Masuala makuu yanayohusu tamaduni nyingi za wanafunzi na walimu na muktadha wake uliomo na mitindo ya mafunzo yanayotolewa katika Vyuo Vikuu vya Kipapa na katika nyumba za malezi za maisha ya wakfu. “ Masuala makuu yanayohusu tamaduni nyingi za wanafunzi na walimu na muktadha wake uliomo na mitindo ya mafunzo yanayotolewa katika Vyuo Vikuu vya Kipapa na katika nyumba za malezi za maisha ya wakfu. “ 

Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniana:Kongamano kuhusu tamaduni nyingi katika malezi

Mnamo 17 hadi 19 Novemba limefanyika Kongamano la Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana na mada:“Jumuiya za utamaduni mwingi katika malezi yapi?“Utofauti huwa unatisha kidogo kwa sababu unahatarisha usalama unaopatikana na kuondoa utulivu uliopo.Tukikabiliwa na tofauti za kiutamaduni,kikabila,kisiasa na kidini,tunaweza kuwa na mitazamo miwili:kujifunga binafis au kujifungulia wengine"(Papa Francisko).

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Kongamano la Kimataifa la kila mwaka la Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana lililofanyika katika chuo kikuu chini ya mamlaka ya Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu kuanzia tarehe 17 hadi 19 Novemba 2021, liliongozwa na mada: “Jumuiya za kiutamaduni kwa ajili ya malezi gani? Kongamano hilo liliwezekana kuhudhuriwa kwa kufuata kanuni za kupambana na Covid-19, kwa uwep wa watu na hata kufuatilia mtandaoni, kwa tafsiri ya wakati mmoja katika lugha mbali mbali ambapo liliwaona washiriki, watafiti na wasomi kutoka Australia, Ubelgiji, Chile, Kolombia, Ujerumani, Ghana, India, Ireland, Italia, Msumbiji, Hispania na Marekani.

KONGAMANO LA CHUO KIKUU URBANIANA

"Utofauti huwa unatisha kidogo kwa sababu unahatarisha usalama unaopatikana na kusababisha utulivu uliopatika. (...) Tukikabiliwa na tofauti za kiutamaduni, kikabila, kisiasa na kidini, tunaweza kuwa na mitazamo miwili, kwanza kujifunga wenyewe kwa utetezi mkali wa kile kinachoitwa utambulisho wetu au tujifungulia ili kukutana na wengine na kukuza pamoja ndoto ya jumuiya ya kidugu". Ndivyo  Baba Mtakatifu Francisko  alisema wakati wa ziara yake ya Kitume huko Budapest, mnamo tarehe 12 Septemba 2021, wakati wa kuadhimisha misa Takatifu ya kuhitimisha Kongamano la 52 la Ekaristi Takatifu Kimataifa chini Hungaria ambalo liliongozwa na kauli mbiu “Visima vyangu vyote vimo kwako” Zab. 87:7, na ambapo Kongamano hili limepa msukumo wake.

Kongamano la chuo Kikuu Urbaniana kuhusu mada hiyo kwa maana hiyo lilikusudia kutoa uchambuzi na uelewa unaowezekana wa kile kinachotokea katika jumuiya za malezi ambapo wanaofunda na watu walio katika malezi wanatoka kwa watu, mataifa na tamaduni tofauti. Nguvu hiyo kwa hakika inapatikana leo hii katika vyuo vikuu vya kipapa, katika taasisi za mafunzo katoliki na katika vituo vya mafunzo ya watawa wa kike na kiume. Katika Kongamano hilo liwasilishwa hata matokeo ya utafiti wa kijamii,  kielimu na kianthropolojia uliofanywa kuanzia mwaka 2017 hadi leo hii na Taasisi Juu ya Katekesi na Tasaufi ya Kimisionari, ya Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana, kwa ushirikiano na  Umoja wa Mama wakuu wa Mashirika (UISG) kuhusu “tamaduni nyingi, mafunzo na uwezo wa kiutamaduni katika vyuo vikuu vya kipapa na katika malezi ya maisha ya waliokwa wakfu”.

Kwa kupanua majadiliano na kubadilishana mawazo wakati wa siku hizo za Kongamano ratiba ya  Kongamano ilizingatia masuala makuu yanayohusu tamaduni nyingi za wanafunzi na walimu na muktadha wake uliomo na mitindo ya mafunzo inayotolewa katika Vyuo Vikuu vya Kipapa na katika nyumba za malezi ya  katika maisha ya  wakfu. “Ikiwa tamaduni nyingi ni ukweli wa jamii zetu nyingi na hasa mazingira ya malezi ya Kanisa Katoliki,ndilo lilikuwa dokezo kutoka Chuo Kikuu cha Urbaniana ambacho kilituma taarifa zake katika Shirika la Habari za Kimisionari Fides kuwa utamaduni mwingi, kubadilishana na mabadiliko ya pamoja, bado ni upeo unaotazamwa kwa udadisi au wasiwasi, changamoto ya kielimu ambayo inawahusu hasa wanaofunda na kwa hivyo na watu wanaofunzwa”. Ujuzi wa tamaduni nyingi na ustadi wa taaluma mbalimbali kwa maana hiyo ni  mustakabali wa mapatano ya elimu ya kimataifa, kwa mtazamo wa ujenzi shirikishi wa mtu fungamani  na wa jamii ya dada na kaka.

24 November 2021, 14:04