Tafuta

2021.10.08 Bwana  Robert Abela Waziri Mkuu wa Malta amekutana na Papa Francisko. 2021.10.08 Bwana Robert Abela Waziri Mkuu wa Malta amekutana na Papa Francisko. 

Papa amekutana na Waziri Mkuu wa Malta Bwana Abela

Waziri Mkuu wa Malta amekutana na Papa Francisko ambaye mara baada ya Mkutano amekutana na Katibu wa Vatican akiambatana na katibu wa Vatican wa Mahusiano na ushirikiano wa Nchi.

Ijumaa tarehe 8 Oktoba 2021, Papa Francisko amekutana na Waziri Mkuu wa Malta Robert Abela na baadaye akakutana na Kardinali Pietro Parolin, katibu wa Vatican, akiambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusianao na ushirikianio na Nchi.

Katika mazunguzmo yao na Katibu Mkuu, wamethibitisha uhusiano mzuri kati yao na ushirikiano mwema kati ya Kanisa na serikali. Vile vile wamezungumzia juu ya mchango wa ukristo katika historia, utamaduni na maisha ya watu wa Malta na jitihada za Kanisa kwa ajili ya maendeleo ya binadamu na kijamii katika Nchi hasa katika uwanja wa Elimu na kiafya.

Mkutano wa Papa na Waziri Mkuu wa Malta
Mkutano wa Papa na Waziri Mkuu wa Malta

Pamoja na hayo wametazama mantiki ya pamoja ambayo inahusu uhamiaji ambao unaona juhudi kubwa ya Kanisa na serikali na baadhi ya masuala ya kimaadili Wakiendelea na mazungumzo hayo pia wamegusia hali ya Ulya na kimataifa kwa kwa namna ya pekee umakini wa dini katika enelo la Kimediterania na zaidi umuhimu wa mazungumzo ya kiekumene na kidini katika ujenzi wa amani na udugu kati ya watu.

Mkutano wa Papa na Waziri Mkuu wa Malta
Mkutano wa Papa na Waziri Mkuu wa Malta
08 October 2021, 16:12