Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Jonas Benson Okoye kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Nnewi, Nigeria Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Jonas Benson Okoye kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Nnewi, Nigeria 

Askofu Jonas Benson Okoye Jimbo Katoliki Nnewi, Nigeria

Askofu Jonas Benson Okoye alizaliwa tarehe 25 Januari 1964, huko Kaduma, nchini Nigeria. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi tarehe 29 Agosti 1992 akapewa Daraja takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Awka. Papa, tarehe 30 Mei 2014 akamteua kuwa Askofu msaidizi wa jimbo Katoliki la Awka Nigeria na hatimaye, akaweka kuwa Askofu tarehe 29 Agosti 2014.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu Hilary Paul Odili Okeke wa Jimbo Katoliki la Nnewi la kutaka kung’atuka kutoka madarakani. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Askofu msaidizi Jonas Benson Okoye kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Nnewi nchini Nigeria. Hadi kuteuliwa kwake alikuwa ni Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Awka, Nigeria. Itakumbukwa kwamba, Askofu Jonas Benson Okoye alizaliwa tarehe 25 Januari 1964, huko Kaduma, nchini Nigeria.

Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi tarehe 29 Agosti 1992 akapewa Daraja takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Awka. Baba Mtakatifu Francisko tarehe 30 Mei 2014 akamteua kuwa Askofu msaidizi wa jimbo Katoliki la Awka Nigeria na hatimaye, akaweka kuwa Askofu tarehe 29 Agosti 2014. Tarehe 9 Novemba 2021, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Awka Nigeria. 

Uteuzi Nigeria
09 November 2021, 17:16