Tafuta

Rais Frank Walter Steinmeier wa Ujerumani tarehe 25 Oktoba 2021 amekutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko Rais Frank Walter Steinmeier wa Ujerumani tarehe 25 Oktoba 2021 amekutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko 

Rais Frank W. Steinmeier Akutana na Papa Francisko Mjini Vatican

Katika mazungumzo yao, Baba Mtakatifu pamoja na mgeni wake, wamegusia masuala ya siasa za ndani nchini Ujerumani. Baadaye wamejielekeza katika masuala ya wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji; baadhi ya migogoro na vita katika medani za Kimataifa sanjari na umuhimu wa Jumuiya ya Kimataifa kuhakikisha kwamba, inapata suluhu ya matatizo na changamoto hizi pevu!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

 

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 25 Oktoba 2021 amekutana na kuzungumza na Rais Frank Walter Steinmeier wa Ujerumani ambaye baadaye amekutana na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa mjini Vatican.

Katika mazungumzo yao, Baba Mtakatifu pamoja na mgeni wake, wamegusia masuala ya siasa za ndani nchini Ujerumani. Baadaye wamejielekeza zaidi katika masuala ya wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji; baadhi ya migogoro na vita katika medani za Kimataifa sanjari na umuhimu wa Jumuiya ya Kimataifa kuhakikisha kwamba, inapata suluhu ya matatizo na changamoto zote hizi, ili kudumisha haki, amani na maridhiano kati ya watu!

Rais wa Ujerumani
25 October 2021, 14:57