Tafuta

2021.10.20 Uwakiisho wa kitabu 'Siate autentici!' cha  Ary Waldir Ramos Diaz 2021.10.20 Uwakiisho wa kitabu 'Siate autentici!' cha Ary Waldir Ramos Diaz 

'Muwe halisi' ni kitabu cha mawasiliano na mtindo wa Papa

Ni nini maana ya mawasiliano ya Papa Francisko na yeye anawasilianaje? Je wahudumu wa mawasiliano wanawezaje kuvutia mfano wake katika zoezi lao la kitaaluma? Kitabu kilichowakilishwa katika Makao ya Radio Vatican kinatafuta kujibu maswali hayo na mengine.Maneno yaliyo ndani mwake ni kama udhati,usahihi,usikivu na ukina.Kati ya watoa mada yupo hata Kardinali Mario Grech,Katibu Mkuu wa Sinodi ya maaskofu.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

'Muwe wa kweli'  ndiyo kichwa cha habari cha kitabu cha mwanandishi na mtaalam wa masuala ya Vatican kilichochapishwa na toleo la Kanisa na kuwakilishwa Jumanne tarehe 19 Oktoba 2021 katika makao makuu ya Radio Vatican. Udhati ni tabia ya Papa Francisko katika kuwasilisha na ambapo katika kitabu kinapendekeza kutathimini maneno na ishara za kwa kipindi cha miaka  8 ya upapa wake. Yapo baadhi ya maneno ambayo Papa Francisko anarudia mara nyingi na ambayo sasa yamekwisha enea kwa mfano, neno la upole, huruma, kuanza michakato zaidi ya kuchukua nafasi au kufanya mangan’amuzi, vita ya tatu vilivyogawanyika vipande vipande, mzungumzo, huduma, usikivu, matumaini na mengine mengi.

Na kuna ishara nyingi ambazo zimetimizwa na Papa Francsiko na ambazo kwa walio wengi wetu, haziwezi kusahauliwa. Ni nani ambaye anaweza kusahau Papa anaosha miguu kwa wafungwa wakati wa Alhamisi kuu, kwa kupiga magoti na kubusu miguu ya viongozi wa Sudan Kusini akiwaomba wafanye kazi kwa ajili ya amani ya  nchi yao; au bembelezo aliowapatia watoto wengi na wazee, walemavu na waathiriwa wa biashara ya binadamu. Lakini pia hata picha ya Papa akiwa anapanda ngazi ya za ndege mkononi mfuko  wake na kushukwa kwa urahisi akiwafikia watu mahali walipo wanamsubiri kuwasalimia.  Papa Francisko anatamani kuwasiliana na anajua kuwa kuwasiliana lazima kuguse akili na moyo wa mtu. Mara nyingi kuna hisia na kuleta hisia kali.

Mratibu wa uwakilishi wa kitabu hicho alikuwa ni Dk. Alessandro Gisotti, makamu mhariri wa Vyombo vya habari Vatican, Kardinali  Mario Grech, Katibu mkuu wa Sinodi ya Maaskofu; Eva Fernández, Mwakilishi kwa ajili ya Italia na Vatican ya Radio Cope; Jesús Colina, Makamu rais wa Mtandao Katoliki wa  Aleteia, na mwandishi wa kitabu mwenyewe. Kichwa kidogo cha kitabu ni Na Papa Francisko kwa ajili ya kuboresha uhusiano wetu na uwasiliano wetu.Katika kitabu chake, mwandishi wa kitabu hicho Ramos Diaz amekabiliana na mawasilino na Papa kwa namna ya kuwasiliana katika nyakati hizi baada ya ukweli. Na anatoa mifano ambayo inasisitiza vipimo vitatu vya msingi katika mawasiliano yake kwa mfano  ukina, kusikiliza na, hasa, uhalisi, vitu vinavyoonesha kuunda madaraja kati ya watu, hata mbali au tofauti, kwa lengo kuu la mawasiliano yake.

Ary Waldir Ramos Diaz
Ary Waldir Ramos Diaz

Kuelewa mawasiliano ya Papa Francisko kunamaanisha kukaribia siri ya mawasiliano shirikishi, yaliyojaa maadili, yaliyo jaa uwazi kwa utofauti na uundaji wa jumuiya, anaandika katika utangulizi mwandishi ambaye anachambua mawasiliano yasiyo ya maneno na ya binafsi ya Papa kupitia ushuhuda wa watu waliokutana naye katika maisha yao kama vile waamini, wasioamini Mungu, washirika, marafiki, watu wa taasisi au mashahuda  rahisi . Lengo la kitabu  tena kwa maneno ya mwandishi, ni kumsaidia msomaji kuchukua,  hatua kwa kufuata mfano wa Baba Mtakatifu Francisko, ile njia ya ukuaji wa binafsi na kijamii (...) Mchakato wa njia wa kuvunja kuta za kutojali, kuwa na wasiwasi, shauku na kuboresha uhusiano kati ya watu. Kwanza, Papa anaamini kuwa mawasiliano ni mazungumzo na mtu aliye mbele, hata ikiwa ana umati mbele yako.

Naye Kardinali Grech wakati wa hotuba amejikitia kwa mada kusikiliza.  Kwa mujibu wame ameeleza kuwa mawasiliano mazuri yanaweza kutokana na kusikiliza. Haishangazi kwamba Papa alitaka kuanza safari ya sinodi hasa kwa kuanzia na kuwasikiliza watu wa Mungu. Lakini inamaanisha nini kusikiliza? Katibu mkuu wa Sinodi amekumbuka kuwa tayari katika Wosia wa Evangelii gaudium, Papa Francisko anaandika kuwa kusikiliza ni zaidi ya kusikia. Na anasema: kusikiliza ni sanaa, zoezi sio la akili tu bali pia la moyo. Sio kitendo tu, ukosefu wa maneno. Inamaanisha kuchukua mtazamo wa upatikanaji wa yule mwingine ambaye ni zawadi kwangu. Kusikiliza kwa hivyo kunamaanisha kutoa nafasi kwa mwingine, ukiacha ubaguzi. Ni kuondoa  kila kitu kinachotufanya tuwe viziwi. Katika msingi wa kusikiliza, Kardinali Grech amesisitiza kuwa kila wakati kuna uhusiano na hutoa usawa. Kardinali ametaja visa vikubwa vya unyanyasaji ambavyo sio sio nadra kwa mfano kwa unyanyasaji wa mwili na kisaikolojia unaoteseka, mateso mengine yanaongezwa kwa mwathiriwa. Lakini lile neno ambalo linaumiza kuliko kuponya ni neno ka kutotaka kusikiliza. Mwishowe, ametaja tena juu ya  Sinodi ambayo imeanza hivi karibuni, ambayo inaweza kuwa wakati mzuri wa kuponya vidonda vingi ambavyo  Kanisa linabeba, na kama jamii na kama wanadamu. “ Tusaidie kumsikiliza kila mtu hasa wale ambao wanaishi pembezoni, wale ambao walijeruhiwa na Kanisa, viziwi na bubu, ambaye anasubiri sikio na moyo ulio tayari kusikiliza”, amehitimisha.

Kwa upnde wa Eva Fernández kitabu kuhusu “Kuwa halisi!” ni njia isiyo na kifani ya kushughulikia mawasiliano ya Papa na mwandishi wa habari amezingatia dhamana yake kama huduma inayotilia mkazo maneno matatu: zawadi, kazi na ukarimu. Anathibitisha kuwa mawasiliano ya Papa ni zawadi kwetu sisi sote kwa sababu inatusaidia kuelewa Injili na kuifanya iwe ya kuvutia kwetu. Zawadi ya neno pia ni muhimu kwa kutoa thamani nzuri kwa mawasiliano. Lakini hii inahitaji kazi, kwa sababu inahitaji maandalizi, amesisitiza Fernández kuwa Papa  anaweka nguvu zake zote katika mawasiliano yake. Kufanya kama yeye inahitaji ujasiri, lakini pia unyenyekevu, kusisitiza ujumbe zaidi kuliko kwa yeyote aliyeuchukua. Mwishowe, ukarimu, ambao pia unamaanisha kujua kwamba unabeba hatari kwa kuwasiliana kwa ujasiri. Na hii Papa anajua vizuri, amehitimisha.

Ary Waldir Ramos Diaz
Ary Waldir Ramos Diaz

Hatimaye katika uwakilishi huo yalikuwa ni maneno ya mwandishi wa kitabu, Ary Waldir Ramos Diaz ambaye amependa kusema kwamba kitabu kiitwacho “Kuwa halisi!” kimezaliwa kutoka kwa wote na ambacho ni matokeo ya kazi ya pamoja na bado inasisitiza umuhimu wa uthabiti ambao pia unamaanisha kuzuia zile dhambi za taaluma ya mwandishi wa habari iliyooneshwa na Baba Mtakatifu Francisko yaani ile ya upotoshaji, kashfa na kugushi. Mawasiliano halisi yanahitaji uvumilivu na ujasiri, lakini itatusaidia kubomoa kuta na shukrani kwa uthabiti, tutaaminika, amehitimisha.

20 October 2021, 11:06