Tafuta

2021.10.18 Uzindunduzi wa Manesho yanahusiana na uhusiano kati ya Serbia na Vatican. 2021.10.18 Uzindunduzi wa Manesho yanahusiana na uhusiano kati ya Serbia na Vatican. 

Vatican na Serbia kati ya 1878-1914:Maonesho ya hati na picha huko Roma

Asili na maendeleo ya uhusiano kati ya sehemu mbili:Vatican na Serbia hadi kufikia saini ya mkataba wa mnamo 1914.Limezinduliwa pango hifadhi la maonesho ya Serikali ya Seribia katika Chuo Kikuu cha Laterano,Roma.Askofu Mkuu Gallagher ameeleza juu ya ushirikiano wa pamoja na utafutaji wa wema wa pamoja ambao unaongoza mafunzo ya historia ya uhusiano kimataifa.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa mahusiano na ushirikiano na Nchi ametoa hotuba yake katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Laterano, katika fursa ya uzinduzi wa Maonesho ya “Serba na Vatican 1878-1914 iliyoandaliwa na Taifa la Serbia kwa uwepo wa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Jamhuri ya Seribia Bwana Nikola Selaković. Katika hotuba yake ni matumaini yake  kuwa mafunzo yanayoendelea ya Historia ya uhusinao wa kimataifa yanaweza kweli kuigwa na kupendwa na kizazi kipya ili wachangie kujenga jamii yenye tabia daima ya kushirikiana na utafutaji wa wema wa pamoja.  Katika hotuba hiyo Askofu Gallagher alisisitiza zaidi kile ambacho alikiita masuala ambayo mara nyingi ni nyeti na magumu ya mahusiano kati ya Vatican na watu wa nchi za mashariki ya Ulaya na ambayo licha ya hayo yote hayakokoma kuwa na umuhimu wake unaoendelea na mkubwa katika ujumla wake kisiasa na kidini.

Askofu Mkuu Gallagher aidha amekumbuka kipindi  cha kati ya mwisho wa Karne ya XIX na mwanzo wa Karne ya XX ambacho kilikuwa na magumu sana yanayo husiana na kimataifa wakati iwe kwa upande wa Belgrando na hata Vatican walikuwa wakitafuta kuboresha uhusiano wao, kwa kukabiliana  na changamoto nyingi zilizotokana na tofauti za sera za kisisa na kidini. Askofu Mkuu pia amegusia juu ya Saini ya mwaka 1914 ambayo hata kama haikuweza kufanya mengi hasa katika matendo na wala kufikia malengo yaliyokusudiwa, lakini amesema kuwa ilichangia kwa kiasi kikubwa ukarabati na kurudisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya Makao makuu Vatican na Ufalme wa wakati ufalme wa Serbia, Croatia na Slovenia mnamo 1920, wakati ulipozindulia hata Ubalozi wa kitume wa Vatican  huko Belgrado.

Kuthamanisha mahusiano ya nchi zote mbili ambayo yana mzizi tayari katika mwisho wa 1800 na kuonesha mchakato wa kihistoria ambao ulipelekea ujenzi na baadaye mandeleo ya Serikali ya Serbia, hakikisho tangu mwanzo wa uhuru wa kidini na ibada una asili yake, kama alivyoeleza Srdjan Miljkovic, Makamu wa Utume wa Kidiplomasia wa Serbia anayewakilisha nchi jijini Vatican. Katika kueleza hayo amegusia baadhi ya vipindi muhimu vya kihistoria vinavyoonesha kwa njia za hati mbali mbali zilizohifadhiwa katika pango la Serikali ya Serbia. Ni matumaini yake kwamba maonesho haya yataweza kuongeza nguvu zaidi kwa ajili ya mahusianp mema yaliyopo kati ya Vatican na nchi ya Serbia.

19 October 2021, 16:26