Mkutano wa Papa na Kansela Angela Merkel
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu, Alhamisi tarehe 7 Oktoba 2021, asubuhi alikutana na Kansela wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Angela Merkel, ambaye baadaye alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akiambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na ushirikiano na Mataifa.
Katika mazungumzo yao wameonesha kupongezana juu ya mahusiano mema yaliyopo kati ya nchi hizi mbili na matunda ya ushirikiano kati ya Vatican na Ujerumani kwa mujibu wa maelezo ya Msemaji wa vyombo vya habari Vatican.
Baadaye amegusia masuala yanayowahusu wote katika muktadha wa kimataifa na kikanda, wamejikita kuona fursa za kuzindua kwa ushirikiano kwa ajili ya kukabiliana na mgogoro mkubwa unaoendelea kwa namna ya pekee juu ya matokeo mabaya ya dharurua ya kiafya na uhamiaji.
Katika kubadlishana zwadi, Papa Francisko ametoa zawadi ya Picha ya shaba inayoonesha Mlango mtakatifu, Kitabu kikubwa chenye mkusanyo wa hati za Papa, Ujumbe wa Amani ya Mwaka na Hati juu ya Udugu wa Kibinadamu. Na zawadi kwa upande wake Kansela wa Ujerumani Merkel, amempatia Papa Tafakari ya Injili za Dominika za vitabu vitatu, Kitabu kikubwa cha Michelangelo na bidhaa nyingine za vyakula.