Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.
Kila tarehe 16 Novemba ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Stahamala au kuvumiliana iliyoanzishwa na Shirika la elimu,sayansi na utamaduni, la Umoja wa Mataifa (UNESCO). Kwa njia hii Umoja wa Mataifa unatumia fursa ya siku hii kueleza kuwa sitahamala si suala la kuvumiliana tu kwa sababu ya kutofautiana bali ni utayari wa kuheshimu na kukubali watu wengine kwa kuzingatia hali sawa za binadamu.Mara nyingi utangamano au mchanganyiko wa watu kutoka maeneo tofauti ni aina ya mfumo wa utajiri na si sababu ya kuleta mgawanyiko. Baba Mtakatifu Francisko katika fursa ya siku hii kwenye ujumbe mfupi kupitia mtandao wa kijamii ameandika kuwa "mazungumzo kati ya watu wa dini tofauti hayawezi kufanyika tu kwa njia za kidipolasia, utafadhali au kuvumiliana. Lengo kuu la mazungumzao ni kudumisha urafiki, amani, maelewano na kushirikishana thamani za uzoefu wa kimaadili na kiroho katika roho ya ukweli na upendo".
Kutovumilia mara nyingi ni sawa na ujinga na hofu. Hali hizi za kihisia zinatokana na kujifunza kwa kuiga tangu umri mdogo; kwa maana hiyo ni lazima kuwa na umakini mkubwa wa elimu ya uvumilivu na haki za binadamu. Juhudi kubwa zaidi zinahitajika ili kueneza thamani kubwa za mshikamano kwa watoto. Hii ni kwa sabababu watoto na vijana wanapaswa kuwaangaliwa na wengine kwa udadisi na kufungulia ulimwengu kwa sababu amani haipatikani kwa njia ya chuki. Na bila amani hakuna wakati ujao kwa yeyote kati yetu. Katika hili Papa Francisko mara nyingi amekuwa akikaribisha kuwa na ujasiri wa watu wengine na kusema kuwa: “Ikiwa tunaamini kuwepo kwa familia ya kibinadamu, basi ni lazima ihifadhiwe. Kama ilivyo katika kila familia, hii hutokea zaidi ya yote kupitia mazungumzo ya kila siku na yenye ufanisi. Inakisia utambulisho wa mtu mwenyewe, ambao mtu hapaswi kuuacha ili kumfurahisha mwingine.
Lakini wakati huo huo maombi kwa ajili ya kuwa na ujasiri wa wengine, ambayo inahusisha utambuzi kamili wa mwingine na uhuru wake na dhamira ya matokeo ya kutumia mwenyewe ili haki zake msingi daima zithibitishwe, kila mahali na kwa mtu yeyote. Kwa sababu bila uhuru sisi si watoto tena wa familia ya kibinadamu, bali watumwa. Miongoni mwa uhuru papa amesisitiza ule wa kidini. Sio tu kwa ajili ya uhuru wa ibada peke yake, lakini kiukweli kuona kuwa ndugu mwingine, mwana wa ubinadamu mwenyewe ambaye Mungu anamwacha huru na ambaye kwa maana hiyo hakuna taasisi ya kibinadamu inayoweza kulazimisha, hata kwa jina lake (Hotuba ya Abu Dhabi, 4 Februari 2019).