Tafuta

Katika mchakato wa Sinodi ni kujifunza wakati wa kuiishi na uzoefu na kwa kuishi sinodi na wote kwa kusikiliza na kufanya mang'amuzi. Katika mchakato wa Sinodi ni kujifunza wakati wa kuiishi na uzoefu na kwa kuishi sinodi na wote kwa kusikiliza na kufanya mang'amuzi. 

Kard.Grech:Kanisa la kisinodi linatamani kuwa na huruma isiyoisha!

Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Sinodi ya Maaskofu ametoa hotuba yake katika Mkutano wa kwanza wa Kanisa la Amerika ya Kusini na Visiwa vya Carribien,kwa kuangazia zaidi tabia halisi ya mchakato wa sinodi katika jumuiya za mabara:“Tangu Mtaguso wa II wa Vatican na kuendelea kazi yenu imekuwa ya kutembea pamoja”.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Kutembea kwa pamoja kwa namna ya kisinodi ndiyo asili ya tasaufi ya Kanisa la Amerika ya Kusini kama ilivyoagizwa na Baba Mtakatifu Francisko ambaye sasa analiomba kila Kanisa ulimwenguni kutembea pamoja. Imeonesha historia na kuunganishwa kutoka “Medellín, Puebla, Santo Domingo, Aparecida” pia Kardinali  Mario Grech ambaye ameitambua kwamba wao wametoa ushuhuda wa uzoefu wao maalum wa umoja wa kikanisa ambao wameishi,na wanaweza kweli kuwa mfano kwa mabaraza mengine mengi ya maaskofu. Amesema hayo huto Mkuu wa Sekretarieti ya Sinodi ya maaskofu katika Mkutano wa kwanza wa Kikanisa wa Bara la Amerika ya Kusini na Caribbien ambao unaendelea hadi tarehe 28 Novemba 2021 na kuwakilisha tabia za ulimwengu zinzoongoza mchakato wa Sinodi akiunganisha na zile za utamaduni wa Kanisa la Bara hilo la Amerika Kusini.

Kardinali Grech,Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu akitoa hotuba yake kwa washiriki wa Mkutano wa kwanza wa kikanisa
Kardinali Grech,Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu akitoa hotuba yake kwa washiriki wa Mkutano wa kwanza wa kikanisa

Baada ya Mkutano wa Aparecida, Sinodi kuhusu Amazonia na uzoefu ndani mwake na utambulisho wa jumuiya za Amerika ya Kusini inaonesha wazi jinsi ambavyo Kardinali Grech alivyo weza kupata fursa ya kuelezea kiini na Kanisa la watu wa Mungu kwa namna ambayo Papa Francisko analitaka Kanisa linalipaswa kutoka nje. Amenukuu kifungu cha  Wosia wa  Evangelii Gaudium, anapozungumza juu ya nafasi kuu ya kimisionari ya Kanisa, kwa namna ya pekee ya Kanisa linalotoka nje  na mahali ambamo mitume wake wanaitwa kufanya hivyo kwa kusindikiza, kutoa matunda na kusheherekea. Haya ni mambo ambayo kiukweli ni tabia ya jumuiya ya kuinjilisha na kufaa zaidi katika jumuiya iliyo kwenye mchakato wa sinodi, kwa mujibu wa Kardinali Grech.

Mpango kama huo unazaliwa kutokana na kwamba Kanisa ambalo linataka kuwa la kisinodi linatenda bila kuogopa kwenda kwenye njia panda ili kuwaalika waliobaguliwa vile vile kwa sababu hiyo Kanisa la kisinodi linatamani kuwa na huruma isioisha.  Kwa kufanya hivyo inategemea na utashi wa huduma na ishara za maisha ya kila siku kwa wengine, kwa kufupisha umbali na kuinama hadi unyenyekevu ikiwa unahitajika. Usindikizwaji unawalenga binadamu wote na kwa michakato yake yote, hata kama ni migumu na ya muda mrefu inawezekana kwa sababu ni Kanisa la Sinodi, amesisitiza Kardinali Grech. Kwa kuongezea amesema binadamu anajua nini maana ya kazi ngumu na uvumilivu wa kiutume. Na pia jumuiya ya kisinodi inatambua jinsi gani ya kupata matunda kwa sababu ya utunzaji wa ngano bila kupoteza amani kwa sababu ya kuibuka kwa magugu mabaya.  Hatimaye Jumuiya ya kisinodi daima inatambua namna ya kufanya sherehe. Inaadhimisha kwa kila ushindi mdogo, kila hatua fupi mbele ya mchakato wa kisinodi katika uzuri wa liturujia.

Washiriki wa Mkutano wa kwanza wa kikanisa wa bara la Amerika Kusini
Washiriki wa Mkutano wa kwanza wa kikanisa wa bara la Amerika Kusini

Kwa hakika katika mchakato wa Sinodi, ni kujifunza wakati wa kuiishi na uzoefu na kwa kuishi sinodi, wakati huo huo ni wamisionari. Katibu Mkuu wa Sinodi, ametoa mfano kwamba Kanisa moja la Sinodi mbalo Unjilishaji wake unataka kuwa wa kibinafsi, wa makundi yanayojitegemea, kwa misingi ya ujuzi binafsi na taaluma, ingekuwa ni kinyume cha utume ambao unazaliwa na umoja wa kanisa ambalo lisingekuwa na ukweli wa utangazaji wa Injili. Mpango wa kimisionari unaweza kuzaliwa tu kutokana na mchakato wa sinodi ya kusikiliza, kufanya mang’amuzi na ambayo zaidi ya hatua hizo ni zoezi la mfuasi.  Kutafakari uhusiano kati ya nafasi muhimu ya Kanisa, inaweza kuwa moja ya mchango wenye maana katika Mkutano huo na safari ya mchakato wa Sinodi ya Makanisa ya Bara la Amerika ya Kusini na visiwa vyake vya Caraibi, ameelekeza Kardinali Grech.

Lakini ikiwa tangu Mtaguso wa II wa Vatican na kuendelea kwa namna ya pekee wa mtindo wa kutembea pamoja umekuwa sehemu ya kidunia katika mchakato wa kisinodi sisi sote ni wanafunzi “na wote mmekuwa hivyo kwa siku nyingi kwa kuwa mliweza kuhifadhi taalimungu ya watu wa Mungu”. Kanisa la Amerika ya Kusini hata hivyo kwa miaka 30 katika eneo hilo wanaishi hali ngumu kama inavyofafanulia na kitabu maarufu akilinganisha na” joho lililochanika”.   Kwa upande wa Kardinali Grech amesema kwamba haitawezakana kuwana uogofu wa kimisionari ikiwa hawatapyaishi uongofu wa kisinodi, ambao unapelekea usikivu mnyenyekevu na heshima ya mwingine na hoja zake; ambapo lazima kuwa na ujasiri wa kuomba na kutoa msamaha; unaotaka kuwa na umoja na si gharama ya ukweli, lakini usiojitambulisha ukweli wangu, bali ukweli.  Kwa mujibu wa kardinali amethibitisha kuwa labda hii itakuwa ngumu sana lakini ambayo itajenga hata ushuhuda wa nguvu. Hata katika hali ya uzushi wa madhehebu mbali mbali, ambayo yanakuza ufahamu wa ubinafsi na wa ndani wa imani. Umoja, sinodi, vitakuwa jibu la kuaminika zaidi. Sio wimbo wa upamoja, wenye noti zinaofanana na sauti moja, lakini,(Sauti) ambayo kila sauti, kila rekodi, kila mlio wa sauti unaboresha Injili moja, inayoimbwa kwa uwezekano usio na kikomo wa tofauti, amehitimisha Kardinali Grech.

Washiriki wa Mkutano wa kwanza wa kikanisa wa bara la Amerika Kusini
Washiriki wa Mkutano wa kwanza wa kikanisa wa bara la Amerika Kusini
26 November 2021, 15:33