Tafuta

Askofu mkuu Franco Coppola ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Ubelgiji. Askofu mkuu Franco Coppola ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Ubelgiji. 

Askofu Mkuu Franco Coppola Balozi wa Vatican nchini Ubelgiji

Askofu mkuu Franco Coppola alizaliwa kunako tarehe 31 Machi 1957 huko Maglie, nchini Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 12 Septemba 1981 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Kunako mwaka 1993 akajiunga na utume wa Kidiplomasia mjini Vatican na kubahatika kufanya utume wake nchini Lebanon, Burundi, Colombia, Poland na hatimaye Vatican.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Franco Coppola kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Ubelgiji, kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Coppola alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Mexico.  Amewahi pia kuwa Balozi wa Vatican nchini Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati na hivyo kushiriki kuandaa hija ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Afrika ya Kati, tukio ambalo limeacha chapa ya kudumu kwa familia ya Mungu nchini humo, kwani Baba Mtakatifu Francisko akiwa Jimbo kuu la Bangui aliweza kufungua Lango la Maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu kwa mara ya kwanza katika historia ya Kanisa, tukio kama hili kufanyika nje ya Vatican. Hii ni Jubilei iliyozinduliwa rasmi tarehe 8 Desemba 2015 na kuhitimishwa rasmi tarehe 20 Novemba 2016, Sherehe ya Kristo Yesu Mfalme wa Ulimwengu.

Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Franco Coppola alizaliwa kunako tarehe 31 Machi 1957 huko Maglie, nchini Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 12 Septemba 1981 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Kunako mwaka 1993 akajiunga na utume wa Kidiplomasia mjini Vatican na kubahatika kufanya utume wake nchini Lebanon, Burundi, Colombia, Poland na hatimaye Vatican. Tarehe 16 Julai 2009 Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu mkuu na hatimaye kumweka wakfu kuwa Askofu mkuu hapo tarehe 12 Septemba 2009. Tangu wakati huo amekuwa ni Balozi wa Vatican nchini Burundi, Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati na Chad pamoja na Mexico. Tarehe 15 Novemba 2021 ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Ubelgiji!

Ubelgiji
17 November 2021, 15:17