Tafuta

2021.09.28 Padre  Pozzoli  mwenye asili ya Italia akiwa mmisionari nchini  Argentina alimbatiza Papa Francisko 25 Desemba 1936. 2021.09.28 Padre Pozzoli mwenye asili ya Italia akiwa mmisionari nchini Argentina alimbatiza Papa Francisko 25 Desemba 1936. 

Kard.Sandri amekuwa Lod katika uwakilishi wa kitabu kuhusu Padre Pozzoli

Rais wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki amekubali mwaliko wa Askofu wa Lodi Maurizio Malvestiti na ametoa ushuhuda wake juu ya sura ya msalesiani aliyezaliwa katika Kata ya Senna Lodigiana na kutoa huduma yake ya kichungaji ambapo mnamo tarehe 25 Desemba 1936 alimabatiza mtoto mchanga Jeorge Bergoglio.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Kardinali Leonardo Sandri, Rais wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashriki alishiriki tarehe 15 Novemba 2021 mchana huko Senna Lodigiana, Wilaya ya Lodi, katika uwakilishi wa Kitabu cha Ferruccio Pallavera  kiitwacho “Ho fatto cristiano il Papa”,  yaani nilimfanya Papa kuwa Mkristo”, ambacho kimecapishwa na nyumba ya vitabu Vaticana. Kitabu kinahusu masuala ya mwanadamu na tasaufi ya Padre mmoja wa Kisalesiani Enrico Pozzoli, mzaliwa wa kata ndogo ya Lodigiano, Italia aliyeondoka kama mmisionari kwenda nchini Argentina mnamo 1904 na kumbatiza mtoto mchanga Jorge Mario Bergoglio huko Buenos Aires (yaani Papa Francisko) mnamo tarehe 25 Desemba 1936.

Kardinali Sandri alikubali mwaliko huo kutoka kwa Askofu wa Lodi Maurizio Malvestiti, ambaya aliwahi kuwa Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki na kupeleka ushuhuda wake juu ya sura ya Padre Pozzoli, ambaye amemfanya amkumbuke kwa mambo mengi hasa yanayohusu mchakato wa wito wake, familia yake uhamiaji hata yeye nchini Argentina kutoka Italia, maeneo mbali mbali na watu ambao aliwajua huko Buenos Aires.

Kwa namna ya pekee, katika hotuba yake alipitia mchakato wa simulizi ya kitabu ambacho kieleza  maisha ya Padre Pozzoli na yale ya familia ya Bergoglio (yaani papa Francisko) wakiwa wahamiaji nchi Argentina na hatua za kwanza za ukristo wa kijana Jorge Mario, hadi kufikia uchaguzi wa kuingia katika seminari. Kardinali Sandri alifika huko Lodi Jumamosi jioni na kuadhimisha misa ya Dominika katika Kanisa la Monasteri ya Watawa wa ndani Wakarmeli. Mwisho wa liturujia hiyo alikutana na wanajumuiya hiyo ya kimonaki na kuzungumza nao kuhusu hali halisi ya Makanisa ya mashariki na kuhusiana na ziara yake ya hivi karibuni nchini Siria mahali ambapo aliadhimisha hata misa katika Monasteri ya Wakarmeli wa Aleppo. Mchana alikwenda katika Parokia ya Senna Lodigiana, mahalia ambapo alibatizwa Padre Pozzoli na mara baada ya kutambulishwa na Askofu wa Lodi, Kardinali Sandri aliwakilisha utangulizi wa kitabu hicho.

16 November 2021, 15:44